Waziri
wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto)
akizungumza na wadau wa ngumi (hawapo pichani) kuhusu mchakato wa
kukamilisha rasimu ya katiba ya kusimamia mchezo wa ngumi nchini maara
baada ya kukabidhiwa jana jijini Dar es Salaam,kulia kwake ni Msajili wa
Vyama vya Michezo Nchini kutoka Baraza la Michezo la Taifa Bw. Ibrahim
Mkwawa.
Katibu
Mtendaji Baraza la Michezo la Taifa Bw.Mohamed Kiganja (kulia) akitoa
taarifa kuhusu mchakato wa kuundwa kwa rasimu ya katiba ya mchezo wa
ngumi kwa Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison
Mwakyembe (kushoto) kabla ya makabidhiano ya rasimu hiyo jana jijini Dar
es Salaam,wapili kulia ni Msajili wa Vyama vya Michezo Nchini kutoka
Baraza la Michezo la Taifa Bw Ibrahim Mkwawa.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Kuunda rasimu ya Katiba ya kusimamia mchezo wa Ngumi
nchini Bw.Emmanuel Salehe akikabidhi rasimu ya katiba hiyo kwa
Mheshimiwa Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison
Mwakyembe () jana jijini Dar es Salaam katikati ni Katibu Mtendaji
Baraza la Michezo la Taifa Bw.Mohamed Kiganja.
Mmoja
wa wanakamati waliyoandaa rasimu ya Katiba ya kusimamia mchezo wa ngumi
Bw.Ally Champion akitoa maoni yake na kuwasihi wadau wangumi kuacha
tofauti zao za vikundi vyao waungane kwa lengo la kuimarisha mchezo
wangumi kwa taifa jana katika mkutano wa kukabidhi rasimu hiyo kwa
Mheshimiwa Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison
Mwakyembe (hayupo pichani).
Baadhi
ya wajumbe waliyoandaa rasimu ya Katiba ya kusimamia mchezo ngumi
wakiwa katika picha ya pamoja na Mheshimiwa Waziri wa Habari Utamaduni
Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (wanne kulia)mara baada ya
kumkabidhi rasimu hiyo jana jijini Dar es Salaam,watatu kulia ni
Mwenyekiti wa Kamati ya Kuunda rasimu hiyo Bw.Emmanuel Salehe na watatu
kulia ni Katibu Mtendaji Baraza la Michezo la Taifa Bw.Mohamed Kiganja.
Waziri
wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto)
akimsikiliza bondia wa kike Bi.Feriche Mashauri (kulia) alipokuwa
akimweleza changamoto za mchezo wa ngumi nchini jana jijini Dar es
Salaam baada ya Waziri kukabidhiwa rasimu ya mchezo wa ngumi .
……………………………………………………………………………………
Na Anitha Jonas – WHUSM-Dar es Salaam
Waziri
wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe
ameipongeza Kamati iliyoandaa rasimu ya katiba ya mchezo wa ngumi nchini
kwa kumaliza kazi hiyo kwa wakati.
Mheshimiwa
Mwakyembe ametoa kauli hiyo alipokuwa akikabidhiwa rasimu ya katiba
hiyo jana jijini Dar es Salaam mara baada kukamilika kwa kuandaliwa
kwake na kamati maalum iliyokuwa na wajumbe 13 wakuteuliwa ambao
walifanya kazi ya kuzunguka kwa wadau wa ngumi na kukusanya maoni.
“Nitateuwa
watu wasaba kutoka katika kamati hii iliyounda rasimu watakao uungana
na Baraza la Michezo la Taifa kuboresha rasimu hii ili tuweze kuitisha
kikao kikubwa cha wadau wote wa mchezo wa ngumi na tuweze kuipitisha
rasimu hii,”Dkt.Mwakyembe.
Akiendelea
kuzungumza katika makabidhiano hayo Waziri Mwakyembe alieleza kuwa
ataendelea kupokea maoni ya wadau hao ndani ya miezi mitatu kwa
kuzingatia sheria ili kufanikisha kikao cha kupitisha rasimu hiyo
ambacho kitaitishwa kwa mujibu wa sheria ili kufanikisha lengo la
kuboresha sekta ya mchezo wa ngumi nchini.
Pamoja
na hayo waziri huyo alisisitiza kuwa na mapema wiki ijayo atamuagiza
Katibu Mtendaji Baraza la Michezo la Taifa Bw.Mohamed Kiganja kutangaza
wajumbe atakao kuwa amewateuwa kuungana na BMT katika kuboresha rasimu
hiyo.
Akizungumza
katika sherehe za makabidhiano ya rasimu hiyo ya katiba ya kusimamia
mchezo wa ngumi nchini Mwenyekiti wa Kamati hiyo Bw.Emmanuel Salehe
alieleza kuwa pamoja na kukamilisha rasimu hiyo kamati hiyo iliunda pia
kanuni za kusimamia mchezo wa ngumi kwa lengo la kuhakikisha misingi
imara inawekwa katika kuboresha sekta ya mchezo huo.
Kwa
Upande wa Katibu Mtendaji Baraza la Michezo la Taifa Bw. Mohamed Kiganja
alisema kuwa ofisi yake iko tayari kuungana na wajumbe watakaoteuliwa
na Mheshimiwa Waziri kukamilisha mchakato wa kuboresha rasimu hiyo kabla
ya kupitishwa.
Pamoja
na hayo naye bondia wa zamani aliyekwisha kushinda katika mikanda ya
kimataifa Bw.Rashid Matumla alitoa maoni yake pamoja na kuipongeza
serikali kwa kufanya maamuzi ya kuunda chombo imara kitakacho simamia
mchezo wa ngumi kwa kuzingatia sheria tofauti na awali huku akiwasihi
wadau wangumi kuacha tofauti zao na kuangalia suala la msingi kuboresha
mazingira ya mchezo huo na kuufanya uwe na tija kwa zaidi pamoja na
kuondoa mazingira yenye utata katika uendeshaji wa mchezo huo.
No comments:
Post a Comment