Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Selemani Jafo akifanya ukaguzi wa miundombinu inayojengwa katika Shule ya Sekondari Ihungo.
Naibu
Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Selemani Jafo akiwa katika ukaguzi wa
ujenzi wa madarasa na mabweni katika Shule ya Sekondari Ihungo.
Jengo la bweni linalojengwa katika shule ya Sekondari Ihungo.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Selemani Jafo akikagua majengo yanayojengwa katika Shule ya Sekondari Ihungo.
Baadhi
ya wanafunzi wa kidato cha tano katika shule ya Sekondari ya Omumwani
wakimsikiliza Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Selemani Jafo
………………………………..
Naibu
Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa(Tamisemi)
Selemani Jafo amefurahishwa na maendeleo ya ujenzi wa shule ya wavulana
ya kidato cha tano na sita ya Ihungo ambayo majengo yake yalibomoka
kutokana na tetemeko la ardhi lililotokea mwaka Jana.
Kutokana
na kubomoka kwa majengo hayo, Serikali iliamua kuijenga upya kwa
kutumia wakala wa majengo Tanzania (TBA). Akiwa katika ziara ya kukagua
miradi mbalimbali mkoani Kagera, Jafo alitembelea shuleni hapo kukagua
ujenzi wake.
Naibu
Waziri Jafo aliwapongeza wakandarasi kwa kazi nzuri wanayoendelea
kuifanya ambapo kazi hiyo inatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi
Agosti. Akizungumza na wananchi waliokuwepo katika eneo hilo, Jafo
alisema serikali imeamua kuijenga sekondari hiyo kisasa zaidi. Alisema
sekondari hiyo inatarajiwa kuwa sekondari ya mfano ndani ya Tanzania kwa
kuwa na majengo ya kisasa zaidi kuliko sekondari zote hapa nchini.
Hata
hivyo, Jafo alitoa angalizo kwa sekondari hiyo kubaki kuwa sekondari ya
wavulana kwani kutokana na uzuri wa miundombinu ya kisasa inayojengwa
isije baadae wakaja watu na kubadilisha mawazo kuwa Chuo kikuu jambo
ambalo sio sahihi.
Alibainisha
serikali imejipanga kuimarisha ubora wa elimu ya sekondari kwasasa.
Katika ziara hiyo, Jafo pia alitembelea shule ya Omumwani ambayo imeanza
kuchukua wanafunzi wa kidato cha tano ambao ni wasichana kwa mwaka huu.
Alitoa maagizo kwa manispaa ya Bukoba kumalizia ukarabati wa maabara
ndani ya wiki mbili zijazo ili kuwawezesha wanafunzi kufanya vyema zaidi
katika masomo yao kivitendo.
No comments:
Post a Comment