Na Said Mwishehe, Globu ya jamii.
BENKI
ya Equity imezindua huduma za kibenki kwa njia ya mtandao ambapo
wateja wao sasa watapata huduma mahali popote kupitia simu za mkononi,
tablets na kompyuta za mezani na mpakato.
Huduma
hizo watazipata kupitia Eazzy Banking kwa kufanya miamala kirahisi iwe
usiku au mchana, wakiwa nyumbani, au ofisini na kubwa zaidi sasa
watakuwa na nafasi ya kuokoa muda na gharama.
Akizungumza
Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa Eazzy Banking, Mkurugenzi Mtendaji
wa Equity Joseph Iha amesema kuwa huduma hizo mpya zitatoa fursa kwa
wateja kufanya miala mahali popote.
"Huduma
za Eazzy Banking zitaambana na EazzyBanking App, app ya kimataifa ya
masuala ya kifedha inayounganisha huduma za laini za simu na kuwawezesha
wateja kutuma fedha na pia kufanya malipo kupitia simu zao popote
walipo na wakati wowote.
"EazzyBanking
ni rahisi kuianzisha na hutoa huduma za kipekee kama kutuma fedha
kwenda akaunti za benki au mitandao ya simu, kuomba na kulipia mikopo ,
kulipia bili(ankara) na aina ya huduma za malipo," amesema Iha.
Amefafanua
kwa wale wenye simu za kawaida, kuna suluhisho kwao ambalo
linajukulikana kama Eazzy24/7. Huduma hiyo ambayo imeboreshwa
inawezesha watumiaji kupata huduma zilezile kama za EazzyBanking App kwa
kupigiga *150*07# kupitia simu zao.
Ameongeza
ndani ya huduma hiyo kuna kipengele cha huduma ambacho mtandaoni
unaweza kufanya manunuzi ya rejareja ambapo wateja wataendesha akaunti
zao na hiyo inajulikana kama EazzyNet; huduma ya malipo mbalimbali
inayoitwa EazzyPay ambayo huwezesha kufanya malipo ya bili kama
ving'amuzi, Tanesco,Luku na Dawasco.
Pia
amesema inawezesha kununua na kulipia bidhaa na huduma kupitia kwa
wauzaji waliosajiliwa kama Supermarket na hoteli kwa pale unapoona bango
au stika ya "EazzyPay inakubalika hapa".
"Huduma
ya mkopo kwa njia ya simu inayoitwa EazzyLoan pamoja na uvumbuzi na
usimamizi wa fedha kwa SMEs /wafanyabiashara wa kati na wateja wakubwa,
kampuni kubwa au Wizara kwa kupata huduma kupitia EazzyBiz.
"Pia
kuna EazzyKikundi ambayo hiyo inatoa nafasi ya kusaidia Saccos,
Viccoba , vikundi vya kiuchumi na uwekezaji na utunzaji kumbukumbu za
biashara,"amesema na kusisitiza kupitia EazzyBanking wateja watapata
huduma za kibenki kirahisi , salama na bila stress,"amesema Iha.
Akifafanua
zaidi amesema uzinduzi wa huduma hiyo ya kibunifu unaongozwa na huduma
mama ya EazzyBanking App ambayo itaimarisha mbinu mkakati za kibenki
katika kuwahudumia wateja kimtandao kutokana na mabadiliko ya mahitaji
yao.
"Hii
imejulikana kutokana na mienendo ya kibenki ya wateja ambayo imeonesha
kukua kwa huduma binafsi zinazowezesha kubenki popote na muda
wowote.Mteja anachotakiwa kufanya ni kupakua tu EazzyBanking App na
apate urahisi wa kubenki," amesema.
Amewahakikisha
Watanzania kuwa benki hiyo ipo makini katika kuhakikisha inaendelea
kutoa huduma bora kwa wateja wake na kuomba wale ambao hawajajiunga na
benki hiyo huu ndio wakati sahihi kwani mambo yote ya kibenki unayafanya
bila Stress.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Equity, Joseph Iha akizungumza na wageni
waalikwa na wanahabari waliofika katika uzinduzi uliofanyika jijini Dar
es Salaam katika uzinduzi wa huduma ya Eazzy Banking inayomsaidia mteja
kufanya miamala yake bila stress wakati wowote 24/7 popote atakapokuwa.
Wateja walihudhuria uzinduzi wa huduma ya Eazzy Banking inayotolewa na benki ya Equity jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya Equity Joseph Iha akizungumza na wanahabari jijini
Dar es Salaam kutoa ufafanuzi wa masuala mbali mbali mara baada ya
uzinduzi wa huduma ya Eazzy Banking inayomsaidia mteja kufanya miamala
yake bila stress wakati wowote 24/7 popote atakapokuwa. Pembeni ni
wakurugenzi wa Bodi ya Benki hiyo ikiongozwa na Simbeye.
No comments:
Post a Comment