Kaimu
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Richard
Mayongela (kushoto) akimkabidhi funguo ya gari, Kamishna Jenerali wa
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Tanzania, Thobias Andengenye katika hafla
iliyofanyika janao kwenye Kituo cha Zimamoto cha Kiwanja cha Ndege cha
Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam.
Kamishna
Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Tanzania, Thobias Andengenye
akiwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania
(TAA), Bw. Richard Mayongela wakiwa katika picha ya pamoja na maafisa wa
kikosi hicho na menejimenti ya TAA.
Gari
aina ya Toyota Hilux alilokabidhiwa Kamishna Jenerali wa Jeshi la
Zimamoto na Uokoaji Tanzania, Thobias Andengenye na Kaimu Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Richard
Mayongela litakalotumiwa na Kamanda wa Kikosi cha ZImamoto na Uokoaji wa
Viwanja vya Ndege Tanzania, Christom Manyoroga.
Kaimu
Mkuu wa Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani cha Mamlaka ya Viwanja vya Ndege
Tanzania (TAA), Bi. Irene Sikumbili (kushoto) akiagana na Kamishna
Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini, Thobias Andengenye
jana baada ya kukabidhiwa gari litakalotumiwa na Kamanda wa kikosi cha
Zimamoto cha Viwanja vya Ndege Tanzania. Wengine kulia ni Mkuu wa Idara
ya Manunuzi na Ugavi Bw. Mtengela Hanga na (katikati) Mkuu wa Idara ya
Udhibiti Viwango Bw. Paul Rwegasha.
Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw.
Richard Mayongela (kulia) akiagana na makamanda wa kikosi cha zimamoto
na Uokoaji baada ya kukabidhi gari jana.
MAMLAKA
ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) jana imekabidhi gari aina Toyota
Hilux kwa Idara ya Zimamoto na Uokoaji ya Kiwanja cha Ndege cha
Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), ili kuchocheo ufanisi wa kazi.
Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa TAA, Bw. Richard Mayongela akikabidhi gari hilo
katika hafla fupi iliyofanyika jana katika Kituo cha Zimamoto na Uokoaji
cha JNIA, alisema litasaidia usafiri wa haraka kwenye matukio kwa
Kamanda wa Zimamoto wa Viwanja vya Ndege Tanzania, Kamishna Msaidizi,
Christom Manyoroga, ambaye awali alikuwa na gari kuukuu.
Bw.
Mayongela alisema kuwa gari hilo lenye thamani ya zaidi ya Sh milioni
80, mbali na kusaidia usafiri wa haraka kwenye matukio ya ndani ya
kiwanja na nje endapo watatakiwa kutoa msaada, pia litasaidia shughuli
mbalimbali za zimamoto na uokoaji.
Alisema
Zimamoto ni miongoni mwa taasisi kubwa inayofanya kazi na TAA, hivyo ni
jukumu la mamlaka kuhakikisha wanawezeshwa kwa vifaa na vitendea kazi
ili waweze kufanya kazi kwa weledi.Pia Bw. Mayongela alisema mbali na
msaada ya gari hilo TAA itatoa fedha kiasi Sh milioni 120 kwa ajili ya
kuwapatia mafunzo wafanyakazi wa vituo vya Zimamoto vya viwanja vya
ndege, ili weaweze kwenda na mabadiliko yanayotokea duniani.
“Mafunzo
haya kwa askari wa Zimamoto ni muhimu sana ukizingatia hawa wanatumia
mitambo haya magari hakuna wazimamoto wengine wanaoweza kutumia zaidi
hawa wa viwanja vya ndege, hivyo wanahitaji kwenda na wakati na
kujifunza mambo mapya, kwani wapo waliopata mafunzo kwa muda mrefu na
wengine hawajapata mafunzo kabisa,” alisema Bw. Mayongela.Aliongeza
…“TAA itaendelea kudumisha ushirikiano baina yao na kwa karibu zaidi na
idara Zimamoto na uokoaji,”.
Naye
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Tanzania, Thobias
Andengenye, aliishukuru TAA kwa msaada wa gari hilo, ambalo litachochea
ufanisi mkubwa wa kazi wa askari kwa kuwa Mkuu wao atakuwa na usafiri wa
kumfikisha maeneo mbalimbali.
Alisema
viwanja vya ndege ndio lango kuu la kuingilia wawekezaji na watalii,
ambapo kuimarisha idara hiyo kutasaida kutimiza lengo la Tanzania ya
Viwanda na kufikia malengo ya mwaka 2025 kuwa na viwanda
vitakavyowekezwa na wawekezaji wazawa na wageni kutoka nje ya nchi.
Kamishna
Jenerali Andengenye alisema bila usalama wawekezaji na watalii
watashindwa kuingia nchini kwa kuogopa usalama wao na mali zao.
No comments:
Post a Comment