*Polisi yaendelea kuchunguza kifo cha Akwilina,waua majambazi Dar
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
JESHI
la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, limesema linamshikilia mwanamke
mmoja na mwanaume mmoja kwa tuhuma za kuhusishwa na mauaji ya kada wa
Chadema Daniel John aliyekutwa amekufa maeneo ya Coco Beach jijini.
Akizungumza
leo, Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam Lazaro Mambosasa amesema
kutokana na uchunguzi unaendelea kuhusu mauaji hayo huko maeneo ya
Hananasifu Kinondoni wamefanikiwa kuwakamata watu wawili.
Amesema
majina ya watu hao yamehifadhiwa kwa lengo la kutoharibu uchunguzi
unaoendelea kuhusu tukio hilo la mauaji ya kada huyo wa Chadema.
UCHUNGUZI KIFO CHA AKWILINA WAENDELEA
Wakati
huohuo, Kamanda Mambosasa amesema bado wanaendelea na uchunguzi wa
tukio la mauaji ya aliyekuwa mwanafunzi wa mwaka wa kwanza katika Chuo
cha Usafirishaji Akwilina Akwiline aliyefariki dunia baada ya kupigwa
risasi.
Mambosasa
amesema bado wanaendelea kuchunguza tukio hilo ambalo limegusa hisia za
watu wengi na baada ya kukamilisha uchunguzi wao watatoa taarifa kwa
umma ili ujue.
WAKAMATA SILAHA TANO, RISASI 35
Pia
Mambosasa amesema Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam kwa takriban
wiki mbili sasa wamekuwa wakifanya operesheni ya kukamata wahalifu
wanaojihusisha na matukio ya ujambazi wa kutumia silaha katika maeneo
mbalimbali jijini.
Amesema
maeneo ya Pugu alikamatwa mtu mmoja aitwaye Peter Kwema a.k.a Babu na
alipohojiwa alikiri kujihusisha na matukio ya ujambazi katika mikoa ya
Dar es Salaam,Morogoro,Arusha,Tanga na Kilimanjaro.Pia ametaja baadhi ya
wenzake ambao amekuwa akishirikiana nao.
"Baada
ya kumhoji alikubali kwenda kutuonesha ambako wenzake wapo lakini
baadae aliamua kupiga kelele kuwashutua kwa lengo la polisi washambuliwe
ili yeye atoroke.
"Majambazi
hao walianza kurushia risasi askari na ndipo yakaanza majibizano na
hatimaye Polisi kufanikiwa kuua majambazi wawili.Pia tumekamata silaha
mbili ambazo ni SMG moja iliyokuwa na risasi saba na bastola mbili aina
ya Saurus mmoja iliyokuwa na risasi tatu,"amesema Mambosasa.
Amesema
jambazi Kweka yeye alipigwa risasi ambazo zilimjeruhi sehemu mbalimbali
za mwili wake wakati akijaribu kutoroka chini ya ulinzi wa Polisi na
hatimaye akafariki dunia.
Pia
Februari 16 mwaka huu,Polisi walipata taarifa za kiitelejensia huko
maeneo ya Chanika kuna kundi la wahalifu limepanga kufanya tukio la
unyang'anyi wa kutumia silaha. Jeshi la Polisi lilianza ufuatiliaji.
Amesema
saa tano usiku wakiwa njiani kuelekea maeneo ya Chanika Homboza
kuelekea eneo la kufuatilia wahalifu hao walikutana na kundi la watu
sita na waliposimamishwa walikaidi amri na kuanza kufyatua risasi kwa
askari.
Amesema askari walijibu mashambulizi na hatimaye kuwazidi nguvu na kusababisha majeraha kwa majambazi huku wengine wakikimbia.
Majambazi
hao walipopekuliwa mmoja alikutwa na SMG iliyofutwa namba ikiwa na
risasi 28 ndani ya magazini na mwingine akiwa na Bastola aina ya
Browning yenye namba Tz Car 103143 ikiwa na risasi 9 ndani ya magazini.
No comments:
Post a Comment