Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza
na wakulima, wadau wa kilimo na wananchi kwa ujumla wakati wa kufunga maadhimisho
ya sikukuu ya wakulima, (Nane nane) ambayo kitaifa yamefanyika katika viwanja
vya Ngongo, Manispaa ya Lindi leo tarehe 8 Agosti 2017.(Picha zote na Mathias Canal)
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (Kushoto)
akijadili jambo na Mbunge wa Viti maalumu mkoa wa Lindi Mhe Salma Kikwete wakati
alipotembelea Mabanda ya Maonesho ya Nanenane katika viwanja vya Ngongo,
Manispaa ya Lindi leo tarehe 8 Agosti 2017.
Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi, Mhe Dkt Dk Charles Tizeba akisisitiza jambo kabla ya kufungwa kwa Maonesho ya Nanenane katika viwanja vya
Ngongo, Manispaa ya Lindi leo tarehe 8 Agosti 2017.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi
Mhandisi Methew Mtigumwe akiwasalimu wakulima, wadau wa kilimo na wananchi kwa
ujumla wakati wa sherehe za Maonesho ya Nanenane katika viwanja vya Ngongo, Manispaa ya Lindi leo
tarehe 8 Agosti 2017.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (Kushoto)
akisikiliza maelezo kuhusu Teknolojia ya Serikali ya Mtandao Kutoka kwa Bi Caroline Munuo Marealle Mtaalamu
wa Teknolojia, Habari na Mawasiliano (TEHAMA) wa Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi wakati
alipotembelea banda la wizar ahiyo wakati wa Maonesho ya Nanenane katika viwanja vya Ngongo,
Manispaa ya Lindi leo tarehe 8 Agosti 2017.
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango
akizungumza kabla ya kufungwa kwa Maonesho ya Nanenane katika viwanja vya Ngongo, Manispaa ya Lindi leo
tarehe 8 Agosti 2017.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akisikiliza maelezo kuhusu utuzwaji wa bata mzinga kwenye banda la JKT
wakati wa kufunga maadhimisho
ya sikukuu ya wakulima, (Nane nane) ambayo kitaifa yamefanyika katika
viwanja
vya Ngongo, Manispaa ya Lindi leo tarehe 8 Agosti 2017.
Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi
Zanzibar, Mhe. Hamad Rashid Mohamed akihimiza jambo alipokuwa akizungumza kabla
ya kufungwa kwa Maonesho
ya Nanenane katika viwanja vya Ngongo, Manispaa ya Lindi leo tarehe 8 Agosti
2017.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akimshukuru Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea Mkoani Lindi Mhe Rukia Muwango
kwa zawadi mbalimbali wakati alipotembelea banda la Halmashauri ya
Wilaya ya Nachingwea kabla ya kufunga maadhimisho
ya sikukuu ya wakulima, (Nane nane) ambayo kitaifa yamefanyika katika
viwanja
vya Ngongo, Manispaa ya Lindi leo tarehe 8 Agosti 2017.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Greyson
Lwenge akihimiza jambo alipokuwa akizungumza kabla
ya kufungwa kwa Maonesho
ya Nanenane katika viwanja vya Ngongo, Manispaa ya Lindi leo tarehe 8 Agosti
2017.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
alipotembelea Shamba Darasa la JKT kabla ya kufunga maadhimisho
ya sikukuu ya wakulima, (Nane nane) ambayo kitaifa yamefanyika katika
viwanja
vya Ngongo, Manispaa ya Lindi leo tarehe 8 Agosti 2017.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya
Utafiti Dkt Hussein Mansoor kuhusu kilimo cha mazao mbalimbali mara
baada ya kutembelea banda la Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi kabla ya
kufunga maadhimisho
ya sikukuu ya wakulima, (Nane nane) ambayo kitaifa yamefanyika katika
viwanja
vya Ngongo, Manispaa ya Lindi leo tarehe 8 Agosti 2017.
Baadhi ya Wananchi Kutoka Mkoa wa Lindi na Mtwara wakimsikiliza kwa makini Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
wakati akihutubia maadhimisho
ya sikukuu ya wakulima, (Nane nane) ambayo kitaifa yamefanyika katika
viwanja
vya Ngongo, Manispaa ya Lindi leo tarehe 8 Agosti 2017.
