Naibu
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt.
Faustine Ndugulile (Mb) akiangalia bidhaa ya Tea Masala wakati
alipotembelea moja ya Kikundi cha wanawake wajasiriamali cha kilichopo
Manispaa ya Jiji la Mbeya, mkoani Mbeya, katika ziara ya kuamsha ari ya
wananchi kushiriki shughuli za maendeleo.
Naibu
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt.
Faustine Ndugulile (Mb) akiangalia bidhaa ya Tomato Sauce wakati
alipotembelea moja ya Kikundi cha wanawake wajasiriamali kilichopo
Manispaa ya Jiji la Mbeya, mkoani Mbeya, katika ziara ya kuamsha ari ya
wananchi kushiriki shughuli za maendeleo.
Naibu
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt.
Faustine Ndugulile (Mb) akiwa aevaa koti lililotengenezwa na
wajasiliamali wadogo wakati alipotembelea moja ya Kikundi cha wanawake
wajasiriamali kilichopo Manispaa ya Jiji la Mbeya, mkoani Mbeya, katika
ziara ya kuamsha ari ya wananchi kushiriki shughuli za maendeleo.
Naibu
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt.
Faustine Ndugulile (Mb) akizungumza na wanawake wajasiliamali
walioshiriki kikao cha siku moja katika Halmashauri ya Jiji la Mbeya
huku akiwa ameshika moja ya bidhaa zinazotengenezwa na wajasiriamali hao
wakati wa ziara yake iliyolenga kuamsha ari ya wananchi kufanya
shughuli za maendeleo.
Naibu
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt.
Faustine Ndugulile (Mb) akitoa motisha kwa Vikundi ‘walelewa’ chenye
mtaji mdogo na kuwaunganisha kwa ‘Vikundi Mlezi’ ambacho mtaji wake
umeimarika ili waweze kusaidia katika kukuza biashara zao wakati wa
ziara yake Mkoani Mbeya iliyolenga kuamsha ari ya wananchi kufanyakazi
za maendeleo.
Naibu
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt.
Faustine Ndugulile (Mb) akitoa mkopo wa Shillingi Million 1 kwa mmoja wa
mwananchama wa Saccoss ya wanawake Mbeya wakati wa Uzunduzi wa Saccoss
hiyo wakati wa ziara yake ya Mkoani Mbeya iliyolenga kuamsha ari ya
wananchi kufanya kazi za maendeleo.Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW
Kitengo cha Mawasiliano WAMJW
Naibu
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt.
Faustine Ndugulile (Mb) amezidua Saccoss ya Wanawake katika Halmashauri
ya Jiji la Mbeya kwa ajili ya wajasiriamali wadogowadogo ili kuweza
kutatua changamoto zao na kuwawezesha kupa mbinu mbalimbali za
kufanikisha matarajio yao na kupata maendeleo.
Ameizindua
Saccoss hiyo Mkoani Mbeya wakati akiitambulisha Programu ya ‘Kikundi
Mlezi’ katika Manispaa ya ya Jiji la Mbeya yenye lengo la kuwawezesha
wanawake wajasirimali kuwezeshana kati yao wenyewe katika kuanzisha na
kuendeleza miradi ya biashara.
Dkt.
Ndugulile amesema kuwa katika zoezi la kuamsha ari ya wananchi kushiriki
katika shughuli za maendeleo linaenda sambamba na uwezeshwaji wa
wanawake katika kuwashirikisha wanawake wenyewe katika kuibua miradi na
kuanzisha shughuli za uzalishaji kwa kuzingatia matumizi ya fursa na
weledi wa wananchi wenyewe.
Dkt.Ndugulile
amesema kuwa ili kufanikisha kufikiwa kwa Tanzania ya viwanda Serikali
kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo itaendelea kuweka mazingira
wezeshi kwa wajasiriamali wadogo wadogo hasa wanawake kuwaweza kuanzisha
vikundi vitakavyoanzisha viwanda vidogo vidogo na kuzalisha bidhaa
zitakazo uzwa ndani na nje ya mkoa wa Mbeya na hivyo kuutangaza mkoa
kupitia bidhaa zilizozalishwa kwa kutumia ubunifu na rasilimali
zilizopo.
Ameongeza
kuwa lengo la kuzindua Programu ya ‘Kikundi Mlezi’ na Saxccoss ya
Wanawake ni kuwawezesha wanawake wajasiriamali kiuchumi na
kuwashirikisha wajasiliamali waliokomaa katika biashara kuwasaidia
wanawake wajasiriamali wanaoanza shughuli hizo kwa kuwapatia ujuzi,
mbinu, maarifa, taarifa za soko na upatikanaji wa mikopo na vifaa.
“Niseme
uzinduzi wa Saccoss hii kwa ajili ya wajasiriamali ni muhimu kwenu
wanawake wajasiriamali na hata wale ambao wanaanza na kwa asilimia kubwa
itasaidia kuibua wanawake ambao hawakuwa na mitaji ya kufanya shughuli
zao pamoja na kuwawezesha kuanzisha biashara zao na kufanya wanawake
kujiunga na vikundi na hatimaye kuanzisha viwanda vidogo na vya
kati”alisisitiza Mhe. Dkt. Ndugulile.
Naye
Mwakilishi wa Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Bw.
Julius Mbilinyi amesema kuwa Wizara itaendelea kuhamasisha wanawake
kujitokeza na kujiunga na vikundi na kusaidiana katika kuendesha
biashara na kusaidia kuhamasisha Halmashauri kutenga asilimia 10 kwa
wanawake na vijana ambazo zitatumika kama mtaji wenye masharti nafuu wa
kuwasaidia kujikwamua kiuchumi.
Kwa
upande wake Mweyekiti wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya Bw. amesema kuwa
programu ya ‘Kikundi Mlezi’ na Saccoss ya wanawake itasaidia kuwainua
wanawake ikiwa halmashauri zitashirikiana na wadau wa maendeleo
kuwawezesha wanawake kujitokeza kwa wingi kujishughulisha na shughuli za
uzalishaji na kumwahakikishia Naibu Waziri kushirikiana na Maafisa
Maendeleo ya Jamii katika kufanikisha masuala ya maendeleo katika Mkoa
wa Mbeya.
Mmoja
wa Wanawake wajasiliamali Manispaa ya Jiji la Mbeya Bi. ameishukuru
Serikali kwa kuzindua Progarmu ya kikundi Mlezi na kuanzishwa kwa
Saccoss hiyo utakaowawezesha wanawake kusaidiana katika kuanzisha na
kuboresha biashara ambazo zitawasaidia kujikwamua kiuchumi.
Naibu
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt.
Faustine Ndugulile (Mb) anafanya ziara mkoani Mbeya kwa kuwatembelea
wanawake wajasiliamali katika kuhamasisha wanawake kujishughulisha ili
kusaidia kuchangia lengo la kuanzisha biashara ndogo na za kati kwa
manufaa ya Taifa. Msisitizo umetolewa kwa wananchi kupenda kununua
bidhaa zetu wenyewe ili kufikia lengo la uanzishaji wa viwanda 100 kwa
kila mkoa.
No comments:
Post a Comment