Naibu Waziri wa Afya,
maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile (MB)
akikagua Bin Kadi ambayo inaonesha idadi ya Dawa zilizoingia na zilizobaki
katika stoo ya dawa ya Kituo cha Afya Nkomolo Mkoani Rukwa.
Naibu Waziri wa Afya,
maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile (MB)
akikagua jokofu la Chanjo wakati alipotembelea katika Kituo cha Afya cha
Nkomolo kilichopo Nkasi Mkoani Rukwa wakati wa Ziara yake ya kukagua Huduma za Afya
Mkoani Rukwa.
Naibu Waziri wa Afya,
maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile (MB)
akikagua Idadi ya watu waliohudhuria Kituoni hapo kupitia mfumo wa Kompyuta
katika stoo ya dawa ya Kituo cha Afya Nkomolo Mkoani Rukwa.
Naibu Waziri wa Afya,
maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile (MB) akipokea
maelezo kutoka kwa Mtaalamu wa Majengo Mhandisi Mwakyembe kutoka Ofisi ya Mkoa
wa Rukwa.
Naibu Waziri wa Afya,
maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile (mwenye
tisheti ya mistari) akipokea maelekezo ya ramani ya jingo jipya la Mama na
Mtoto katika kituo cha Afya Nkomolo, anaemfuatia ni Mganga Mkuu wa Mkoa Dkt. Boniface
Kasululu na wa mwisho ni Mhandisi Mwakyembe.
Naibu Waziri wa Afya,
maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiendelea
na ziara yake katika kituo cha Afya Nkomolo, anaemfuata ni Mhandisi Mwakyembe
na Mbunge wa Nkasi kaskazini Mh.Kessy Ally.
Na WAMJWW. RUKWA-NKASI
Serikali yaanza kutumia mfumo wa nyota kupima huduma zitolewazo na Vituo vya Afya, Hospitali na Zahanati nchini ili kupima utendaji kazi wa watumishi wa Sekta ya Afya katika kutoa huduma kwa wananchi.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile alipotembelea Kituo cha Afya cha Nkomolo Wilaya ya Nkasi Mkoani Rukwa, ikiwa ni muendelezo wa Ziara yake ya kukagua shughuli za utoaji wa huduma za Afya na kuamsha hali kwa wananchi katika kujihusisha na shughuli za maendeleo katika maeneo yao.
“Tumeanza utaratibu wa kutoa nyota katika vituo vya Afya, imeanzia nyota sifuri mpaka nyota tano, sifuri maana yake kituo hicho hakifai kutoa huduma ya Afya na nyota tano maana yake kinafanya vizuri sana” Alisema Dkt. Ndugulile.
Kwa upande mwingine Dkt. Ndugulile aliridhishwa na hali ya upatikanaji wa Dawa katika kituo hicho, hivyo kuwatoa hofu wananchi na kusisitiza kuwa hawapaswi kuuziwa dawa zote muhimu kwani Serikali imeboresha hali ya upatikanaji wa Dawa katika vituo vyote vya Afya nchini.
“Dawa zote za msingi tunazo zakutosha, hivyo hatutarajii kuona mtu aje hapa kutibiwa kisha aambiwe akanunue katika vituo binafsi, Hali ya upatikanaji wa Dawa ni nzuri katika kituo hiki na ni asilimia 85 ” aliendelea Dkt. Ndugulile.
Aidha, Mbunge wa Jimbo la Nkasi Kaskazini Mh. Ally Kessy aliupongeza uongozi wa Mkoa kwa kusimia vizuri ujenzi wa kituo hicho, uliojumuisha Thieta, Wodi ya mama na mtoto mochwari na maabara mpaka hatua ya kupaua kwa jumla ya kiasi cha shilingi Bilioni 290 kwa kutumia nguvu kubwa ya wananchi (fixed akaunti).
Akiwasilisha taarifa ya Mkoa, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Dkt Boniface Kasululu amesema kuwa Mkoa wa Rukwa umeendelea kuboresha huduma za Afya ya mama na mtoto katika maeneo ya vijijini kama juhudi za kupunguza tatizo la vifo vya wanawake na watoto wachanga vitokanavyo na matatizo ya uzazi.
Dkt. Boniface aliendelea kusema kwamba, Zaidi ya vituo 214 kati ya 223 vilivyopo, vinatoa huduma muhimu za mzazi na mtoto jambo linalosaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza vifo vya kina mama wajawazito na watoto wachanga licha ya upungufu mkubwa wa vituo hivyo.
Kwa upande mwingine Dkt. Boniface Kasululu alisema kwamba Mkoa unaendelea kuelimisha jamii kuhusu umuhimu wa kuwapeleka watoto katika vituo vinavyotoa huduma za chanjo, Hadi kufikia Mwezi Novembe 2017 jumla ya Watoto 48,494 wenye umri wa chini ya mwaka mmoja walipewa chanjo, kati ya watoto 50,245 waliotarajiwa ambao ni sawa na asilimia 96 jambo lililoufanya mkoa kuvuka lengo la kitaifa la asilimia 90.
No comments:
Post a Comment