Wakati Tanzania ikiendelea kujikita katika kukuza uchumi kupitia sekta ya utalii, zaidi ya washiriki kutoka nchi 50 duniani wamekutana mkoani Arusha kushiriki Maonesho ya Kimataifa ya Karibu-KiliFair yanayolenga kufungua masoko mapya na kuongeza idadi ya watalii wanaotembelea nchi
Maonesho hayo yanakuja wakati serikali ikiendelea kutekeleza mikakati mbalimbali ya kuitangaza Tanzania katika masoko ya kimataifa na kuimarisha mazingira ya uwekezaji katika sekta ya utalii
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa maonesho hayo, Mkurugenzi wa Idara ya Utalii, Bi. Theresa Mugobi, aliyemwakilisha Waziri wa Maliasili na Utalii, alisema serikali imeweka mkazo katika kuboresha miundombinu ya utalii, huduma za ukarimu na viwango vya utoaji huduma ili kuifanya Tanzania kuwa miongoni mwa nchi zinazovutia zaidi watalii duniani
Alisema pamoja na kuendeleza masoko ya jadi, serikali pia inaelekeza nguvu katika kufungua masoko mapya barani Afrika, Asia, Ulaya, Mashariki ya Kati na Amerika ili kuongeza ushindani wa Tanzania katika soko la utalii duniani
Kwa mujibu wa waandaaji wa Karibu-KiliFair, maonesho hayo yameendelea kuwa daraja muhimu linalowaunganisha wanunuzi wa huduma za utalii, wawekezaji na waendeshaji wa safari kutoka mataifa mbalimbali
Mkurugenzi Mwenza wa Karibu-KiliFair, Dominic Shoo, alisema ongezeko la washiriki kutoka mataifa mbalimbali ni ishara kuwa Tanzania imeendelea kujijengea heshima kama kitovu muhimu cha biashara ya utalii katika ukanda wa Afrika Mashariki
Aliongeza kuwa ushirikiano kati ya serikali na sekta binafsi utaendelea kuwa nguzo muhimu katika juhudi za kuitangaza Tanzania na kuongeza mchango wa utalii katika uchumi wa taifa
Karibu-KiliFair imeendelea kuwa moja ya maonesho makubwa zaidi ya utalii katika Afrika Mashariki, yakitoa nafasi kwa wadau kutangaza vivutio vya utalii, kujenga mitandao ya biashara na kuibua fursa mpya za uwekezaji ndani ya sekta hiyo.

.jpeg)

.jpeg)
.jpeg)

.jpeg)

Post a Comment