Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Hifadhi za Taifa nchini (TANAPA),
Jenerali Mstaafu,George Waitara akizungumza na Mhandisi wa ujenzi wa
uwanja huo,Makuye Muhinga juu ya mikakati ambayo inaendelea ya ujenzi wa
uwanja wa ndege wilayani Chato mkoani Geita.
Barabara ya kutua na kuruka ndege (run away) yenye urefu wa Mita 300 ambayo kwa sasa hipo kwenye hatua nzuri za mwisho kukamilika.
Baadhi ya watendaji na wajumbe wa Bodi ya TANAPA wakikagua ujenzi wa mradi wa uwanja wa Ndege Wilayani Chato Mkoani Geita.
Mwenyekiti
wa bodi ya hifadhi za Taifa nchini (TANAPA), Jenerali Mstaafu George
Waitara akizungumza na Mkuu wa Wilaya ya Chato Shaaban
Ntarambe pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi ,Robert Gabriel
Luhumbi(kushoto) wakati walipofika na kujionea ujenzi wa uwanja wa ndege ambao
unajengwa Wilaya ya Chato unavyokwenda kwa kasi.
Mhandisi
wa ujenzi wa uwanja huo,Makuye Muhinga akizungumza na Mwenyekiti wa bodi
ya hifadhi za Taifa nchini (TANAPA), Jenerali Mstaafu,George Waitara
pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Gabriel,Juu ya hatua
ambazo wamezifikia hadi sasa za ujenzi wa uwanja wa Ndege.
Na Joel Maduka-Chato
Kukamilika
kwa ujenzi wa uwanja mkubwa wa ndege wilayani Chato mkoani Geita
unatarajia kuwavutia watalii wengi kutembelea kivutio cha hifadhi ya
Taifa cha Rubondo Kilichopo mkoani humo .
Ujenzi wa
uwanja huo umeanza rasmi mwezi wa Septemba mwaka jana na unatarajia
kukamilika Juni mwaka huu.Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa bodi ya
wadhamini (TANAPA), Jenerali Mstaafu George Waitara wakati alipotembelea
uwanja huo pamoja na wajumbe wa bodi hiyo na baadhi ya watendaji kwa
nia ya kujionea maendeleo ya ujenzi huo ambao umeelezwa kukamilika kwa
asilimia 65.
“
Kiukweli niseme kazi kubwa sana ambayo imefanyika ya ujenzi wa uwanja
huu utakuwa na faida kubwa sana kwaajili ya mambo ya utalii na mambo
mengine kama ya biashara na suala jingine kubwa ni kuibua vivutio
vingine tupate watalii wengi zaidi , tunatarajia utakapokamilika utaleta
manufaa sana katika sekta mbali mbali zikiwemo za utalii na biashara
mkoani Geita na mikoa ya jirani,”alisema Waitara.
Kwa
upande wake, Mhandisi wa ujenzi wa uwanja huo,Makuye Muhinga,Alisema
uwanja huo wenye barabara ya kutua ndege (run a way ) yenye urefu wa
Mita 300 upo kwenye hatua nzuri na kwamba wanatarajia kukamilisha mwaka
huu ujenzi wa uwanja.
Aidha
Mkuu wa Mkoa wa huo , Mhandisi Robert Gabriel Luhumbi ambaye alikuwa ni
miongoni mwa watu ambao wametembelea uwanja huo alisema kukamilika kwa
uwanja huo kutafungua uwigo mpana wa kiuchumi kutokana na kwamba mkoa
utaweza kutembelewa na wageni kutoka mataifa ya nje na jirani.
“Wito
wangu kwa wananchi ni kuhakikisha wanachangamkia fursa mbalimbali za
maendeleo hasa uanzishwaji wa viwanda vidogo vya kuchakata mazao
yalimwayo mkoani humu, na tunaamini uwanja huu utarahisisha usafirishaji
wa bishara ambazo watakuwa wanazifanya badala ya kupitia Mwanza sasa
hivi wataweza kupitia kwenye mkoa wao”Alisema Luhumbi.
Jumla ya hifadhi zilizopo nchini ni 16 ambazo zinatambulika kimataifa ikiwemo na hifadhi ya Rubondo ambayo hipo Mkoani Geita.
No comments:
Post a Comment