Afisa
wa NIDA Wilaya ya Ikungi Agness Mtei akimpa maelekezo Mkuu wa Wilaya ya
Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu ya namna vitambulisho vya Taifa
vinavyotengenezwa mara baada ya kuzinduzi zoezi la usajili na utambuzi
kwa wananchi kwa ajili ya kupatiwa vitambulisho vya Taifa.
Na Mathias Canal, Singida.
Zoezi
linalotekelezwa na serikali kupitia Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa
(NIDA) iliyo chini ya Wizara ya Mambo ya ndani ya Nchi la usajili na
utambuzi wa watu wanaoishi katika Wilaya ya Ikungi wenye umri wa kuanzia
miaka 18 na kuendelea limezinduliwa rasmi huku wananchi wakihamasishwa
kutoa ushirikiano katika zoezi Hilo.
Zoezi
Hilo litatekelezwa katika awamu nne ambapo katika awamu ya kwanza
utekelezaji wake utakuwa katika Tarafa ya Ikungi yenye Kata sita kwa
wananchi wapatao 45,599, Awamu ya Pili itakuwa Ni Tarafa ya Sepuka yenye
Kata Saba na wananchi wakiwa Ni 49,035, Awamu ya Tatu Ni Tarafa ya
Ihanja yenye Kata nne huku wananchi wakiwa 54,887 na awamu ya nne
itakuwa katika Tarafa ya Mungaa yenye Kata Saba na jumla ya wananchi
wapatao 35,311.
Akizungumza
Katika Kijiji na Kata ya Dung'unyi kwenye uzinduzi wa zoezi la usajili
na utambuzi kwa wananchi kwa ajili ya kupatiwa vitambulisho vya Taifa
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu alisema kuwa zoezi
Hilo linalenga kupata taarifa sahihi za watu zitakazotumiwa na mifumo
Yote ya serikali na binafsi kubadilishana taarifa kwa lengo la kuboresha
Huduma na kuinua hali za watu kutoka kipato Cha chini kwenda Cha Kati.
Alisema
umuhimu wa zoezi Hilo Ni Kuimarisha ulinzi na usalama wa Nchi hususani
maeneo ya mipakani, Wananchi kushiriki kikamilifu katika shughuli za
uzalishaji Mali hususani Biashara, usalama katika miamala ya kibenki
pamoja na kuwezesha wananchi kukopeshana kirahisi, Upatikanaji kirahisi
wa pembejeo na zana za Kilimo, na Wananchi katika Kaya maskini
kutambulika haraka na kupata misaada kupitia TASAF.
Umuhimu
mwingine Ni Upatikanaji wa mikopo ya elimu ya just, Kupunguza
ukiritimba katika upatikanaji wa Huduma za Jamii na Kupunguza serikali
gharama za kusafirisha daftari la wapinga kura na kuwa na daftari lenye
taarifa sahihi za watu na mahali walipo.
Mhe
Mtaturu aliwataka wananchi kutoa taarifa sahihi na kutoa ushirikiano wa
karibu kwa viongozi, Wataalamu na wasimamizi wa zoezi Hilo
waliokasimishwa jukumu la usajili.
Alisema
kuwa wananchi wote wanapaswa kuwa na viambatanisho muhimu ambavyo Ni
Cheti Cha kuzaliwa, Kadi ya kupinga kura, Vyeti vya shule, Pass ya
kusafiria (Passport), Leseni ya udereva, Kadi ya Bima ya Afya, Kadi ya
Mfuko wa hifadhi ya jamii, Nambari ya utambulisho ya mlipa Kodi na
Kitambulisho Cha Mzanzibari Mkaazi.
Alisema
kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe
Magufuli ameagiza kufanyika kwa zoezi Hilo Bure kote nchini ili wananchi
waweze kupata haki yao ya Msingi ya kusajiliwa na kutambulika katika
Taifa lao.
Mhe
Mtaturu alisisitiza kila mmoja kukemea kwa vitendo viashiria vyote vya
Rushwa, ama udanganyifu utakaofanywa na wachache wasioitakia mema Nchi
kwa kuzorotesha zoezi Hilo.
Katika
kuhakikisha zoezi linafanyika Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA)
Kupitia Ofisi ya Wilaya ya Ikungi inakamilisha jukumu lake la kusajili
wananchi ambao Ni Raia halali pamoja na uchukuaji wa alama za
kibaiolojia katika awamu zote nne.
Mkuu
wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akizungumza na wananchi
kwenye mkutano wa hadhara wakati wa zoezi la usajili na utambuzi kwa
wananchi kwa ajili ya kupatiwa vitambulisho vya Taifa katika Kijiji na
Kata ya Dung'unyi.
Katibu
wa Cha Cha Mapinduzi Wilaya ya Ikungi Ndg Philiph Elieza akitoa salama
za chama kwa wananchi kwenye mkutano wa hadhara wakati wakati wa zoezi
la usajili na utambuzi kwa wananchi kwa ajili ya kupatiwa vitambulisho
vya Taifa katika Kijiji na Kata ya Dung'unyi.
Wananchi
Kijiji na Kata ya Dung'unyi wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe
Miraji Jumanne Mtaturu wakati wa zoezi la usajili na utambuzi kwa
wananchi kwa ajili ya kupatiwa vitambulisho vya Taifa katika.
Makamu
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Mhe akitoa salamu wakati
wa zoezi la usajili na utambuzi kwa wananchi kwa ajili ya kupatiwa
vitambulisho vya Taifa katika.
Afisa
wa NIDA Wilaya ya Ikungi Bi Agness Mtei akisoma taarifa ya zoezi la
usajili na utambuzi kwa wananchi kwa ajili ya kupatiwa vitambulisho vya
Taifa katika.
Maafisa
wa NIDA Wilaya ya Ikungi wakiwasalimu wakazi wa kijiji na Kata ya
Dung'unyiwakati wa zoezi la usajili na utambuzi kwa wananchi kwa ajili
ya kupatiwa vitambulisho vya Taifa katika. Kulia ni Agness Mtei, Doris
Niyukuri na Mary Maputa
Wananchi
Kijiji na Kata ya Dung'unyi wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe
Miraji Jumanne Mtaturu wakati wa zoezi la usajili na utambuzi kwa
wananchi kwa ajili ya kupatiwa vitambulisho vya Taifa katika.
Katibu
Tawala Wilaya ya Ikungi akizungumza kabla ya kumkaribisha Mkuu wa
Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu wakati wa zoezi la usajili
na utambuzi kwa wananchi kwa ajili ya kupatiwa vitambulisho vya Taifa
katika Kijiji na Kata ya Dung'unyi.
Wananchi
Kijiji na Kata ya Dung'unyi wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe
Miraji Jumanne Mtaturu wakati wa zoezi la usajili na utambuzi kwa
wananchi kwa ajili ya kupatiwa vitambulisho vya Taifa katika.
Mkuu
wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akisalimiana na wananchi
mara baada ya kuwasili Kijiji na Kata ya Dung'unyi wakati wa zoezi la
usajili na utambuzi kwa wananchi kwa ajili ya kupatiwa vitambulisho vya
Taifa katika Kijiji na Kata ya Dung'unyi.
No comments:
Post a Comment