Waziri
wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (aliyeshika kipaza sauti) akiwasalimu
wananchi wa Kijiji cha Pembamoto, Wilaya ya Kongwa, mkoani Dodoma,
alipofanya ziara kukagua utekelezaji wa Mradi wa Umeme Vijijini Awamu ya
Tatu (REA III)
Spika
wa Bunge ambaye pia ni Mbunge wa Kongwa, Job Ndugai (kushoto),
akimpokea Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (kulia) alipowasili
jimboni kwake Kongwa kukagua Mradi wa Umeme Vijijini Awamu ya Tatu (REA
III).
Waziri
wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (kushoto), akifafanua jambo kwa Mkuu
wa Mkoa wa Dodoma, Bilinith Mahenge (kulia), alipofika ofisini kwake
hivi karibuni, kabla ya kutembelea Wilaya za Kongwa na Kondoa kukagua
utekelezaji wa Mradi wa Umeme Vijijini Awamu ya Tatu (REA III). Kushoto
kwa Waziri ni Kamishna wa Nishati na Masuala ya Petroli, Mhandisi
Innocent Luoga. Wengine ni watendaji kutoka Shirika la Umeme Tanzania
(TANESCO), Wakala wa Nishati Vijijini (REA) pamoja na wakandarasi
wanaotekeleza Mradi husika katika Wilaya hizo.
Waziri
wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (kushoto) akimkabidhi Spika wa Bunge
ambaye pia ni Mbunge wa Kongwa, Job Ndugai, kifaa kinachotumika
kuunganisha umeme katika nyumba pasipo kutandaza nyaya, kijulikanacho
kama UMETA. Waziri alitoa kifaa hicho kama zawadi kwa baadhi ya wazee
katika Kijiji cha Makole, Wilaya ya Kongwa, wakati wa ziara yake kukagua
utekelezaji wa Mradi wa Umeme Vijijini (REA III) pamoja na kuzungumza
na wananchi.
Waziri
wa Nishati Dkt. Medard Kalemani (kulia), akifafanua jambo kwa Spika wa
Bunge ambaye pia ni Mbunge wa Kongwa, Job Ndugai (kushoto), alipokuwa
katika ziara ya kazi jimboni humo kukagua utekelezaji wa Mradi wa Umeme
Vijijini Awamu ya Tatu (REA III). Wengine pichani ni viongozi mbalimbali
wa Serikali pamoja na wataalam kutoka wizarani, Shirika la Umeme
Tanzania (Tanesco) na Wakala wa Nishati Vijijini (REA).
Diwani
wa Kata ya Nhumbi, Wilaya ya Kongwa, Sina Mude akizungumza wakati wa
ziara ya Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani kukagua utekelezaji wa
Mradi wa Umeme Vijijini Awamu ya Tatu (REA III).
Meneja
wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) Wilaya ya Kongwa, Seif Shabani
(kulia), akiorodhesha jina la mmojawapo wa wazee waliopatiwa zawadi ya
kifaa cha Umeme Tayari (UMETA) na Waziri wa Nishati, Dkt. Medard
Kalemani wakati wa ziara yake kukagua utekelezaji wa Mradi wa Umeme
Vijijini Awamu ya Tatu (REA III)
Sehemu
ya umati wa wananchi katika Vijiji vya Makole, Pembamoto na Bereko
wilayani Kongwa na Kondoa, wakimsikiliza Waziri wa Nishati, Dkt. Medard
Kalemani (hayupo pichani) wakati wa ziara yake kukagua utekelezaji wa
Mradi wa Umeme Vijijini Awamu ya Tatu (REA III).
Waziri
wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (aliyeshika kipaza sauti),
akiwatambulisha wakandarasi wanaotekeleza Mradi wa Umeme Vijijini Awamu
ya Tatu (REA III) katika Wilaya ya Kongwa, wakati wa ziara yake kukagua
maendeleo ya utekelezaji wa Mradi huo.
Mkuu
wa Wilaya ya Kondoa, Sezaria Makota (kulia) akiwa pamoja na Kamati ya
Ulinzi na Usalama ya Wilaya hiyo wakimpokea Waziri wa Nishati, Dkt.
