Na Veronica Simba .
Serikali
imeliagiza Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kuhakikisha wateja wote
walioomba na kulipia huduma hiyo mwaka 2017 wanaunganishiwa kabla ya
Desemba 30 mwaka huu.
Waziri
wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani alitoa agizo hilo kwa nyakati tofauti
hivi karibuni, akiwa katika ziara ya kazi kukagua utekelezaji wa miradi
ya umeme mkoani Singida na Dodoma.“Agizo
hili ni kwa nchi nzima. Hakikisheni wateja waliowasilisha maombi yao na
kulipia ndani ya mwaka huu wa 2017 wawe wameunganishiwa umeme siyo
zaidi ya Desemba 30 mwaka huu.”.
Aidha,
Dkt Kalemani aliwaagiza watendaji wa shirika hilo kutoa elimu kwa umma,
hasa wananchi walioko vijijini kuhusu umuhimu wa kutumia umeme ili
kuwahamasisha kuunganisha nishati hiyo katika makazi yao.
Akifafanua,
Waziri alisema kuwa takwimu zinaonesha kuwa baadhi ya wananchi
hawajaunganisha umeme katika makazi yao japokuwa tayari Serikali
imekwishawafikishia nishati hiyo katika maeneo yao.“Inawezekana
baadhi ya wananchi hawajatambua umuhimu wa kutumia umeme, hivyo ni vema
wapatiwe elimu husika. Tuwatembelee mahali waliko, hususan vijijini na
tuwapatie elimu hiyo,” alisisitiza.
Akizungumzia
faida za umeme, Waziri Kalemani alisema umeme ni kichocheo kikubwa cha
maendeleo kwani shughuli nyingi za kiuchumi zinahitaji nishati hiyo.Aliongeza
kuwa, ili dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano ya Uchumi wa Viwanda
ifanikiwe, ni lazima kuwepo na umeme wa kutosha na wa uhakika. “Ndiyo
maana tumedhamiria kufikisha umeme hadi vijjijini kwa kasi kubwa, hivyo
wananchi tafadhali tumieni umeme ili kukuza pato lenu na uchumi wa nchi
kwa ujumla.”.
Waziri
aliwapongeza viongozi wa Serikali wakiwemo Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa
Wilaya, Wabunge na Watendaji wa Halmashauri na Vijiji, kwa jitihada zao
za kufuatilia utekelezaji wa ahadi za serikali kwa wananchi ikiwemo
upelekaji wa umeme vijijini.
Aliwataka
wananchi kutoa ushirikiano kwa Serikali kwa kutunza miundombinu ya
umeme katika maeneo yao ili isihujumiwe na hivyo kuwakosesha huduma hiyo
muhimu na pia kuleta hasara kwa serikali.
Ziara
hiyo ya Waziri Kalemani ni muendelezo wa ziara mbalimbali ambazo
amekuwa akifanya nchi nzima kukagua utekelezaji wa miradi ya umeme na
kuzungumza na wananchi wa maeneo husika ikiwa ni pamoja na kupokea kero
na changamoto mbalimbali za wananchi kuhusu sekta ya nishati ili
zifanyiwe kazi.
Katika
ziara hii, Waziri ametembelea Wilaya za Mkalama na Singida Vijijini
mkoani Singida pamoja na Wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma.
Waziri
wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani akizungumza na wananchi wa Kijiji cha
Ibaga, Wilaya ya Mkalama mkoani Singida, wakati wa ziara yake hivi
karibuni kukagua utekelezaji wa miradi ya umeme.
Mbunge
wa Iramba Mashariki, Allan Kiula akizungumza wakati wa ziara ya Waziri
wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani jimboni kwake hivi karibuni, kukagua
utekelezaji wa miradi ya umeme.
Mbunge
wa Mtera, Livingstone Lusinde (kushoto), akizungumza wakati wa ziara ya
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani, jimboni kwake hivi karibuni
kukagua utekelezaji wa miradi ya umeme.
Waziri
wa Nishati, Dkt Medard Kalemani, akiwakabidhi baadhi ya wazee kifaa
kinachotumika kuunganisha umeme pasipo kutandaza mfumo wa nyaya,
kijulikanacho kama Umeme Tayari (UMETA) alipokuwa katika ziara ya kazi
Mikoa ya Singida na Dodoma hivi karibuni.
Afisa
Uhusiano wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Innocent Lupenza,
akiandika majina ya baadhi ya wazee waliopatiwa zawadi ya kifaa
kijulikanacho kama Umeme Tayari (UMETA) na Waziri wa Nishati, Dkt Medard
Kalemani (hayupo pichani), alipokuwa katika ziara ya kazi Mikoa ya
Singida na Dodoma hivi karibuni.
Baadhi ya wataalam wa Wizara ya Nishati na Shirika la Umeme Tanzania
(Tanesco), wakimsikiliza Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (hayupo
pichani) wakati wa ziara yake katika Kijiji cha Muungano, Wilaya ya
Chamwino hivi karibuni, kukagua utekelezaji wa miradi ya umeme.
Sehemu
ya Umati wa wananchi wa vijiji mbalimbali vya Mikoa ya Singida na
Dodoma, wakimsikiliza Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (hayupo
pichani) alipokuwa akizungumza nao wakati wa ziara yake hivi karibuni
kukagua utekelezaji wa miradi ya umeme.
Waziri
wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (wa pili - kushoto) na Mbunge wa
Mtera, Livingstone Lusinde (kushoto) wakimsikiliza Msimamizi wa Mradi wa
Ujenzi wa Kiwanda cha Ngozi kilichopo kijiji cha Idifu, Wilaya ya
Chamwino, Dkt. Francis Njau (wa tatu – kulia), kuhusu mahitaji ya umeme
kwa kiwanda hicho.
Waziri
wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani, akiwasalimu wananchi wa Kijiji cha
Idifu, Wilaya ya Chamwino alipokuwa katika ziara ya kazi kukagua
utekelezaji wa miradi ya umeme.
No comments:
Post a Comment