Naibu
Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Dotto Mashaka Biteko akizungumza na
wakuu wa idara na vitengo pamoja na wafanyakazi wote wa wizara ya madini
mara baada ya kuwasili ofisini Mjini Dodoma, Leo Januari 15, 2018.
Picha Zote Na Mathias Canal.
Naibu
Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Dotto Mashaka Biteko akisisitiza jambo
wakati akizungumza na wakuu wa idara na vitengo pamoja na wafanyakazi
wote wa wizara ya madini mara baada ya kuwasili ofisini Mjini Dodoma,
Leo Januari 15, 2018.
Naibu
Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Stanislaus Nyongo akizungumza jambo
kabla ya kumkaribisha Naibu Waziri mwenzake katika Wizara hiyo Mhe Dotto
Mashaka Biteko kuzungumza na wakuu wa idara na vitengo pamoja na
wafanyakazi wote wa wizara ya madini mara baada ya kuwasili ofisini
Mjini Dodoma, Leo Januari 15, 2018.
Naibu
Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Dotto Mashaka Biteko akizungumza na
wakuu wa idara na vitengo pamoja na wafanyakazi wote wa wizara ya madini
mara baada ya kuwasili ofisini Mjini Dodoma, Leo Januari 15, 2018.
Na Mathias Canal, Dodoma
Sekta
ya Madini inachangia kati ya asilimia 3.5 mpaka 4 katika Pato la Taifa
ukilinganisha na sekta zingine ambazo zimejitutumua kwa kiasi kikubwa
katika mchango mahususi wa pato la Taifa nchini Tanzania.
Naibu
Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Dotto Mashaka Biteko amebainisha kuwa
kiasi cha kati ya asilimia 3.5 mpaka 4 ni kidogo sana ukilinganisha na
umuhimu wa sekta hiyo nchini hivyo Wizara ya Madini imekusudia kuongeza
tija katika mchango wa pato la Taifa kupitia sekta hiyo muhimu ya
Madini.
Mhe
Biteko amebainisha hayo Leo Januari 15, 2018 wakati akizungumza na wakuu
wa idara na vitengo pamoja na watumishi wa Wizara ya Madini ofisi Kuu
Mjini Dodoma huku akiwataka watumishi wote kufanya kazi kwa bidii,
nidhamu na uzalendo mkubwa kwa manufaa ya Taifa.
Alisema
kuwa sekta ya Madini ni muhimu nchini kutokana na rasilimali Madini
ilizonazo hivyo watumishi wote wanapaswa kufikiria namna ya kufanya kazi
kwa tija ili kuwa na ongezeko la mchango mkubwa katika pato la Taifa.
"Natamani
nione kwenye taarifa ya robo mwaka ya BOT ikisoma kwamba sekta ya
madini inachangia angalau asilimia 10 ya Pato la Taifa kuliko ilivyo
hivi sasa na hilo naamini linawezekana kwa ushirikiano wa pamoja"
Alisisitiza Mhe Biteko
Mhe
Biteko alisema kuwa hakuna mtu yeyote ambaye atatutumua mabega kwamba ni
mkubwa katika Wizara badala ayake ukubwa wa cheo na umri utaonekana
katika matokeo muhimu na makubwa katika utendaji kazi.
"Mimi
kuwa Naibu Waziri hapa So What... kama sitofanya kazi yenye matokeo
makubwa kutokana na imani niliyopewa na Rais nitakuwa si lolote, hivyo
kwa ushirikiano wenu pekee tutaweza kutimiza utendaji uliotukuka na
wenye manufaa makubwa" Alikaririwa Mhe Biteko wakati akizungumza na
watumishi wa Wizara ya Madini
Mhe
Biteko alisema kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John
Pombe Magufuli anafanya kazi nzuri kwa manufaa makubwa ya watanzania
wote hivyo watumishi mbalimbali wa serikali, sekta binafsi na wananchi
kwa ujumla wanapaswa kuunga mkono jitihada hizo pasina kurudisha nyuma
makusudi na matakwa ya utekelezaji wa ilani ya ushindi ya Chama Cha
Mapinduzi (CCM) Mwaka 2015-2020.
Asubuhi
siku ya Jumatatu Januari 8, 2018 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli alimuapisha Mhe Dotto Mashaka
Biteko kuwa Naibu Waziri wa madini, Ikulu Jijini Dar es salaam.
No comments:
Post a Comment