Mkurugenzi
mkuu wa Idara ya Masoko na Usambazaji wa Vodacom Tanzania PLC, Hisham
Hendi(kulia) akimshuhudia Mwakilishi wa timu ya Yanga ambaye ni Afisa
habari wa timu ya Simba, Haji Manara(kushoto) baada ya timu hiyo kukosa
mwakilishi akimtania mmoja wa vijana aliyeitambulisha jezi ya Yanga
itakayotumika katika msimu wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara
2017/2018 wakati wa hafla iliyoandaliwa na Vodacom Tanzania ya
kukabidhi vifaa kwa timu 16 zinazoshiriki ligi hiyo jana jijini Dar es
Salaam.
Ofisa
Mtendaji Mkuu wa bodi ya ligi, Boniface Wambura akipokea keki toka kwa
Mkurugenzi mkuu wa Idara ya Masoko na Usambazaji wa Vodacom Tanzania
PLC, Hisham Hendi(kulia)kuashiria Uzinduzi wa msimu mpya wa ligi kuu ya
Vodacom Tanzania bara,wakati wa hafla iliyoandaliwa na Vodacom Tanzania
ya kukabidhi vifaa kwa timu 16 zinazoshiriki ligi hiyo jana jijini Dar
es Salaam.
Mkurugenzi
mkuu wa Idara ya Masoko na Usambazaji wa Vodacom Tanzania PLC, Hisham
Hendi(kulia)akimpongeza mmoja wa vijana aliyeitambulisha jezi ya Azam FC
wakati wa hafla iliyoandaliwa na Vodacom Tanzania ya kukabidhi vifaa
kwa timu 16 zinazoshiriki ligi hiyo jana jijini Dar es Salaam,Kutoka
kushoto ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa bodi ya ligi, Boniface Wambura na
Mwakilishi wa Timu hiyo, Jafari Maganga.
Ofisa
Mtendaji Mkuu wa bodi ya ligi, Boniface Wambura(kushoto)akiwashuhudia
mwakilishi wa timu ya Simba Afisa habari wa timu hiyo, Haji
Manara(watatu kushoto)pamoja na Mkurugenzi mkuu wa Idara ya Masoko na
Usambazaji wa Vodacom Tanzania PLC, Hisham Hendi(kulia)wakiwapongeza
vijana walioitambulisha jezi ya nyumbani na ugenini ya timu hiyo wakati
wa hafla iliyoandaliwa na Vodacom Tanzania ya kukabidhi vifaa kwa timu
16 zinazoshiriki ligi hiyo jana jijini Dar es Salaam.
Timu
zinazoshiriki ligi kuu ya Vodacom tanzania bara zimekabidhiwa vifaa
mbalimbali na mdhamini mkuu wa ligi hiyo Kampuni ya mawasiliano ya
Vodacom Tanzania, vifaa hivyo vilivyokabidhiwa kwa timu zinazoshiriki
ligi hiyo vina thamani ya zaidi ya shilingi milioni 500/=
Akikabidhi
vifaa hivyo jana jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi mkuu wa Idara ya
Masoko na Usambazaji wa kampuni hiyo, Hisham Hendi, alisema kuwa kwa
mara nyingine tena katika kuhakikisha ligi ya soka nchini inaenda vizuri
Vodacom inakabidhi vifaa mbalimbali vya ligi ambavyo ni jezi
mbalimbali, viatu vya mazoezi na mechi, soksi, vilinda ugoko, nguo za
mazoezi, nguo za kawaida, gloves, mabegi ya kusafiria, nguo za marefa,
bendera, substitution boards na vifaa vingine vingi vinavyohitajika.
“Tunajisikia furaha kukabidhi vifaa hivi siku ya leo tukiwa
tunatekeleza matakwa ya mkataba wa udhamini, ni imani yetu kwamba timu
zitakazoshiriki ligi zimejiandaa vya kutosha kwa msimu mpya wa ligi wa
2017/2018”Alisema Hendi.
Hendi
alisema Vodacom inaendelea kudhamini ligi kuu kwa sababu soka ni mchezo
unaopendwa sana hapa nyumbani ukiwa na washabiki wengi hivyo inapenda
kuona wananchi ambao baadhi yao ni wateja wake wanapata burudani ya
mchezo waupendao pia siku zote inaamini kuwa michezo ni ajira kubwa
duniani kote, ikiendelezwa inaweza kubadilisha maisha ya watu wengi na
taifa kunufaika kwa mapato makubwa ya kodi kutoka katika sekta hii.
Aliwataka
wadhamini wengine kujitokeza ili kuboresha zaidi ligi ya Tanzania na
kuongeza maslahi kwa wachezaji wanaoshiriki katika ligi “Tukiunganisha
nguvu timu zetu zinaweza kuwa na wachezaji wa kimataifa pia ni muhimu
kwa wadau mbalimbali kuanza kuwekeza katika timu za vijana chipukizi
kwa kuwa vipaji vinaanzia ngazi ya chini ambako vinapaswa kuibuliwa na
kuendelezwa ”Alisema Hendi.
Naye
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi,Boniface Wambura aliishukuru hiyo,
na kuzitaka klabu zinazoshiriki ligi hiyo kuheshimu chapa ya mdhamini
wakati wote wa mechi za ligi. “Ninatoa mwito kwa klabu zote kutumia jezi
zenye nembo ya mdhamini mkuu katika kuhakikisha ligi inafanikiwa kama
inavyotakiwa,”alisema.
Aliongeza
kuwa TFF isingependa kutumia kanuni na sheria kuadhibu klabu
inayokwenda kinyume, bali kila klabu izingatie masharti ya mdhamini
kama ambavyo anavyotimiza haki yake ya kuwapatia vifaa.
Alisema
ligi ya mwaka huu itakuwa bora kutokana na maandalizi yote kukamilika
mapema pia timu zitazoshiriki zimejiandaa vya kutosha kuhakikisha ligi
inakuwa na msisimko na ushindani mkubwa.
No comments:
Post a Comment