Wanafunzi wamehamasishwa kujiamini na kusoma kwa bidii ili kujijengea msingi imara ya mafanikio katika maisha yao.
Hayo
yamesemwa leo jijini Dar es salaam na Muasisi wa Dr. Ntuyabaliwe
Foundation, Bi. Jacquiline Mengi alipowatembelea wanafunzi wa shule za
msingi za Muungano na Serengeti zilizopo Manispaa ya Temeke, siku
ambayo duniani kote inaadhimishwa siku ya mtoto Duniani.
Akizungumza
na wanafunzi hao Muasisi wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation amesema ujumbe
wake muhimu kwao wakati wa kuadhimisha siku ya mtoto Duniani ni
kujiamini na kusoma kwa bidii, kwani ndiyo ufunguo wa mafanikio katika
maisha
Akizungumza
katika hafla hiyo Mkurugenzi wa Huduma ya simu kwa Mtoto ( C-SEMA) Bw.
Michael Marwa amewataka watoto kuripoti mara moja kwa njia ya simu
vitendo vya ukatili wanavyofanyiwa watoto ili wahusika wachukuliwe
hatua.
Akitoa
shukrani Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi ya Muungano, Esther Matowo
amesema ujio wa Muasisi wa Taasisi ya Dr Ntubaliwe umewahamasisha
wanafunzi kujitambua na kujua wajibu wao.
Hafla
hiyo ilihudhuriwa pia na Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke
Salum Upunda, Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Serengeti Daud Sabai na
walimu wa shule hizo mbili.
Mwalimu mkuu wa shule ya msingi ya Muungano, Esther Matowo(kushoto) akimkaribisha Mkurugenzi
wa Dr.Ntuyabaliwe Foundation na Miss Tanzania 2000, Bi. Jacqueline
Mengi mara alipowasili shuleni hapo kwenye siku ya maadhimisho ya
siku mtoto Duniani.
Mkurugenzi
wa Dr.Ntuyabaliwe Foundation na Miss Tanzania 2000, Bi. Jacqueline
Mengi akizungumza na wanafunzi wa shule ya Msingi ya Muungano na
Serengeti alipowatembelea katika maadhimisho ya Siku ya Mtoto Duniani
yanayofanyika Novemba 20 ya kila mwaka.
Mkurugenzi wa Huduma ya simu kwa Watoto( C-SEMA) Bw. Michael Marwa akionesha namba ya huduma zinazotumika kuripoti mara moja kwa njia ya simu vitendo vya ukatili wanavyofanyiwa watoto ili wahusika wachukuliwe hatua wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mtoto Duniani yanayofanyika Novemba 20 ya kila mwaka yaliyofanyika katika shuleni hapo.
Afisa Elimu na Ufundi manispaa ya Temeke, Salum B. Upunda aliyemwakilisha Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke akizungumza wakati wa maadhimisho ya Siku ya watoto Duniani mara ya viongozi wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation walipotembelea shuleni hapo .
Mwalimu
mkuu wa shule ya msingi ya Muungano, Esther Matowo akitoa shukrani kwa
uongozi wa Dr.Ntuyabaliwe Foundation kutembelea shuleni hapo na
kuzungumza na wanafunzi wa shule hiyo wakati wa maadhimisho ya siku ya
mtoto Duniani.
Baadhi
ya wanafunzi wa Shule ya Serengeti na Muungano wakifuatilia mada wakati
wa uongozi wa Dr.Ntuyabaliwe Foundation ulipotembelea shule hizo katika
maadhimisho ya siku ya mtoto Duniani.
Mmoja wa wanafunzi akionesha kipaji cha kucheza wakati wa maadhimisho ya simu ya mtoto duniani.
Mkurugenzi
wa Dr.Ntuyabaliwe Foundation na Miss Tanzania 2000, Bi. Jacqueline
Mengi akiwa kwenye picha ya pamoja na wanafunzi wa shule ya msingi ya
Serengeti na Muungano mara baada ya kuzungumza na wanafunzi hao wakati
wa maadhimisho ya siku ya mtoto Duniani.
Mkurugenzi
wa Dr.Ntuyabaliwe Foundation na Miss Tanzania 2000, Bi. Jacqueline
Mengi akiagana na wanafunzi wa shule ya msingi ya Serengeti na Muungano
leo jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment