Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya
Kalambo pamoja na kamati yake ya Ulinzi na Usalama kwa kushirikiana na
Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Kalambo kukaa pamoja na kuandaa
mkakati wa kuzui uvuvi haramu unaoendelea katika mwambao wa ziwa
Tanganyika ili kuokoa viwanda vilivyopo katika mwambao huo.
Amesema
kuwa uvuvi haramu unaoendelea katika mwambao huo unahatarisha maendeleo
ya viwanda vya samaki vilivyopo na hatimae kudhoofisha ajira za
wananchi waliopo karibu na viwanda hivyo na hatimae kurudisha nyuma
juhudi za serikali ya awamu ya tano katika kuibua na kuimarisha viwanda
vilivyopo.
“Mwisho
wa mwezi huu nataka taarifa ya namna mlivyojipanga kupiga marufuku
uvuvi haramu ikiwa ni pamoja na kutoa elimu na kuwakamata wale
wanaokaidi na kuendesha uvuvi haramu, uvuvi haramu ukiendelea hiki
kiwanda hakitakuwepo, kwasababu ya kuua samaki na watoto wake, achene
uvuvi haramu, mnamaliza samaki katika ziwaletu hili,” RC Wangabo
Alisisitiza
Ameongeza
kuwa samaki ndio rasilimali pekee inayowaajiri pamoja na kuendesha
kiwanda na kuwataka wananchi kuungana pamoja kuhakikisha wanatunza
rasilimali hiyo, na kupiga marufuku aina zote za uvuvi haramu na kuonya
kutosikia kiwanda kimefungwa kutokana na kukosa samaki amabao wamekwisha
kwasababu ya uvuvi haramu.
Ameyasema
hayo alipotembelea viwanda viwili vya samaki vya Mikebuka Fisheris
Tanzania Limited pamoja na Akwa Fisheries Tanzania Limited vilivyopo
katika kata ya Kasanga ambapo kiwanda pekee kinachojikongoja ni Mikebuka
fisheries huku AkwaFisheries kikiwa kimesimamisha uzalishaji.
Awali
alipokuwa akisoma taarifa ya Kiwanda cha Mikebuka Fisheries Tanzania
Limited Mtendaji wa Kijiji cha Muzi Gasper Kateka amesema kuwa mbali na
ukosefu wa samaki ametaja kuwa changamoto nyingine ni Umeme na barabara
jambo linalowafanya kutumia gharama kubwa kendesha kiwanda hicho kwa
majenereta na kupakia samaki kwenye boti hadi bandari ya kasanga ili
kuweza kuwasafirisha kwenda Sumbawanga kukwepa kipande cha barabara cha
Km 1.2 kilichojaa mawe.
“Mikebuka
Fisheries in maeneo mawili ya kuchakata samaki ikiwa Sumbawanga yenye
uwezo wa kilo 8000 kwa siku na kasanga yenye uwezo wa kilo 15000 kwa
siku lakini kutokana na uhaba wa samaki uwezo umeshuka na kuchakata kilo
3000 hadi 4000 kwa siku na kuajiri watu 30 na vibarua 55,” Kateka
alieleza.
Kwa
upande wake Afisa uvuvi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo Godfrey
Makoki alitoa ufafanuzi wa makubaliano ya matumizi ya ziwa Tanganyika
yaliyofanya na nchi nne (Zambia, Burundi, Tanzania na DR Congo) katika
kikao kilichofanyika 18/10/2012 Mjini Bujumbura katika kanuni ya nne ya
makubaliano hayo imekataza uvuvi wa dagaa mchana katika ziwa Tanganyika.
“jambo
linalotupa shida ni uvuvi wa kuvua dagaa mchana, kitaalamu dagaa huwa
wanakuja kutaga mchana hivyo wanakuwa wakubwa kwasababu wana mayai na
usiku huwaoni, sasa huwa tunawaambia kuwa huo ni uvuvi haramu hapo
inakuwa ni tatizo,” Makoki Alibainisha.
Katika
Kutatua tatizo la Umeme na Barabara Mh. Wangabo amemuagiza Meneja wa
Tanesco Mkoa wa Rukwa kuhakikisha umeme wa REA awamu ya tatu unawafika
haraka katika Kijiji hicho kwani kipo kwenye mkakati na kuwaagiza TARURA
na TANROAD kushirikiana na Mkurugenzi wa Halmashauri kuhakikisha ndani
ya miezi mitatu wanairekebisha barabara ya Km 1.2 ili iweze kupitika.
Mwambao
wa Ziwa Tanganyika kwa Mkoa wa Rukwa una Viwanda Vinne vya Samaki,
Viwili vipo Kata ya Kipili, Wilaya ya Nkasi na Viwili vipo Kata ya
Kasanga, Wilaya ya Kalambo Mkoani Rukwa.
Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa, Mh. Joachim Wangabo (wa tatu kutoka kulia) akipewa
maelezo na Mkurugenzi wa Mikebuka Fisheries Tanzania Ltd Azim Premji (wa
pili kutoka kulia) katika kiwanda cha Mikebuka Fesheries Tanzania Ltd.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Mh. Joachim Wangabo akipiga marufuku uvuvi
haramu katika ziwa Tanganyika ili kuokoa viwanda vilivyopo katika
mwambao wa Ziwa hilo, (kushoto aliyekaa) Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Mh.
Julieth Binyura.
Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa, Mh. Joachim Wangabo (Katikati) akitoa maelekezo kwa
Meneja wa Tanesco Mkoa wa Rukwa Mhandisi, Herini Mhina (Kulia) na
(Kushoto) Mkuu wa Wilaya ya Kalambo, Juleth Binyura.
Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa, Mh. Joachim Wangabo (wa tatu kushoto) akipokea
maelezo kutoka kwa Mhandisi Mshauri, Martin Hossey (wa pili kushoto)
kuotoka Kampuni ya Nicholas O'Dwyer inayosimamia ujenzi wa Barabara ya
Sumbawanga - Matai - Kasanga yenye urefu wa Km 112 ya thamani ya Bilioni
133 iliyomalizika kwa kiwango cha Km 71.5.
Mwonekano wa Kiwanda cha Akwa Fisheries Tanzania Ltd kilichosimamisha uzalishaji.
No comments:
Post a Comment