Katibu
Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhandisi Mussa Iyombe amewaasa watendajii
wa mkoa wa Manyara kuchukua hatua stahiki zinazohusu masuala ya
watumishi ili kupunguza au kuondoa migogoro mkoani Manyara.
Katibu
Mkuu Mhandisi Iyombe ameyasema hayo mjini Babati wakati akiongea na
watendaji na watumishi wa Mkoa wa Manyara, Halmashauri ya Mji Babati na
Halmashauri ya Wilaya Babati kwamba kiwango kikubwa cha migogoro hasa ya
ardhi mkoani humo inatokana na baadhi ya watendaji kutotimiza wajibu
wao ipasavyo hali wakizingatia sheria na taratibu za nchi.
“migogoro
mingi inaanzia Sight (sehemu wanazotwaa ardhi ili kupima) kwa kuleta
taarifa iliyo na mapungufu na pia zingatieni sheria za ardhi, migogoro
ipungue kwa kwa kutenda”
Pia
Mhandisi Iyombe amesema wapo Watendaji ambao wanashindwa kutumia Mamlaka
waliyopewa na kuzuia migogoro ya ardhi ambayo inazuilika lakini pia
amehoji mbona mipaka ya mikoa na wilaya ipo wazi na kwanini sehemu
nyingine za kiutawala, “msilazimishe migogoro ya ardhi kwani tumewapa
mamlaka kwa kufanya Ugatuaji wa madaraka (D by D) hivyo amueni”
Akipokea
taarifa ya elimu kuhusu kuwashusha vyeo walimu wakuu zaidi ya 250,
ametoa angalizo kuwa mamlaka na Uongozi wa mkoa mzima unapaswa
kushauriana katika masuala mbalimbali kama hilo la elimu kabla ya
kuchukua maamuzi magumu ambayo hayajafanyiwa utafiti wa kina kwani
yanaleta athari kiutendaji na kisaikolojia kwa watumishi. Mhandisi
Iyombe amewataka watendaji wa mkoa kuepuka suala la kuwa na Maafisa
wengi wanaokaimu hali sheria zipo wazi kwani kufanya hivyo kunapunguza
hamasa ya utendaji na kuongeza gharama zisizo za lazima.
“suala
la kukaimu lisizidi miezi sita ili kuboresha utendaji, kwanini
Halmashauri zingine wanakaimu hadi miaka mitatu” amewataka kufuata
sheria za kazi ili kupunguza hoja zisizo na msingi.Kwa upande wake Kaimu
Katibu Tawala wa Mkoa Misaile Mussa amesema mkoa wa manyara una
upungufu wa watumishi wapatao 6644 kwa mkoa mzima ambapo watumishi 2,076
wapo Halmashauri ya wilaya ya Babati.
Lakini
pia mkoa unakabiliwa na Maafisa wengi wanaokaimu kuanzia ngazi ya mkoa
na Halmashauri za mkoa huo.Naye Mkuu wa wilaya ya Babati, Mhe.Raymond
Mushi amesema kuwa changamoto ya upatikanaji wa maji na hasa ya
miundombinu ya kupeleka maji na pia mipaka ya wilaya ya Babati na
Monduli, na Babati na Kondoa anaendelea kufuatilia kuona mipaka halisi
mahali ilipo.
Katibu
Mkuu Mhandisi Mussa Iyombe yupo katika ziara ya kikazi ya siku mbili
mkoani Manyara ambapo leo hii ameongea na watumishi hali akisikiliza
kero zao na kuzitolea majibu papo hapo na kesho atatembelea miradi ya
maendeleo kujionea jinsi inavyotekelezwa
Katibu
Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhandisi Mussa Iyombe akiongea na
watumishi wa Halmashauri ya Babati na Babati Mji katika ukumbi wa
Halmashauri ya wilaya Babati wakati wa ziara yake.
Katibu
Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhandisi Mussa Iyombe akiongea na
watumishi wa Halmashauri ya Babati na Babati Mji katika ukumbi wa
Halmashauri ya wilaya Babati wakati wa ziara yake.
Baadhi
ya Wakurugenzi wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
(OR TAMISEMI) walioshiriki ziara ya Katibu Mkuu OR TAMISEMI Mha. Mussa
Iyombe wakiwa katika chumba cha mikutano Babati.
Katika
picha ya pamoja ni Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhandisi Mussa
Iyombe na Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara Misaile Mussa
wakisikiliza taarifa ya Halmashauri ya Mji Babati
Baadhi
ya watumishi wa ofisi ya Mkoa wa Manyara, Babati Mji na Halmashauri ya
Wilaya Babati wakimsikiliza Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhandisi
Mussa Iyombe alipokuwa akiongea nao mjini Babati.
Katibu
Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhandisi Mussa Iyombe alipowasili katika
ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya Babati kuongea na watumishi .
No comments:
Post a Comment