Mratibu
wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali (NGO's) kutoka Mamlaka ya Kudhibiti
na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Bibi. Salome Mbonile akizungumza
wakati wa hafla ya kusherehekea miaka minne tangu kuanzishwa kwa Kituo
cha Upataji nafuu kwa watumiaji wa Dawa za Kulevya (PEDDEREF) kilichopo
Kigamboni Jijini Dar es Salaam jana. Kutoka kushoto ni Msimamizi wa
Programu wa Kituo hicho Khamis Ajib Dimand na Mkurugenzi na Mwanzilishi
wa kituo hicho Bi. Nuru Salehe Ahmed.
Mkurugenzi
na Mwanzilishi wa kituo hicho Bi. Nuru Salehe Ahmed akizungumza wakati
wa hafla ya kusherehekea miaka minne tangu kuanzishwa kwa Kituo cha
Upataji nafuu kwa watumiaji wa Dawa za Kulevya (PEDDEREF) kilichopo
Kigamboni Jijini Dar es Salaam jana. Kutoka kushoto ni Msimamizi wa
Programu wa Kituo hicho Khamis Ajib Dimand na Mratibu wa Mashirika
yasiyo ya Kiserikali(NGO's) kutoka Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana
na Dawa za Kulevya (DCEA) Bibi. Salome Mbonile (katikati).
Mmoja
wa wanufaika wa Kituo cha upataji nafuu kwa watumiaji wa dawa za
kulevya (PEDDEREF) kilichopo Kigamboni Jijini Dar es Salaam Bi. Amina
Mbonde akitoa ushuhuda namna alivyofanikiwa kuacha matumizi ya dawa za
kulevya wakati wa hafla ya kusherehekea miaka minne tangu kuanzishwa
kwa kituo hicho jana. Kutoka kulia ni Mkurugenzi na Mwanzilishi wa kituo
hicho Bi. Nuru Salehe Ahmed, Msimamizi wa Programu wa Kituo hicho
Khamis Ajib Dimand na Mratibu wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali (NGO's)
kutoka Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA)
Bibi. Salome Mbonile na Msimamizi wa Programu wa Kituo hicho Khamis Ajib
Dimand.
Msimamizi
wa Programu wa Kituo hicho Khamis Ajib Dimand akielezea jambo wakati wa
hafla ya kusherehekea miaka minne tangu kuanzishwa kwa Kituo cha
upataji nafuu kwa watumiaji wa Dawa za Kulevya (PEDDEREF) kilichopo
Kigamboni Jijini Dar es Salaam jana. Kutoka kulia ni Mkurugenzi na
Mwanzilishi wa kituo hicho Bi. Nuru Salehe Ahmed na Mratibu wa Mashirika
yasiyo ya Kiserikali (NGO's) kutoka Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana
na Dawa za Kulevya (DCEA) Bibi. Salome Mbonile (katikati).
Mratibu
wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali (NGO's) kutoka Mamlaka ya Kudhibiti
na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Bibi. Salome Mbonile(wapili
kushoto) akishiriki zoezi la kukata keki wakati wa hafla ya kusherehekea
miaka minne tangu kuanzishwa kwa Kituo cha upataji nafuu kwa watumiaji
wa Dawa za Kulevya (PEDDEREF) kilichopo Kigamboni Jijini Dar es Salaam
jana. Kutoka kushoto ni Mmoja wa wanufaika wa Kituo hicho Bi. Amina
Mbonde,Mkurugenzi na Mwanzilishi wa kituo hicho Bi. Nuru Salehe Ahmed na
Afisa Habari toka Ofisi ya Waziri Mkuu Bi. Nyanzobe Magalle.
Mratibu
wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali (NGO's) kutoka Mamlaka ya Kudhibiti
na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Bibi. Salome Mbonile(wapili
kushoto) akimlisha keki Mmoja wa wanufaika wa Kituo cha upataji nafuu
kwa watumiaji wa Dawa za Kulevya (PEDDEREF) kilichopo Kigamboni Jijini
Dar es Salaam Bi. Amina Mbonde wakati wa hafla ya kusherehekea miaka
minne tangu kuanzishwa kwa kituo hicho jana. Kulia ni Mkurugenzi na
Mwanzilishi wa kituo hicho Bi. Nuru Salehe Ahmed.
