Na Mathias Canal, Dar es salaam
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy A.
Mwalimu leo Septemba 4, 2017 amezindua Ugawaji wa vitambulisho vya awali
7296 vya matibabu Bure kwa Wazee katika Halmashauri ya Manispaa ya
Ubungo Jijini Dar es salaam.
Akizungumza
katika uzinduzi huo uliofanyika katika Viwanja vya TP Sinza E Waziri
Ummy alipongeza uongozi wa Wilaya ya Ubungo kwa kutambua umuhimu wa
kutekeleza kwa vitendo maelekezo ya serikali ya kuwatambua Wazee katika
Halmashauri na kuwapatia vitambulisho vitakavyo wawezesha kupata Huduma
za matibabu bila vikwao.
Alisema
kuwa Wazee ni asilimia 5.6 ya wananchi wote wa Tanzania idadi ambayo
kwa kiasi kikubwa inaleta msukumo wa nchi kuweka mifumo madhubuti ya
kuhudumia Wazee ikiwemo kurahisisha upatikanaji wa Huduma katika
matibabu.
Alisema
kuwa Jambo hilo ni kuzingatia ukweli kwamba Wazee wanakabiliwa na
changamoto mbalimbali zinazosababishwa na umri mkubwa na mtazamo wa
Jamii ambao umekuwa ukichangia ukiukwaji wa haki na maslahi ya Wazee
katika ngazi mbalimbali.
Alisema
Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo imeingia kwenye rekodi kwa kuwatambua
Wazee wasio na uwezo kwani watapatiwa vitambulisho vitakavyo wawezesha
kupata Huduma za matibabu Bure.
Mhe
Ummy alisema kuwa Halmashauri zingine kote nchini zinapaswa kuanzisha
haraka zoezi la kuwathamini Wazee kwa kuwapatia Huduma Bora za afya
kabla ya kutoa Huduma za matibabu kwa Wazee kote nchini kwa kuanzisha
dirisha maalumu na wataalamu wa kuwahudumia Wazee.
Alitoa
Rai kwa watoa Huduma wa Afya kuviheshimu vitambulisho wakati wote Wazee
wanapoenda navyo kupatiwa matibabu huku akiwasihi Wazee kutumia
vitambulisho hivyo kwa kuzingatia maelekezo sio kwa kuwapa watu wengine
wasiohusika navyo.
Aidha
waziri Ummy ameahidi bima ya afya kwa watoto 100 wenye umri chini ya
miaka 18 wanaoishi kwenye mazingira magumu wilaya ya Ubungo na
uandikishwaji utaanza leo pia ameahidi kujenga wodi ya wazazi, watoto na
maabara ya damu kwenye kituo kimoja cha afya wilaya ya ubungo mara
baada ya kusikia hotuba ya kaimu mganga mkuu wa wilaya ya Ubungo.
Muheshimiwa
waziri ameiomba jamii kujiunga na bima za afya za gharama nafuu ili
kupunguza mzigo kwa halmashauri na kulinda afya za wananchi.Kwa upande
wake Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori alisema kuwa lengo la
uzinduzi huo wa ugawaji wa vitambulisho ni kuonesha umma kuwa Wilaya ya
Ubungo inawajali Wazee ikiwa ni Sehemu ya utekelezaji wa ilani ya
ushindi ya Chama Cha Mapinduzi katika kipindi Cha mwaka 2015-2020, sera
ya Taifa ya Wazee ya mwaka 2003 na sera ya Afya ya Mwaka 2007.
Mhe
Makori alisema kuwa serikali ya awamu ya tano chini ya Uongozi wa
Mheshimiwa Dkt John Pombe Magufuli imejipanga kuhakikisha Wazee wote
nchini wanapata Huduma Bora za afya bila vikwao hivyo Wilaya ya Ubungo
imeanza na utoaji vitambulisho kea Wazee 7296 waliojiandikisha na zoezi
hilo litakuwa endelevu.
Naye
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akizungumza na
mtandao wa www.wazo-huru.blogspot.com mara baada ya uzinduzi wa ugawaji
wa vitambulisho vya Tiba kwa Wazee alisema kuwa Manispaa ya Ubungo
imetekeleza agizo la serikali lililotolewa na Waziri Mkuu kwenye
maadhimisho ya siku ya Wazee Octoba 1, 2009 kuwa Hospitali zote na Vituo
vya Afya vya Umma kutenga dirisha na watumishi maalumu wa Afya kwa
ajili ya kutoa Huduma za matibabu bure kwa Wazee.
Mkurugenzi
Kayombo alisema kuwa Manispaa ya Ubungo ina jumla ya Vituo 19 vya
kutolea Huduma za afya ikiwa ni pamoja na Hospitali moja, Vituo vya afya
vitatu, Zahanati 15, na Kliniki Moja ya Mama na Mtoto hivyo Vituo hivyo
vyote vitaanza kutoa Huduma za matibabu kwa Wazee wasio na uwezo bila
malipo.
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy A.
Mwalimu akizungumza wakati wa uzindua wa Ugawaji wa vitambulisho vya
matibabu Bure kwa Wazee katika Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Jijini
Dar es salaam.
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy A.
Mwalimu (Wa Tatu Kushoto) akionyesha vitambulisho vya Wazee akiwa na
viongozi wengine wa Chama na serikali Wilaya ya Ubungo wakati wa Ugawaji
wa vitambulisho vya matibabu Bure kwa Wazee katika Halmashauri ya
Manispaa ya Ubungo Jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi
wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akisalimiana na baadhi ya
Wazee walioshiriki uzinduzi wa Ugawaji wa vitambulisho vya matibabu
Bure kwa Wazee katika Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Jijini Dar es
salaam.
Kaimu
Mganga Mkuu Wilaya ya Ubungo Bi Maria Maliwa akisoma taarifa ya huduma
za afya, Ustawi wa jamii na Msamaha kwa niaba ya Mkurugenzi wa Manispaa
ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo katika uzinduzi wa vitambulisho vya
msamaha kwa wazee wa Manispaa ya Ubungo.
Zoezi
la Uzinduzi wa Ugawaji wa vitambulisho vya awali 7296 vya matibabu Bure
kwa Wazee katika Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Jijini Dar es
salaam
Mkuu
wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori akizungumza kabla ya kumkaribisha
mgeni rasmi kwa ajili ya uzinduzi wa Ugawaji wa vitambulisho vya awali
7296 vya matibabu Bure kwa Wazee katika Halmashauri ya Manispaa ya
Ubungo Jijini Dar es salaam.
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy A.
Mwalimu akimpatia Mzee Ferooz Kafuru kitambulisho Cha matibabu wakati wa
uzindua wa Ugawaji wa vitambulisho vya matibabu Bure kwa Wazee katika
Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Jijini Dar es salaam.
Baadhi
ya Wazee wa Halmshauri ya Manispaa ya Ubungo wakishuhudia zoezi la
Ugawaji wa vitambulisho vya awali 7296 vya matibabu Bure kwa Wazee.
Zoezi hili limezinduliwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto Mhe Ummy A. Mwalimu Septemba 4, 2017
Katibu
wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Ubungo Ndg Salum A. Kalli akitoa
salamu za CCM wakati wa uzinduzi wa Ugawaji wa vitambulisho vya awali
7296 vya matibabu Bure kwa Wazee katika Halmashauri ya Manispaa ya
Ubungo Jijini Dar es salaam.Kalli amepongeza uongozi wa serikali Wilaya
ya Ubungo kwa kutekeleza ilani ya CCM ya ushindi yenye mkataba na
wananchi kwa kipindi cha miaka mitano 2015-2020
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy A.
Mwalimu akiteta Jambo na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John
Lipesi Kayombo mara baada ya kuzindua Huduma ya Ugawaji wa vitambulisho
vya matibabu Bure kwa Wazee katika Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo
Jijini Dar es salaam.
Mkuu
wa Walaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori akisalimiana na Wazee waliofika
kushuhudia zoezi la uzinduzi wa vitambulisho kwa Wazee wa Halmashauri ya
Manispaa ya Ubungo lilifanywa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy A. Mwalimu.
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy A.
Mwalimu akimpatia Bi Theresia Mbimbo kitambulisho Cha matibabu wakati wa
uzindua wa Ugawaji wa vitambulisho vya matibabu Bure kwa Wazee katika
Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Jijini Dar es salaam.
Baadhi
ya Wazee wa Halmshauri ya Manispaa ya Ubungo wakishuhudia zoezi la
Ugawaji wa vitambulisho vya awali 7296 vya matibabu Bure kwa Wazee.
Zoezi hili limezinduliwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto Mhe Ummy A. Mwalimu Septemba 4, 2017 .
Baadhi
ya Wazee wa Halmshauri ya Manispaa ya Ubungo wakishuhudia zoezi la
Ugawaji wa vitambulisho vya awali 7296 vya matibabu Bure kwa Wazee.
Zoezi hili limezinduliwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto Mhe Ummy A. Mwalimu Septemba 4, 2017
Baadhi
ya Wazee wa Halmshauri ya Manispaa ya Ubungo wakishuhudia zoezi la
Ugawaji wa vitambulisho vya awali 7296 vya matibabu Bure kwa Wazee.
Zoezi hili limezinduliwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto Mhe Ummy A. Mwalimu Septemba 4, 2017
Madiwani
wa Manispaa wakishuhudia zoezi la Ugawaji wa vitambulisho vya awali
7296 vya matibabu Bure kwa Wazee. Zoezi hili limezinduliwa na Waziri wa
Afya.
Post a Comment