Hospitali
ya Taifa Muhimbili (MNH) leo imezindua muongozo utakaosaidia
kuwahudumia watoto wachanga ( Neonatal Guideline) wenye umri kuanzia
siku 0 hadi siku 28 ili kuhakikisha wanapata huduma inayostahiki.
Muongozo
huo umeandaliwa na madaktari wa MNH na kupitiwa na wadau mbalimbali
wakiwemo wataalam kutoka Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi
Muhimbili (MUHAS) pamoja na Chuo Kikuu cha Kwazulu Natal kilichopo
Afrika Kusini.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Profesa Lawrence Museru
amesema muongozo huo si tu unamanufaa kwa MNH bali pia una manufaa kwa
hospitali zingine kwani utawezesha mtoto kupata tiba inayotakiwa hata
sehemu ambazo hakuna watalaam.
Kwa
upande wake Daktari Bingwa wa Watoto Edna Majaliwa ambaye pia ni Mkuu wa
Kitengo cha Watoto Wachanga wa hospitali hiyo amesema kuwepo kwa
muongozo huo kutasaidia kupunguza vifo vya watoto wachanga sanjari na
kupunguza rufaa za watoto hao kuletwa Muhimbili .
‘’
Kusudio letu ni kuendelea kupunguza vifo vya watoto wachanga , MNH
tumefanikiwa kupunguza vifo hivyo kutoka 26 kwa kila vizazi hai 1,000 na
kufikia 18 kwa kila vizazi hai 1,000. Kwa mwaka watoto wanaozaliwa hapa
ni takribani 10,000 hivyo naamini muongozo huuu utaleta mabadiliko
makubwa‘’ amesema Dk. Majaliwa.
Pia
ameelezea vyanzo vinavyosababisha vifo vya watoto wachanga kuwa ni
madhara ya kuwa njiti, mtoto ambaye amezaliwa na hakulia pamoja na mtoto
mwenye vimelea vya bakteria.
Akiwasilisha
mada kuhusu muongozo huo , Daktari wa watoto , Jullieth Cosmas ametaja
sababu zinazochangia watoto wachanga kulazwa Hospitalini kuwa ni mtoto
kuzaliwa kabla ya wakati(Njiti) mtoto kushindwa kupumua vizuri pindi
anapozaliwa , mtoto kupata maambukizi , mtoto kutolia wakapi alipozaliwa
na mtoto kuumia wakati akizaliwa.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence
Museru akizungumza katika uzinduzi wa kitabu chenye mwongozo jinsi ya
kutoa huduma ya afya kwa watoto wachanga wenye umri sufuri hadi siku 28.
Uzinduzi huo umefanyika leo katika hospitali hiyo.
Madaktari
na wauguzi wakiwa kwenye mkutano wa kuzindua kitabu kinachoelezea jinsi
ya kuwahudumia watoto wachanga baada ya kuzaliwa.
Daktari wa watoto wa hospitali hiyo, Dk. Judith Cosmas ambaye ameshiriki kuaanda kitabu hicho akizungumza kwenye mkutano huo.
Baadhi ya wataalamu wa afya wakiwa kwenye mkutano huo leo.
Mkuu
wa Idara ya Watoto, Dk. Merry Charles akisisitiza jambo huku akionesha
kitabu hicho ambacho kitakuwa kikitumika wakati wa kuwahudumia watoto
hao.
Mkurugenzi Mtendaji, Profesa Museru (kaunda suti) akiwa kwenye mkutano huo leo.
Mkurugenzi wa hospitali hiyo akiwa katika picha ya pamoja na wataalamu wa afya MNH na wadau mbalimbali.
No comments:
Post a Comment