Naibu
Waziri wa Wizara ya Mifugo na uvuvi Mhe.Abdalla Hamisi Ulega amefanya
ziara mkoani Arusha katika Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro kwa lengo
la kuhamasisha upigaji chapa mifugo.
Akizungumza na baadhi ya wafugaji katika halmashauri ya Ngorongoro Ulega amempongeza mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe Mrisho Gambo, kwa utendaji mzuri wa kazi hususani katika kuhamasisha upigaji chapa mifugo mkoani humo.
Aidha Mhe Ulega amezitaja baadhi ya halmashauri zilizofanya vizuri katika zoezi la upigaji chapa kuwa ni pamoja na Chemba, Kondoa, Maswa, Mafinga na Misungwi.
Ambapo mhe. Ulega amewahimiza wafugaji kujitokeza kwa wingi katika zoezi la upigaji chapa mifungo linaloendelea nchi nzima.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega, akishiriki zoezi la upigaji chapa mifugo katika hifadhi ya Ngorongoro mkoani Arusha.
Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo akizindua zoezi la upigaji chapa mifugo katika hifadhi ya Ngorongoro mkoani Arusha.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega (wa kwanza kulia)akizungumza na wananchi wanaoishi katika hifadhi ya Ngorongoro baada ya kushuhudia zoezi la upigaji chapa mifugo mkoa wa Arusha. Katikati ni Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo na kushoto, Naibu Muhifadhi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro Dkt. Maurus Msuha.
Naibu Muhifadhi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro,Dkt Maurus Msuha akishiriki zoezi la upigaji chapa mifungo mkoani Arusha.
Zoezi la upigaji chapa mifungo likiendelea mkoani Arusha.(Picha na Emmanuel Massaka,MMG Arusha)
No comments:
Post a Comment