Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga akizungumza katika hafla
ya Waongoza watalii bora kwa mwaka 2017 iliyofanyika jana katika
ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. Wengine ni
waandaji wa tuzo hiyo. ( Picha na Lusungu Helela- Maliasili)
Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (katikati) akiwa na Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Aloyce Nzuki ( wa
nane kulia) wakiwa kwenye picha ya pamoja na Waongoza watalii bora
kwa mwaka 2017 katika hafla iliyofanyika jana katika ukumbi wa Kimataifa
wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. Wengine ni waandaji wa tuzo
hiyo. ( Picha na Lusungu Helela- Maliasili)
Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga ( wa tano kushoto) akiwa
Wakurugenzi wa taasisi zilizo chini ya Wizara ya Maliasili na utalii
katika hafla ya Waongoza watalii bora kwa mwaka 2017 iliyofanyika
jana katika ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. (
Picha na Lusungu Helela- Maliasili)
Mtendaji
Bodi ya Utalii, Devota Mdachi akiwa na mshindi wa kwanza Peter Philemon
aliyeibuka katika kipengele cha Wapagazi bora kwa mwaka 2017 mara
baada ya kumkabidhi tuzo. Kushoto ni Katibu wa tuzo hiyo, Ally Mtemvu.
Lengo la utoaji tuzo ni kuongeza morali na kuhamasisha utoaji wa huduma
bora na wenye kuzingatia weledi wa hali ya juu kwa watalii nchini.
Mkurugenzi
wa Idara ya Utalii Deogratius Mdamu akimkabidhi cheti na mshindi wa
kwanza, Yohana Tumaini aliyeibuka katika kipengele cha Wapishi bora kwa
mwaka 2017 ikiwa lengo la utoaji tuzo ni kuongeza morali na
kuhamasisha utoaji wa huduma bora na wenye kuzingatia weledi wa hali ya
juu kwa watalii nchini
Baadhi
ya Waongoza watalii bora wakifuatilia kwa makini utoaji wa tuzo kwa
mwaka 2017 katika hafla iliyofanyika jana katika ukumbi wa Kimataifa wa
Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. Picha na Lusungu Helela- Maliasili
Mkurugenzi
wa Masoko wa Hifadhi ya Taifa ya Tanzania,Ibrahim Musa akikamkabidhi
cheti mmoja wa washindi katika katika hafla ya utoaji tuzo kwa waongoza
watalii iliyofanyika jana katika ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere
jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment