Pages

July 27, 2017

RWAKATARE CUP 2017 YASAKA VIJANA WENYE VIPAJI VYA SOKA KUCHEZEA TAIFA STARS KILOMBERO

Mbunge wa kuteuliwa CCM mkoa wa Morogoro, Mchungaji Getruda Rwakatare akipiga mpira na kufunga bao kwa njia ya mkwaju wa penalti kama ishara ya mashindano ya Rwakatare Cup 2017 yaliyozzinduliwa kijiji cha Mngeta uwanja wa Lukolongo wilayani Kilombero mkoa wa Morogoro, wa pili mwenye kofia nyekundu ni Mkuuu wa wilaya ya Kilombero, James Ihunyo.

Na Juma Mtanda, Morogoro.
Tanzania inaweza kuwa na hazina kubwa ya wachezaji na kuwa na mafanikio katika siku za baadaye katika mchezo wa soka endapo tu viongozi wa TFF watakuwa na utamaduni wa kuwafuatilia wachezaji wanaong’ara katika mashindano mbalimbali hasa ya vijijini kisha kuwateua na kuwapeleka katika vilabu vya ligi ngazi ya juu hapa nchini.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mashindano ya soka ya Rwakatare Cup 2017 kijiji cha Mngeta wilaya ya Kilombero mkoani hapa, mbunge wa viti maalum CCM mkoa wa Morogoro, Mchungaji Getruda Rwakatare alisema kuwa njia ya kuibua vipaji vya soka kwa vijana na kuwaendeleza hasa upande wa vijijini lipo mikononi mwa viongozi wa TFF.

Mchungaji Rwakatare alisema kuwa viongozi wa TFF ngazi ya wilaya wana fursa kubwa ya kuibua vijana kupitia mashindano ya soka yanayoanzishwa vijijini kwa kuwang’amua wachezaji hao wenye vipaji kisha kuwapeleka katika vilabu zitakazosaidia kuwanoa zaidi na vilabu vingine.

“Wilaya ya Kilombero ina vijana wengi wenye vipaji vya mchezo wa soka, kama golikipa Aishi Manula na wenzake lakini mimi naamini kuwa vijijini kuna vipaji vingi havijaibuliwa kupitia mashindano ya soka na TFF kama wakifanya kazi ya kuwatambua wachezaji katika ngazi hiyo, Tanzania kutakuwa na wanasoka wengi wataosaidia taifa.”alisema Rwakatare.

Mashindano hayo yanashirikisha jumla ya timu 80 za mpira wa miguu na kupangwa katika vituo vya viwanja saba vya Mkamba, Mang’ula, Namawala, Ifakara, Chita, Mlimba na Mng’eta ambapo mshindi wa kwanza ataondoka na zawadi ya sh2 mil huku wa pili akipata sh1mil.

Katika mchezo wa ufunguzi wa mashindano hayo kati ya timu ya Super Mahakama FC na Mchombe Rangers zote za Mngeta zilishindwa kutambiana baada ya kumalizika dakika 90 kwa suluhu ya 0-0 katika mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa Lukolongo Mngeta.

Kwa upande wa mkuu wa wilaya ya Kilombero, James Ihunyo alisema kuwa mashindano hayo ni fursa kwa vijana kuonyesha uwezo wao wa kucheza soka ili kukuza vipaji vyao vitavyofanya timu kubwa ziweze kuvutiwe nao.

Ihunyo alisema kuwa soka kwa sasa ni ajira tosha huku akiwataka vijana kuyatumia mashindano hayo kama njia ya safari ya mafanikio kwa kucheza soka na bidii lenye ustadi mkubwa na kuweka kipaumbele itayosaidia kucheza timu kubwa.

“Mchungaji Rwakatare amesema haya mashindano hana itikadi ya udini, ukabila, siasa na lengo lake ni kuibuka vipaji vya soka kwa vijana wetu katika wilaya hii ili tu viweze kuonekana na kuonwa na vilabu vikubwa na baadaye visaidie timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Star) lakini na kipato katika familia zao.”alisema Ihunyo.

Mashindano hayo yanaendeshwa kwa mfumo wa mtoano naa kila kituo itatoa timu mbili zitakazo kuungana na timu nyingine na kufikia timu 14 ambazo zitapatana timu nane zitazoingia kwenye michezo ya robo fainali kuelekea kwenye michezo ya nusu fainali na fainali

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...