Mhitimu
wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Amina Sanga akitoa mada kwenye
kongamano la siku moja la vijana wasomi kutoka makanisa mbalimbali ya
kikristo lilifanyika Hoteli ya Landmark jijini Dar es Salaam jana lenye
lengo wasomi hao kutumia taaluma walizonazo katika kuitumikia jamii na
taifa kwa ujumla.
Kongamano likiendelea.
Wanakwaya wa Haleluya Celebration wakiwa kwenye kongamano hilo.
Muonekano wa ukumbi katika kongamano hilo.
Meza
kuu katika kongamano hilo. Kutoka kulia ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha
Dar es Salaam (UDSM), Dk. Philip Sanga, Mgeni rasmi wa Kongamano hilo,
Askofu Mkuu wa Kanisa la Abundant Bressing Centre (ABC), Flaston Ndabila
, Mchungaji John Kanafunzi na Mratibu wa kongamano hilo, Ephraim
Mwambapa.
Wanakwaya wa Haleluya Celebration wakitoa burudani ya nyimbo za kusifu.
Burudani ikiendelea.
Maombi yakifanyika.
Waratibu wa kongamano hilo wakijitambulisha. Kutoka kushoto ni Sarafina Kabwe, Irene Sadock, Michael Mhagama na Yona Kilindu.
Katibu Mkuu wa Kongamano hilo, Lendian Bigoli, akitoa mada.
Mratibu wa Kongamano hilo, Ephraim Mwambapa akitoa mada katika kongamano hilo.
Askofu Mkuu wa Kanisa la Abundant Bressing Centre (ABC), Flaston Ndabila, akizungumza kwenye kongamano hilo.
Maombi yakifanyika.
Maombi yakiendelea.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Dk.Philip Sanga akihutubia kwenye kongamano hilo.
Mgeni
rasmi wa kongamano hilo,Askofu Mkuu wa Kanisa la Abundant Bressing
Centre (ABC), Flaston Ndabila akiwa katika picha ya pamoja na viongozi
wengine na waratibu wa kongamano hilo.
Picha ya pamoja
Na Dotto Mwaibale
ASKOFU
Mkuu wa Kanisa la Abundant Bressing Centre (ABC), Flaston Ndabila
amewataka Vijana wasomi na wanataalumu nchini kumsaidia Rais Dk.John
Magufuli kuliletea Taifa maendeleo.
Ndabila
ametoa mwito huo jijini Dar es Salaam jana wakati akiwahutubia wasomi
wanataaluma katika kongamano la siku moja la vijana wasomi kutoka
makanisa mbalimbali ya kikristo lilifanyika Hoteli ya Landmark lenye
lengo kwa wasomi hao kutumia taaluma walizonazo katika kuitumikia jamii
na taifa kwa ujumla.
"Ninyi
wasomi mmesomeshwa kwa ajili ya kuwatumia wananchi na taifa msaidieni
Rais wetu John Magufuli kuliletea taifa la Tanzania na kanisa maendeleo
kwani hakuna mtu mwingine tunaye mtegemea zaidi yenu" alisema Askofu
Ndabila.
Askofu
Ndabila aliwataka wasomi hao waende kwa wananchi wakawanoe na kuweza
kuwiva kisawasawa ili waendenane na kasi ya maendeleo anayoihitaji Rais
Magufuli.
Alisema
wasomi ndio kundi pekee linaloweza kuitoa nchi katika hatua moja na
kuipeleka katika hatua nyingine ya mbali kimaendeleo na kuwa mambo yao
makubwa watakayo yafanya yataweza kuwabadilisha wananchi na nchi
ikasonga mbele.
"Wananchi
hawahitaji kusikia umahiri wenu wa kuongea kiingereza bali wanataka
kuona ni jinsi gani mtafanya kwa vitendo kuwasaidia ili kulipeleka taifa
mbele kimaenndeleo" alisema Ndabila.
Askofu
Ndabila aliongeza kuwa hivi karibuni hapa nchini ilifika meli kubwa ya
kitabibu ambayo ilikuwa na madakatari ambapo walikuwa wakitoa matibabu
kwa wagonjwa kazi ambayo hata madaktari wasomi wa hapa nchini
wakijipanga wanaweza kuifanya kwa kushirikiana na wadau wengine.
Mtoa
mada katika kongamano hilo, Amina Sanga mhitimu wa Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam (UDSM) alisema vijana wanapaswa kuwa wabunifu badala ya kusubiri
kuajiriwa.Aliwataka
vijana kuacha kutumia mitandao ya kijamii kwa kujibizana mambo ambayo
hayana tija kwa wao na taifa kwa ujuma badala yake waitumie kutafuta
fursa za maendeleo.
"Siku
hizi vile vijiwe vya kupiga domo mitaani havipo tena vimehamia kwenye
makundi ya mitandaoni huko utakuta vijana tena wasomi wakishindani
kujibizana vitu ambavyo havina manufaa kwao na taifa" alisema Sanga.
Mhadhiri
wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Dk.Philip Sanga alisema
mabadiliko ya maendeleo yanaanzia kwa mtu mmoja, jamii na hadi taifa na
ili kupata mabadiliko hayo yanawategemea wasomi na si mtu mwingine.
Mratibu
wa Kongamamo hilo, Ephrahim Mwambapa alisema kongamanao hilo linaundwa
na muungano wa wasomi wa kristo uitwao Tanzania for Jesus Prayer
Movement ambao mlezi wake ni Huduma ya I Go Africa for Jesus.
Mwambapa
alisema lengo la kongamano hilo ni kuona jinsi gani wasomi na
wanataaluma wataweza kutumia taaluma na usomi wao kusaidia jamii badala
ya taaluma hiyo kuachwa bila ya kufanyiwa kazi wakati jamii
inachangamoto nyingi.Tunapokuwa
vyuoni tunakuwa na mipango mingi ya maendeleo lakini baada ya kumaliza
masomo kila mtu anakuwa kivyake wakati tunapaswa kushirikiana na jamii
na ndio maana tumeona ni vizuri kuazisha muungano huu lengo likiwa
kujumuika na jamii katika shughuli za maendeleo ya nchi na dini" alisema
Mwambapa.
Alisema
wazo la kuanzisha muungano huo nimatunda ya mkutano mkuu wa kitaifa wa
kuliombea taifa ulioratibiwa na Askofu Flaston Ndabila na kuhudhuriwa na
watu mbalimbali na vijana kutoka vyuo vikuu uliofanyika Uwanja wa Uhuru
jijini Dar es Salaam mapema mwaka huu.
No comments:
Post a Comment