Na Said Mwishehe
WAZIRI
wa Maliasili na Utalii Dkt.Hamis Kigwangala amesema ipo haja ya kuwa na
kauli mbiu ambayo itatumika kuutangaza utalii wa Tanzania katika
mataifa mbalimbali duniani.
Amesema
Tanzania imejaaliwa kuwa na maeneo mengi ya utalii lakini
hayajafahamika kutokana na nguvu ndogo ya kuyatangaza kwake, hivyo
kusababisha watalii wengi kufanya utalii katika maeneo machache ya
utalii ukiwamo Mlima Kilimanjaro.
Dk.Kigwangala
ametoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam leo wakati anazindua Kamati ya
Utambulisho wa Utalii Tanzania na kufafanua kuna vivutio vingi na sasa
ipo haja kuendelea kuvitangaza kwa nguvu zote.
Amesema
wajumbe wa kamati watakuwa na jukumu la kuweka mikakati sahihi ya
kuhakikisha utalii wa Tanzania unaendelea kutangazwa kwa lengo la
kuongeza watalii wa ndani na nje ya nchi.
"Tunayo
maeneo mengi ya utalii lakini yanayofahamika ni machache, kuna watalii
wanakuja kwa ajili ya kwenda Mlima Klimanjaro na wengine Mbuga ya
Serengeti wakati yapo maeneo mengi ya utalii.Lazima tutangaze utalii
wetu na hii kamati itatusaidia kutuongoza,"amesema Dk.Kigwangala.
Amewataka wajumbe wa kamati hiyo kutafuta kauli mbiu ambayo itautangaza utalii wa Tanzania nchi mbalimbali duniani.
"Iwe
kauli mbiu ambayo itatutofautisha Tanzania na nchi nyingine kwenye
mambo ya utalii na lazima tuwe na kauli mbiu ya kipekee katika
kuutangaza utalii wetu,"amesema Dk.Kigwangala.
Amefafanua kuna mbuga za wanyama 16 lakini zinazotambulika chache,hivyo juhudi zinahitaji kutangaza vivuto vya utalii vilivyopo.
Mwenyekiti
Mwenza wa Kamati ya Kitaifa ya Utambulisho wa Utalii Tanzania Richard
Lugimbana amemhakikishia Dk.Kigwangala kuwa wanatambua jukumu ambalo
wamepewa na hivyo ni wajibu wao kuweka mikakati ambayo itasaidia
kuutambulisha utalii wetu.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Bodi ya Utalii Devotha Mdachi amefafanua kamati hiyo ina
jumla ya wajumbe 21 ambao wengi wao ni watalaamu wa masoko.
Ameongeza
utambulisho mpya kwa ajili ya kutangaza utalii wa Tanzania utaifanya
nchi kuwa katika ramani nzuri ya kutambulika kwa vivutio vyake vya
utalii.
Waziri
wa Maliasili na Utalii Dkt. Khamis Kigwangalla akisisistiza jambo
wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kamati ya Kitaifa ya Utambulisho wa
Utalii wa Tanzania leo hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Chuo cha
Taifa cha Utalii Jijini Dar es Salaam leo. Kamati hiyo yenye wajumbe 22
imeundwa na Mhe. Waziri kwa lengo la kupitia na kubuni mkakati mbadala
wa namna ya kutangaza utalii wa Tanzania ndani na nje ya nchi.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Kitaifa ya Utambulisho wa Utalii wa Tanzania Bibi. Devotha
Mdachi akielezea jambo mbele ya wajumbe wa kamati hiyo (hawapo pichani)
mara baada ya kuzinduliwa rasmi kwa Kamati hiyo leo Jijini Dar es
Salaam. Kulia ni Mwenyekiti Mwenza wa Kamati hiyo Richard Rugimbana.
Kamati hiyo yenye wajumbe 21imeundwa na Mhe. Waziri kwa lengo la kupitia
na kubuni mkakati mbadala wa namna ya kutangaza utalii wa Tanzania
ndani na nje ya nchi.
Baadhi
ya wajumbe wa Kamati ya Kitaifa ya Utambulisho wa Utalii wa Tanzania
wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Khamis
Kigwangalla wakati wa hafla ya uzinduzi wa kamati hiyo leo Jijini Dar es
Salaam. Kamati hiyo yenye wajumbe 21 imeundwa na Mhe. Waziri kwa lengo
la kupitia na kubuni mkakati mbadala wa namna ya kutangaza utalii wa
Tanzania ndani na nje ya nchi.
Waziri
wa Maliasili na Utalii Dkt. Khamis Kigwangalla (katikati) akiwa katika
picha ya pamoja na wajumbe wa Kamati ya Kitaifa ya Utambulisho wa Utalii
wa Tanzania lmara baada ya uzinduzi wa kamati hiyo leo Jijini Dar es
Salaam. Kamati hiyo yenye wajumbe 21 imeundwa na Mhe. Waziri kwa lengo
la kupitia na kubuni mkakati mbadala wa namna ya kutangaza utalii wa
Tanzania ndani na nje ya nchi.
Picha na Frank Shija – MAELEZO
No comments:
Post a Comment