Na Mwandishi Wetu
SERIKALI
kupitia Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Nchini
(DCEA) imesema ipo mbioni kutoa mwongozo wa kuratibu na kusimamia
viwango vinavyowiana vinavyotarajiwa kutumika katika Vituo vyote vya
Upataji nafuu kwa watumiaji wa dawa za kulevya nchini.
Hayo
yamesemwa jana Jijini Dar es Salaam na Mratibu wa Mashirika yasiyo ya
Serikali NGO’s kutoka (DCEA), Salome Mbonile wakati wa sherehe za
maadhimisho ya miaka minne ya kituo cha upataji nafuu kwa watumiaji wa
dawa za kulevya (PEDDEREF) kilichopo Kigamboni Jijini Dar es Salaam.
Mbonile
alisema katika kuhakikisha kuwa mwongozo huo unaleta tija
iliyokusudiwa, Serikali inatarajia kuwashirikisha wadau wote katika
mapambano dhidi ya madawa ya kulevya ili waweze kutoa mapendekezo,
ushauri na maoni ili kuweza kuisaidia jamii hususani makundi ya vijana
katika kujiepusha na matumizi ya madawa ya kulevya.
"Kumekuwa
na uwoga kwa wananjamii kutembelea Sober House (Nyumba za upataji nafuu
kwa watumiaji wa madawa ya kulevya, lakini kupitia mwongozo huu
tunataka kuweza viwango vinavyofanana ili kutoa fursa kwa watu wote
kutembelea makazi haya" alisema Mbonile.
Mbonile
alisema mapambano ya vita dhidi ya matumizi ya madawa ya kulevya nchini
hayana budi kuungwa mkono na wadau mbalimbali wa maendeleo na hivyo
Serikali itaendelea kutoa ushirikiano wa na asasi, taasisi mbalimbali
ili kuhakikisha kuwa jamii ya Kitanzania hususani vijana inaendelea kuwa
salama na kuondokana na matumizi ya dawa za kuelvya.
Aliongeza
kuwa hadi sasa Tanzania ina jumla ya Nyumba za upataji nafuu kwa
watumiaji wa dawa za kulevya 25 pamoja na Asasi 16 zinazotoa elimu na
kuhamasisha jamii kutambua madhara mbalimbali yatokanayo na matumizi ya
dawa za kulevya ikiwemo hatari ya maambuzi ya magonjwa mbalimbali pamoja
na vifo.
Aidha
aliongeza kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na mashirika mbalimbali
ya kijamii yenye malengo ya kupambana na matumizi ya dawa za kulevya
nchini, hatua inayolenga kuwaunga mkono na kuendelea kutoa ushirikiano
wa karibu kwa kadri inavyowezekana.
“Nyumba
za upataji nafuu kwa watumiaji wa dawa za kulevya nyingi zinajengwa na
waliowahi kutumia dawa za kulevya na Serikali itaendelea kuunga mkono
juhudi za mashirika haya na kutoa ushirikiano unaohitajika ili kuviweza
kutekeleza vyema majukumu yake” alisema Mbonile.
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa PEDDEREF, Nuru Ahmed alisema suala la
matumizi ya dawa za kulevya limekuwa kubwa hususani kwa makundi ya
vijana na kuwataka wazazi kushikamana kwa pamoja badala ya kutupiana
lawama pindi mtoto anapoanza kujihusisha na matumizi ya dawa za kulevya.
Alisema
kuwa ujenzi wa malezi mapya ya vijana walioacha matumizi ya dawa za
kulevya, yanawezeakana iwapo wadau wote hususani jamii zitajihusisha
katika kukemea unyanyapaa ambao umekushika kazi katika jamii, hatua
inayochangia kufifisha jitihada zinazofanywa na Serikali na mashirika
mbalimbali nchini.
“Kituo
chetu kina jumla ya walaibu 58 wakiwemo wanawake 16 na wanaume 42,
tunashukuru kwa ushirikiano tunaoupata kutoka kwa Serikali na kuwaomba
wadau wengine waendelee kushirikiana katika kujenga jamii salama kwa
mustakabali wa kizazi chetu” alisema Nuru.
Naye
Mraibu aliyepata nafuu katika utumiaji wa dawa za kuelvya, Amina Mbonde
alisema alitumia nusu ya uhai wa maisha yake katika kupambana kuachana
na matumizi ya dawa za kulevya, na kukipongeza kituo cha PEDDEREF
kutokana na mwamko wake wa kuwaweka pamoja walaibu wa madawa ya kulevya
na kuwaonyesha mwanga mapya wa maisha yao.
No comments:
Post a Comment