Pages

January 29, 2018

TUTAPINGA KWA NGUVU ZOTE MSWADA WA KUZUIA MIKUTANO YA SIASA NCHINI :ZITTO KABWE

Leo Januari 24,2018 kipindi cha majadiliano cha TUJADILIANE kinachorushwa na vyombo vya habari (Redio na TV) vinavyorusha matangazo yake kutokea Jijini Mwanza, kimezungumza na Mhe.Zitto Kabwe ambaye ni mbunge jimbo la Kigoma Mjini, Mchumi na Kiongozi wa chama (ACT Wazalendo).
Mhe.Kabwe amefunguka mambo mengi kwenye kipindi hicho kinachoandaliwa na Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania UTPC ikiwemo Uchumi wa Taifa, Mstakabali wa siasa nchini, hofu ya mswada wa kuzuia mikutano ya siasa, chama na mengineyo katika mahojiano hayo yaliyoongozwa na Mtangazaji Dotto Bulendu.


Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT Wazalendo) Mhe.Zitto Kabwe (kulia), akizungumza kwenye kipindi cha Tujadiliane kinachoandaliwa na UTPC. Kushoto ni mtangazaji wa kipindi hicho Dotto Bulendu. Kipindi hicho hurekodiwa na kurushwa na vyombo vya habari washirika kutoka Mwanza.

Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT Wazalendo) Mhe.Zitto Kabwe (kulia), akizungumza kwenye kipindi cha Tujadiliane kinachoandaliwa na UTPC. Kushoto ni mtangazaji wa kipindi hicho Dotto Bulendu.

Washiriki wa kipindi hicho akiwemo Mkurugenzi wa UTPC Abubakary Karsan (kulia) wakifuatilia kipindi hicho.

Mkurugenzi wa UTPC Abubakary Karsan akizungumza wakati wa ufunguzi wa kipindi hicho (kipindi hurekodiwa na kurushwa na vyombo vya habari washirika kutoka Mwanza).

Baadhi ya viongozi wa ACT Wazalendo mkoani Mwanza.

Baadhi ya washiriki

Baadhi ya wanahabari.
 
 Zitto Kabwe "Tutaupinga kwa nguvu zote Muswada wa kuzuia Mikutano ya Siasa nchini

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...