Pages

July 29, 2017

CHANJO YA HOMA YA INI KUPATIKANA KWA WANANCHI WOTE MPAKA KUFIKIA 2020


Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu akiwahutubia waandishi nwa habari (Hawapo kwenye picha) katika kilele cha maazimisho ya siku ya Homa ya Ini Duniani yaliyofanyika leo katika ofisi ndogo za Wizara ya Afya jijini Dar es salaam. Kushoto ni Mganga mkuu wa Serikali Pro Muhamad Bakari kambi na Kulia ni Afisa kutoka kitengo cha magonjwa ya Mlipuko Dkt. Azma Simba.

Waandishi wa habari kutoka vyombo tofauti wakifuatilia kwa ukaribu tamko la kilele cha maadhimisho ya Homa ya Ini Duniani lililotolewa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu (Hayupo kwenye picha) leo katika ofisi ndogo za Wizara ya Afya jijini Dar es salaam
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu akijadiliana kwa ukaribu na Mganga Mkuu wa Serikali Prof Muhamad Bakari Kambi wakati akitoa tamko kuhusu Homa ya Ini Duniani katika Ofisi ndogo za Wizara ya Afya jijini Dar es salaam.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wakifuatilia kwa umakini tamko lilitolewa na Mh. Ummy Mwalimu (hayupo kwenye picha) katika kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Homa ya Ini Duniani mapema leo katika ofisi ndogo za Wizara ya Afya jijini Dar es salaam.

……………………………..

NA WAMJW –DAR ES SALAAM.

CHANJO ya homa ya Ini inatarajiwa kupatikana kwa wananchi wote bila kujali kigezo cha umri wala uwezo wa kifedha kwa wananchi wenye hatari au ugonjwa wa ini kwa bei nafuu mpaka kufikia mwaka 2020 kutoka mwaka wa fedha 2018/2019.

Hayo yamezungumzwa na Waziri wa afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia , Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es salaam kuhusu maadhimisho ya ugonjwa wa homa ya ini duniani.

“Katika kuadhimisha siku ya ugonjwa wa homa ya ini duniani tumedhamiria kuhakikisha chanjo ya ugonjwa huu inapatikana kwa watu wote nchini ambao wana hatari ya kupata maambukizi ya homa ya ini au tayari wamepata ugonjwa huo kwa bei nafuu kwa mswaka wa bajeti 2018/2019” alisema Waziri Ummy.

Aidha waziri Ummy amesema kuwa chanjo ya homa ya Ini kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano inapatikana hapa nchini kwenye vituo vya huduma ya afya vya Serikali na watu binafsi.

Kwa mujibu wa Waziri Ummy amesema kuwa ili kujilinda na maambukizi ya ugonjwa wa homa ya ini mpango wa damu salama unatakiwa kuhakikisha wanapima damu zote za wachangiaji kabla ya kuwawekea wagonjwa wanaohitaji huduma ya damu.

Waziri Ummy ameongeza kuwa ugonjwa wa homa ya ini unaua idadi kubwa ya watu duniani kwa taratibu ikiwa katika watu 100 watu 8 wana maambukizi ya ugonjwa huo na kutoonyesha dalili mapema.

Aidha Waziri Ummy amesema kuwa asilimia 50 ya wanaotumia madawa ya kulevya kwa kujidunga sindano wana maambukizi ya ugonjwa wa homa ya ini hivyo kuwataka watanzania kutojihususha na matumizi hayo na kuepuka ngono zembe.

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Mohamad Bakari Kambi amesema kuwa virusi vikubwa vya ugonjwa wa ini ni A,B na C ambapo vimelea A huletwa na mtu asiye na maambukizi kula chakula kisicho salama na kunnywa maji yasiyo salama.

Aidha Prof. Kambi amesema kuwa virusi B na C vya ugonjwa wa homa ya ini husababishwa pale mtu asiye na maambukizi kugusa majimaji au damu kutoka kwa mgonjwa mwenye ugonjwa wa homa ya ini.

Maadhimisho ya ugonjwa wa homa ya Ini huadhimishwa Julai 28 kila mwaka Duniani na mwaka huu imebeba kauli mbiu isemayo “TOKOMEZA HOMA YA INI” ambapo hapa nchini imeadhimishwa jijini Dar es salaam.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...