Naibu
waziri wa madini Doto Biteko,Akizungumza na wananchi wa kijiji cha
Buntumbili Wilayani Bukombe ambapo kulitokea tukio la mchimbaji kufukiwa
na kifusi wakati alipokuwa kwenye shughuli za uchimbaji.
Naibu
waziri wa madini Doto Biteko,akisaini kwenye kitabu cha wageni wakati
alipokuwa akiwasili kwenye ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Geita.
Afisa
madini wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Ally Maganga akitoa taarifa ya shughuli
za madini mbele ya Naibu waziri wa madini Doto Biteko .
Naibu
waziri wa madini Doto Biteko Akizungumza na Viongozi na Watendaji
mbalimbali ngazi ya Mkoa wakati wa ziara yake ya kikazi.
Naibu
waziri wa madini Doto Biteko pamoja na viongozi wa Wilaya ya Bukombe
wakiwa kwenye eneo ambalo ajali ya mchimbaji kufukiwa na kifusi
ilitokea
Baadhi
ya viongozi na Naibu waziri wa madini Doto Biteko wakiwa kwenye shimo
ambalo ndipo mchimbaji mdogo ambaye alipoteza uhai wakati akiwa kwenye
shughuli za uchimbaji.
Naibu waziri wa madini Doto Biteko akipatiwa maelezo ya namna ajali hiyo ilivyotokea mgodini hapo.
Mmiliki
wa mgodi huo,akitoa maelezo kwa Naibu waziri wa madini namna ambavyo
wachimbaji hao walivyovyamia eneo hilo na kuanza shughuli za uchimbaji
hali ambayo imesababisha mmoja wao kufukiwa na kifusi.
Naibu
waziri wa madini Doto Biteko akitoa mkono wa pole kwa familia ambayo
imekumbwa na msiba wa kuondokewa na kijana wao ambaye alifukiwa na
kifusi wakati akiwa kwenye kazi ya uchimbaji.
Naibu
waziri wa madini ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Bukombe,Doto Biteko
akisalimiana na kutoa pole kwa kaka yake na marehemu wakati alipofika
nyumbani kwao na marehemu.(PICHA NA JOEL MADUKA)
Naibu
waziri wa madini ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Bukombe,Doto Biteko
akifurahia na wananchi wa kijiji cha Ikalanga wakati alipokwenda
kuzungumza nao juu ya mikakati ya maendeleo.
Na,Joel Maduka,Geita.
Naibu
waziri wa madini Doto Biteko amewataka wachimbaji ambao wanamiliki
leseni kuhakikisha wanazingatia sheria ambazo wamepewa likiwemo suala la
kuweka mazingira mazuri ya utendaji kazi kwenye maeneo yao ya mgodi ili
kuepukana na majanga ambayo yamekuwa yakijitokeza mara kwa mara kwenye
shughuli za uchimbaji.
Akizungumza
wakati alipotembelea na kutoa pole kwenye mgodi mdogokijiji cha
Buntubili eneo ambalo hivi karibuni mchimbaji mmoja aliangukiwa na
kifusi na kufariki.Naibu waziri Doto alisema ni vyema kwa kila mwenye
leseni kuhakikisha usalama unakuwa ni jambo la kwanza huku akimwagiza
afisa madini kufuatilia migodi yote kama imewekwa mabango ambayo
yanaelekezea suala la usalama kwenye mazingira hayo.
“Hatutaki
kuona hata mtanzania mmoja anakufa katika mazingira ya uzembe
tunatamani tuone watanzania wote wanachimba wanaendeleza mali na
wanabaki kuwa salama kwaajili ya kulihudumia Taifa hili ,Taifa hili
linawaitaji watu wote kwa hiyo nitoe wito kila mwenye leseni maali
popote alipo ahakikisha kwamba mazingira yake ya kazi usalama kiwe
kipaumbele na sasa kuanzia leo afisa madini ninakuagiza wote wenye
leseni ambao wanaendeleza migodi waweke mabango yanayoeleza umuhimu wa
usalama kila kwenye mgodi unaofanya kazi”Alisisitiza Mh,Doto.
Pamoja
na hayo Naibu Waziri wa Madini amewataka wananchi kutokuingia kwenye
maeneo ambayo yamesimamishwa na ambayo ni hatarishi kwani kufanya hivyo
wanaweza kujisabasha hatari ya kupoteza maisha kutokana na maeneo hayo
kutokuwa kwenye hali nzuri ya uchimbaji.
Akisoma
taarifa kwa Naibu waziri wa madini,mlinzi wa eneo hilo la mgodi ,Bw
Christopha Mazige .amesema kuwa ajali hiyo ilitokana na ubishi wa vijana
watatu ambao walivamia mgodini hapo kwa lengo la kutafuta mali lakini
ghafla wakiwa kwenye mabishano sehemu moja ya ardhi alipokuwa amesimama
kijana ambaye alifukiwa na kifusi ilikatika na kushuka naye kwenye shimo
kutokana na hali hiyo wenzake walikimbia.
Kwa
upande wake Afisa Madini Mkazi Mhandisi Ally Maganga amesema bado kuna
changamoto zinazoikabili Sekta ya madini kama baadhi ya Wachimbaji
wadogo kushindwa kulipa kwa wakati tozo stahiki za madini kama vile ada
za mwaka za leseni na Mrabaha wa madini.
No comments:
Post a Comment