Na Mathias
Canal, Lindi
Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo tarehe 8
Agosti 2017 amefunga maadhimisho ya sikukuu ya wakulima, (Nane nane) ambayo
kitaifa yamefanyika katika viwanja vya Ngongo, Manispaa ya Lindi.
Akizungumza
wakati akiwahutubia wakulima, wadau wa kilimo na wananchi kwa ujumla Makamu wa
Rais amesema kuwa serikali inahakikisha kuwa kila Mtanzania ananufaika na fursa
mbalimbali za uchumi zilizopo nchini, Kwa kutambua kuwa zaidi ya asilimia 65.5
ya watanzania wanajihusisha ama wameajiriwa na kujiajiri katika sekta za
Kilimo, Ufugaji na uvuvi.
Alisema kuwa serikali inaendelea kuchukua
hatua mbalimbali na za makusudi za
kuimarisha sekta hizo za Kilimo Mifugo na Uvuvi kwa kuzifuta na kuzipunguza
baadhi ya Kodi, Tozo na Ada ambazo zimekuwa kero kwa wakulima na wananchi.
Alisema kuwa
pamoja na kuzifuta na kuzipunguza Kodi, Tozo na Ada lakini pia serikali imechukua
hatua za makusudi za kupunguza ushuru wa mazao uliokuwa unatozwa na Serikali za
Mitaa kutoka asilimia 5 hadi asilimia 3 kwa mazao ya biashara na asilimia 2 kwa
mazao ya chakula.
Mhe Suluhu alitilia msisitizo
kuwa kuanzia sasa ni marufuku kwa mtu yeyote kutoza ushuru kwa mazao
yanayosafirishwa kutoka Halmashauri moja kwenda nyingine, ambayo uzito wake
hauzidi tani moja kwani ushuru wa mazao unatozwa
kwenye Halmashauri ambako mazao hayo yanatokea na siyo kila yanakopita.
Hatua nyingine
iliyochukuliwa ni ya kusamehe kodi ya ongezeko la thamani kwenye vyakula vya
mifugo vinavyotengenezwa hapa nchini ili kupunguza gharama ya kununua chakula
hicho kwa wafugaji.
Aidha, alisema
kuwa Serikali pia imesamehe kodi ya ongezeko la thamani kwenye mayai ya kutotoleshea
vifaranga, lengo likiwa ni kupunguza gharama ya uzalishaji vifaranga na kukuza
Sekta ndogo ya Ufugaji ili iweze kuongeza mchango wake katika Pato la Taifa.
Makamu wa
Rais Mhe Samia Suluhu Hassan alisema kuwa serikali itaendelea kuboresha na kuendeleza
misingi mahususi ili kuongeza kasi ya kuleta mapinduzi makubwa katika kilimo,
mifugo na uvuvi.
Alisema kuwa kauli mbiu ya Maonesho ya Nanenane
inayosema “Zalisha kwa Tija Mazao na
Bidhaa za Kilimo Mifugo na Uvuvi ili kufikia uchumi wa kati” inaunga mkono
juhudi za Serikali za kufikia uchumi wa kati unaoendeshwa na viwanda ifikapo
mwaka 2025.
Awali Mhe
Samia akisoma salamu za Mhe. Rais wa Jamhurri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt
John Pombe Magufuli alisema kuwa Mhe Rais anawapongeza wananchi kwa kuendelea
kumuunga mkono kwenye jitahada za mapambano dhidi Rushwa, kurudisha nidhamu kwa
watumishi wa umma na kujenga Tanzania mpya yenye kuendeshwa na uchumi wa
viwanda huku akiwaomba wananchi kuendelea
kulipa kodi kwa wakati na kudai risiti kila wanunuapo bidhaa.
Alisema kuwa Mhe Rais Magufuli yupo bega kwa bega na
wananchi na ataendelea kupunguza utitiri wa kodi kwa wakulima, wafugaji na
wavuvi.
No comments:
Post a Comment