Na Clarence Nanyaro – NEC
ARUSHA.
Tume
ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imevitaka vyama vya Siasa na wadau
mbalimbali wa Uchaguzi kuhakikisha kuwa Uchaguzi Mdogo wa Madiwani
utakaofanyika kesho (Jumapili) Novemba 22, 2017 unafanyika kwa amani na
Utulivu na kutoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga Kura.
Akisoma
risala kwa umma leo Jijini Arusha Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya
uchaguzi Jaji Semistocles Kaijage amesema kuwa Wapiga Kura wapatao
333,309 wanatarajiwa kupiga Kura kuwachagua Madiwani katika Kata 43 za
Tanzania Bara na kuongeza kuwa uchaguzi huo utafanyika katika Vituo 884
vya Uchaguzi ambako ndipo Wapiga kura walijiandikishia kupiga kura
katika Uchgauzi Mkuu wa Rais,Wabunge na Madiwani wa Mwaka 2015.
Amesema
kuwa tofauti na Chaguzi zilizopita,Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kwa
kuzingatia masharti ya sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa kifungu
cha 62 imewaruhusu wapiga kura ambao ama kadi zao za kupigia kura
zimepotea au kuchakaa au kufutika kutumia vitambulisho mbadala kwenda
katika vituo walivyojiandikisha ili waweze kupiga kura katika uchaguzi
huu.
Jaji
Kaijage amesisitiza kuwa masharti ya Mpiga Kura kuruhusiwa kutumia
kitambulisho mbadala yatazingatia sharti la kwamba majina ya mpiga kura
lazima yafanane kwa herufi na majina yaliyoko katika kitambulisho
mbadala ambayo yako katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura
Ameeleza
kuwa katika kutekeleza hatua hiyo,vitambulisho mbadala ambavyo Tume ya
Taifa ya uchaguzi imeruhusu vitumiwe na Wapiga kura katika uchaguzi
mdogo wa Udiwani ni leseni ya udereva, kitambulisho cha uraia
kinachotolewa na Mamlaka ya utambulisho nchini (NIDA), pamoja na pasi ya
Kusafiria
Aidha,katika
risala hiyo Jaji Kaijage amewataka Wasimamizi na Wasimamizi wasaidizi
wa Uchaguzi katika vituo vya kupigia kura kutoa kipaumbele kwa makundi
maalum wakati wa kupiga kura. Aliyataja makundi hayo kuwa ni Wenye
ulemavu wa aina mbalimbali, Wajawazito, Wenye watoto wachanga, Wazee na
Wagonjwa.
Kuhusu
Mawakala wa vyama vya siasa katika vituo vya Kupigia kura,Jaji Kaijage
aliwasihi kufuata na kuzingatia,sheria Kanuni na taratibu zinazoongoza
Uchaguzi katika kipindi chote cha Kupiga,Kuhesabu na kujumlisha kura
vituoni.
Aidha,
Jaji Kaijage, amewataka Wananchi,wapenzi na Wakereketwa wa vyama
kutofanya kampeni ya aina yeyote katika siku ya upigaji kura ikiwemo
kusambaza Vipeperushi, kuwa na bendera za Vyama vyao, na mavazi na
kuwataka wananchi kueshimu sheria za nchi wakati wote wa upigaji
Kura,kuhesabu na kujumlisha kura.
Katika
Uchaguzi huu mdogo unaofanyika leo,Mkoa wa Arusha unaongoza kwa kuwa na
Kata Nane ambazo zinafanya Uchaguzi huo. Kata hizo ni Ambureni,Makiba
Maroroni, Leguruki na Ngabobo katika Halmashauri ya Meru,Kata ya Musa
katika Halmashauri ya Arusha, Kata ya Muriet katika Jiji la Arusha na
Kata ya Moita katika Halmashauri ya Wilaya ya Monduli.
Uchaguzi
huu ni wa Pili tangu kuanza kwa Mwaka huu,ambapo Tume ya Taifa ya
Uchaguzi inatakiwa kufanya Uchaguzi wa Madiwani mara mbili kwa Mwaka kwa
Mujibu wa sheria. Uchaguzi mdogo mwingine wa Ubunge na Udiwani
ulifanyika Januari 22, 2017.
No comments:
Post a Comment