TAASISI
ya kuzuia na kupambana na rushwa mkoani Tanga(Takukuru) imewafikisha
mahakamani wahasibu wawili wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Tanga Josiah
Mwaipela na Julius Idana kwa mashtaka matatu ya rushwa.
Washtakiwa hao wamefikishwa mahakamani kwa makosa ya
uchepushaji,ubadhirifu
na matumizi mabaya ya madaraka kuhusiana na shilingi milioni
276,095,106.9 za mishahara ya watumishi ambaowalikoma utumishi wao wa
umma kati ya Machi 3 ,2012 na Novemba 2013.
Hayo
yalisemwa na Kamanda wa Takukuru Mkoa wa Tanga, Christopher Mariba
wakati akitoa taarifa yake kwa vyombo vya habari ambapo alisema
washtakiwa hao walifikishwa mahakamani jana Desemba 18 mwaka
huu. Alisema washtakiwa hao walifikishwa mbele ya hakimu mfawidhi wa
mahakama ya hakimu mkazi Tanga,Crisencia Kisongo na kusomewa mashtaka na
waendesha mashitaka wa Takukuru Noel Gabba na Neema Kazoka.
Alisema
washtakiwa hao wanadaiwa kutenda makosa ya uchepushaji,ubadhirifu na
matumizi mabaya ya madaraka kuhusiana na shilingi milioni 276,095,106.9
za mishahara ya watumishi ambao walikoma utumishi wao wa umma kati ya
Machi 3 ,2012 na Novemba 2013.
Aidha
alisema katika shitaka la kwanza upande wa mashtaka uliiambia mahakama
kuwa kati ya machi 3,2012 na Novemba 1,2013 washtakiwa walifanya
uchepuzi wa sh.milioni 276,095,106 ambazo ni mali ya serikali kwa
malengo yasiyokusudiwa. Katika shtaka la pili upande wa mashtaka
uliiambia mahakama kuwa kati ya machi 3,2012 na Novemba 1,2013
washtakiwa walifanya ufujaji na ubadhirifu wa sh.milioni 245,500,000
walizoaminiwa na kukabidhiwa na serikali.
Alisema
katika shtaka la tatu upande wa mashtaka uliiambia mahakama kuwa kati
ya machi 3,2012 na Novemba 1,2013 washtakiwa kwa makusudi walitumia
vibaya madaraka yao kwa kushindwa kuziweka sh.milioni 276,095,106.96 za
mishahara isiyolipwa kwenye akaunti ya Benki kuu ya Tanzania (BOT).
Kamanda huyo wa Takukuru alisema washtakiwa walikana mashtaka dhidi yao
na upande wa mashtaka uliiambia Mahakam kuwa uchunguzi wa shauri
umekamilika na uko tayari kuendelea na shauri kwa tarehe itakayopangwa
na mahakama.
“Kesi
hiyo imeahirishwa hadi Januari 2 mwakani itakapokuja kwa ajili ya
kusomewa maelezo ya awali “Alisema Kamanda huyo wa Takukuru. Hata hivyo
alisema mshtakiwa wa kwanza Josiah Mwaipela aliachiwa kwa dhamana baada
ya kutimiza masharti yaliyowekwa na Mahakama ambapo aliweka bondi ya
mali isiyohamishika yenye thamani ya zaidi ya sh.milioni 69,023,776.74
iliyowekwa na mahakama na mdhamini mmoja.
Aliongeza
pia mshtakiwa wa pili Julius Idana alipelekwa gereza kuu la Maweni
Tanga baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana ya kukabidhi fedha
taslimu sh.milioni 69,023,776.74 au mali isiyohamishika yenye thamani
hiyo pamoja na kuwa na mdhamini mmoja.
Kamanda
huyo wa Takukuru alisema kati ya kiasi cha sh.miloni 276,095,106.96
zilizofanyiwa uchepuzi na washtakiwa sh.milioni 25,602,855.31
ziliokolewa na Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa Takukuru na
kurejeshwa serikalini.Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha
No comments:
Post a Comment