Daraja la vioo china.
HEBU vuta
picha, unatembea kwenye daraja, tena la vioo, ukitazama chini unaona
bonde lenye urefu wa zaidi ya mita 300, sawa na viwanja vitatu vya mpira
vilivyounganishwa, ukitembea unahisi kama unataka kudondokea kwenye
korongo hilo au unahisi vioo vinaweza kupasuka na ukadondoka, unaweza
kupiga hata hatua moja?Ni wachache wenye uthubutu huo lakini wengi, hasa
wale wanaosumbuliwa na matatizo ya moyo au hofu ya kupindukia, huishia
kutambaa tu huku wakipiga kelele za kuomba msaada, hawana ujasiri wa
kusimama na kutembea.
Hii si
stori ya kutunga, ni kweli nchini China kuna daraja liitwalo Zhangjiajie
Grand Canyon ambalo limejengwa kwa vioo tupu, hakuna mbao wala bati,
yaani ukiachilia mbali vyuma vilivyolishikiza, sehemu iliyobakia ni vioo
mwanzo mpaka mwisho na kuweka rekodi ya kuwa daraja refu la vioo kuliko
yote duniani.Daraja hilo ambalo linatajwa kuwa miongoni mwa maajabu ya
ulimwengu, limejengwa na Kampuni ya Haim Dotan LTD kutoka nchini Israel
na limeanza kutumika rasmi mwaka huu, 2017, likitajwa kuvutia zaidi ya
watu 8,000 kila siku.
Daraja la vioo likibomolewa.
Daraja
hili linaunganisha vilele viwili vya Milima ya Avatar (Filamu ya Avatar
ilirekodiwa kwenye milima hii), likiwa na urefu wa mita 430 kutoka
ng’ambo ya kwanza mpaka ya pili, likitajwa kugharimu zaidi ya dola 3.4
milioni, sawa na shilingi bilioni 7.6 za Kitanzania.
Vioo
vilivyotumika, hasa sehemu ya kukanyagia, vimepangwa kwa matabaka matatu
ya vioo vigumu, visivy-oweza kuvunjika hata vikipigwa na nyundo ngumu,
vikiwa na uwezo wa kuhimili hata uzito wa gari lililojaza abiria bila
kupasuka.
Daraja la juu.
Tangu
kuzinduliwa kwake, limekuwa kivutio kikubwa kwa watalii, watu wanaofanya
yoga au hata wanaoenda kufunga harusi, huku idadi ya watu waoga,
wanaopatwa na mshtuko mkubwa, wengine presha zikipanda na kuwafanya
wakimbizwe hospitali baada ya kufika kwenye daraja hilo, ikizidi
kuongezeka.
Unaambiwa
kabla ya kutaka kupita kwenye daraja hilo, lazima upimwe presha na
uwezo wako wa kuhimili hofu, ukionekana woga umekuzidi, unazuiwa au
unapewa watu wa kukusaidia kutembea!
No comments:
Post a Comment