Pages

July 29, 2017

WATOTO WA KIKE WAASWA KUSOMA MASOMO YA SAYANSI NA HISABATI


Mgeni Rasmi Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, anayeshughulukia Muungano na Mazingira January Makamba (kulia) akimsikiliza Msajili wa Bodi ya Wahandisi nchini Tanzania(ERB) Mhandisi Patrick Balozi (kushoto) akitoa neno la utangulizi wakati wa uzinduzi wa kongamano la tatu la wahandisi wanawake nchini mapema hii leo jijini Dar es Salaam.

Mgeni Rasmi Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, anayeshughulukia Muungano na Mazingira January Makamba (kulia) akimsikiliza Mwenyekiti wa Chama cha Wahandisi Wanawake nchini Mhandisi Alice Isibike akielezea changamoto wanazokutana nazo wahandisi wanawake mapema hii leo wakati wa uzinduzi wa kongamano la tatu la wahandisi wanawake nchini mapema hii leo jijini Dar es Salaam.

Mgeni Rasmi Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, anayeshughulukia Muungano na Mazingira January Makamba akizungumza na wahandisi wanawake nchini wakati akizindua kongamano la tatu la wahandisi wanawake nchini mapema hii leo jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya wahandisi wanawake wakimsikiliza Mgeni Rasmi Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, anayeshughulukia Muungano na Mazingira January Makamba wakati akizindua kongamano la tatu la wahandisi wanawake nchini mapema hii leo jijini Dar es Salaam.Picha na Eliphace Marwa – Maelezo





Na. Paschal Dotto- MAELEZO


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano Mhe. Janauary Makamba amewaasa watoto wa kike kusoma masomo ya sayansi ambayo yatawawezesha kupata utaalamu katika fani ya uhandisi.

Akizungumza kwa niaba ya Makamu wa Rais katika Tamasha la Wahandisi wanawake(TAWECE) lililofanyika katika ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es salamu Mhe. Makamba amesema kuwa katika juhudi za kujenga taifa la viwanda fani ya uhandisi ni muhimu hivyo watoto wakike hawana budi kuweka kipaumbele katika masomo ya sayansi.

“katika hali ya kawaida wahandisi wa kike ni wachache kulinganisha na wahandisi wa kiume hii ni kutoka na kuwepo kwa imani kuwa masomo katika kada hii ni ya wanaume na si wanawake kama watoto wengi wanavyojua,watoto wa kike onyesheni tofauti someni masomo ya sayansi muweze kutoa mchango kwa taifa “ Alisema Waziri Makamba.

Pia Waziri Mhe. Makamba ameishukuru Serikali ya Norway kwa kutoa nafasi kwa masomo kwa watoto wa kike kusomea uhandisi kwani hali hii imesaidia kuongeza idadi ya wahandisi wa kike kutoka 96 kwa mwaka 2010 hadi kufikia wahandisi 379 kwa mwaka huu.

Naye Mwenyekiti wa chama hicho Mhandisi Alice Sibike ameishauri Serikali ya Tanzania kuwawezesha watoto wa kike katika kuwapa fursa kwa kuwapa mikopo elimu ya juu ili kusaidia kuongeza idadi ya watoto wa kike wanaosoma fani uhandisi.

Katika kutekeleza kwa vitendo mpango huo chama hicho kimeanza kutembelea shule mbalimbali na kutoa elimu kwa watoto wa kike kusoma masomo ya sayansi ambapo mpaka sasa wameshatembelea shule za Azania, Feza girls na Tambaza zote za jijini Dar es salaam.

Mwenyekiti wa usajili wahandisi Mhandisi Patrick Balozi amesema ipo haja ya watoto wa kike na jamii kwa ujumla kuhamasika kuweka kipaumbele cha masomo ya sayansi kwa watoto wa ili kuunga mkono juhudi za serikali za kuwa na uchumi wa viwanda.

Tanzania ina jumla ya wahandisi 19,164 ambao kati yao wanawake ni 1,763 huku wahandisi 4831 wako mafunzoni baada ya kumaliza masomo na kati yao wa kike ni 372.

“tunahitaji wahandisi 80000 ili kukidhi mahitaji ya kujenga nchi ya viwanda lakini watoke katika jinsia zote ili kuweka mfumo sawa katika kutenda kazi”, Alisema Mhandisi Balozi

Tamasha la chama hicho lilianza rasmi mwaka 2015 na lengo ni kuwakutanisha wahandishi wote wa kike ili kubadilishana ujuzi na pia kuwawezesha watoto wa kike kujifunza kutoka kwa wahandisi wenye uzoefu

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...