Medard Kalemani (wa pili kutoka kulia) alipowasili wilayani humo kukagua
utekelezaji wa Mradi wa Umeme Vijijini Awamu ya Tatu (REA III). Kulia
kwa Waziri ni Kamishna wa Nishati na Masuala ya Petroli, Mhandisi
Innocent Luoga.
Waziri
wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (aliyeshika kipaza sauti), akizungumza
na wananchi wa Kijiji cha Bereko, Wilaya ya Kondoa wakati wa ziara yake
kukagua utekelezaji wa Mradi wa Umeme Vijijini Awamu ya Tatu (REA III).
Naibu
Waziri wa Fedha na Mipango ambaye pia ni Mbunge wa Kondoa, Ashatu
Kijaji, akizungumza wakati wa ziara ya Waziri wa Nishati, Dkt. Medard
Kalemani (katikati – mbele) wilayani humo kukagua utekelezaji wa Mradi
wa Umeme Vijijini Awamu ya Tatu (REA III)
Kazi
ya kuunganisha umeme katika Kijiji cha Bereko, Wilaya ya Kondoa ikiwa
katika hatua za mwisho, kama mafundi hawa walivyokutwa na Waziri wa
Nishati, Dkt. Medard Kalemani, wakati wa ziara yake kukagua utekelezaji
wa Mradi wa Umeme Vijijini Awamu ya Tatu (REA III).
Na Veronica Simba – Dodoma
Waziri
wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani amekagua maendeleo ya utekelezaji wa
Mradi wa Umeme Vijijini Awamu ya Tatu (REA III) katika Wilaya za Kongwa
na Kondoa mkoani Dodoma.
Katika
ziara hiyo ya siku moja iliyofanyika Jumatatu Desemba 11, 2017, Waziri
Kalemani aliwasisitiza viongozi wa Halmashauri ambako Mradi wa REA III
unapita, kuhakikisha wanatenga fedha kwa ajili ya kuunganisha umeme
hususan katika Taasisi mbalimbali za umma.
“Siyo
vema Taasisi muhimu za umma zikaendelea kukosa umeme kwa kutokuwa na
fedha hivyo kuwatesa wananchi. Hakikisheni mnatenga fedha kwa shughuli
hiyo muhimu.”
Aidha,
alibainisha kuwa, maeneo yanayopewa kipaumbele katika Mradi wa REA III
ni Taasisi zote za umma ili kuhakikisha zinatoa huduma bora kwa
wananchi.
Pia,
aliwataka wakandarasi wanaotekeleza Mradi huo katika maeneo mbalimbali
nchini, kukutana na viongozi wa maeneo husika wakiwemo wabunge ili
wapewe mwongozo wa sehemu muhimu za kipaumbele zinazotakiwa
kuunganishiwa umeme.
Kwa
upande wake, Spika wa Bunge ambaye pia ni Mbunge wa Kongwa, Job Ndugai,
akizungumza wakati wa ziara ya Waziri jimboni kwake, aliwaasa watendaji
katika Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kuongeza uwajibikaji kwa
wateja wao ili kuboresha utoaji huduma ya umeme kwa wananchi.
“Bado
zipo changamoto kadhaa katika utoaji wa huduma ya umeme kwa wananchi.
Tanesco ongezeni uwajibikaji ili wananchi wanufaishwe na huduma hiyo
muhimu kama Serikali ilivyodhamiria.”
Naye
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango ambaye pia ni Mbunge wa Kondoa, Dkt.
Ashatu Kijaji, alitoa pongezi na shukrani kwa Serikali kupitia Wizara ya
Nishati kwa kupanga kuviunganishia umeme vijiji 24 vya Wilaya hiyo,
kupitia REA III.
“Kwa
niaba ya wananchi wa Kondoa, natoa pongezi za dhati kwa Serikali na
kuiomba iendeleze jitihada hizi za kuwaletea wananchi wake maendeleo
kupitia upatikanaji wa nishati muhimu ya umeme,” alisema.
Katika
ziara hiyo, Waziri Kalemani alifuatana na viongozi na wataalam
mbalimbali kutoka wizarani, Tanesco na Wakala wa Nishati Vijijini (REA),
akiwemo Kamishna wa Nishati na Masuala ya Petroli, Mhandisi Innocent
Luoga.
No comments:
Post a Comment