Mkuu
wa Wilaya ya Nzega, mkoani Tabora, Mh. Geofrey Ngupula akikata utepe
kuashiria uzinduzi rasmi wa gari jipya na la kisasa la kubebea wagonjwa
lililokabidhiwa katika kituo cha Afya Busondo, Tarafa ya Puge,
lililotolewa na Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Mh. Dk. Hamisi
Kigwangalla.
Mbunge
wa jimbo la Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla
amekabidhi gari maalum la kubebea wagonjwa (Ambulance) mpya na la kisasa
katika Kituo cha Afya Busondo kilichopo Tarafa ya Puge ambalo litakuwa
msaada mkubwa kwa wananchi wa Nzega Vijijini.
Tukio
hilo la kukabidhi gari hilo limefanywa na Mkuu wa Wilaya ya Nzega,
mkoani Tabora, Mh. Geofrey Ngupula mapema Julai 26,2017, aliyekuwa mgeni
rasmi ambaye alitoa agizo kali kwa Mganga Mkuu wa Kituo hicho
kuhakikisha gari hilo linatumika kwa shughuli zilizokusudiwa ikiwemo za
kubebea wagonjwa na akina mama wajawazito kuwawaisha sehemu muhimu za
kutolea huduma stahiki.
Mkuu
wa Wilaya huyo alimpongeza Mbunge wa Jimbo hilo Dk. Kigwangalla kwa
kuweza kuwasaidia wananchi wa Jimbo hilo kwa kuweza kuwasaidia gari hilo
la Wagonjwa kwani litasaidia kuokoa maisha ya wananchi hao ambao wapo
maeneo ya mbali na kituo cha Afya huku pia likitarajiwa kuwa msaada kwa
kuwapeleka wateja katika ngazi za juu za huduma hiyo ikiwemo Hospitali
za Wilaya, Mkoa, Kanda na Taifa.
Aidha,
alisema ni marufuku wagonjwa kuombwa kuchangia mafuta ya ambulance hiyo
au gharama yoyote ile, gari hili wagonjwa walitumie bure kwani
limetolewa bure na pia huduma zote zikiwemo za mafuta zinalipwa na
Halmashahuri hiyo.
Gari hilo la kubebea wagonjwa linavyoonekana.
“Gari
hilo lipatikane kituoni wakati wote pamoja na dereva. Tumeshahakikishiwa
hapa Halmshauri imesema ina mafuta ya kutosha litakuwa linajazwa lita
90, kila yatakapokuwa yametumika hivyo kusiwe na kisingizio kingine cha
kuweza kudai mafuta ama kuwatoza wananchi gharama na atakayefanya hivyo
Serikali hii si ya mchezo hatua kali zitafuata , tutakutumbua tu”
alieleza Mh. Ngupula.
Ameongeza
kuwa gari hilo ambalo ni la kisasa, litunzwe na kulindwa ili liweze
kutumika kwa miaka mingi ijayo na kuwa msaada kwa Tarafa hiyo na
wananchi wote watakaopata msaada wakiwemo wale wa maeneo mengine ya
jirani. Kwa upande wake, Dk. Kigwangalla amewaomba wananchi waendelee
kumuombea kwa kazi anayofanya ikiwemo jukumu la kulitumikia Taifa katika
nafasi yake ya Unaibu Uwaziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto.
Dk.
Kigwangalla ameishukuru serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Magufuli
kwa kuweza kuwa karibu na Wananchi ikiwemo kushughulikia suala la maji
kutoka Ziwa Victoria na kuja Mkoa wa Tabora ikiwemo kuanzia katika
Wilaya hiyo ya Nzega na kisha kwenda maeneeo mengine.
“Tunampongeza
Rais wetru Dk. Magufuli kwa kuwa karibu na wananchi wake. Tulikuwa nae
Mkoani kwetu hapa Tabora na amezindua miradi mbalimbali ikiwemo ya
barabara na ule wa maji safi yatakayotoka Ziwa Vitoria. Shida ya maji
kwa wananchi wa Nzega inaenda kuwa historia kwani Maji hayo yatakuja
hapa na kisha kwenda maeneo mengine.
Rais
wetu anatupenda na tuendelee kumuunga mkono hasa juhudi zake za kulinda
rasilimali za nchi yetu na pia katika kushughulikia mafisadi na wahujumu
uchumi wa Taifa letu Mimi Mbunge wenu pia muendelee kuniombea na kila
siku mawazo yangu na akili yangu ipo pamoja nanyi ndio maana nimeweza
kuwaletea gari hili la wagonjwa, na pia kufanikisha kuandaa kambi maalum
ya matibabu bure ya wiki moja kwa wananchi wote wa Nzega bure
inayoendeshwa na Madaktari bingwa wakiwemo wale wa kutoka China na
waliopo hapa nchini” alieleza Dk. Kigwangalla.
Tukio
hilo la ukabidhi wa gari hilo pia lilishuhudiwa na viongozi mbalimbali
wakiwemo Madiwani wa Jimbo hilo na wale wa jimbo jirani ikiwemo Bukuene,
Viongozi wa ulinzi na Usalama pamoja na Mganga Mkuu wa Wilaya ya
Nzega.
Mkuu
wa Wilaya ya Nzega, mkoani Tabora, Mh. Geofrey Ngupula akizungumza mara
baada ya kuzindua rasmi gari jipya na la kisasa la kubebea wagonjwa
lililokabidhiwa katika kituo cha Afya Busondo, Tarafa ya Puge,
lililotolewa na Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Mh. Dk. Hamisi
Kigwangalla.
Mkuu
wa Wilaya ya Nzega, mkoani Tabora, Mh. Geofrey Ngupula akiongozana na
Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo
ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla mara baada
ya kuzindua rasmi gari jipya na la kisasa la kubebea wagonjwa
lililokabidhiwa katika kituo cha Afya Busondo, Tarafa ya Puge,
lililotolewa na Mbunge wa Jimbo hilo.
Mkuu
wa Wilaya ya Nzega, mkoani Tabora, Mh. Geofrey Ngupula akizungumza mara
baada ya kuzindua rasmi gari jipya na la kisasa la kubebea wagonjwa
lililokabidhiwa katika kituo cha Afya Busondo, Tarafa ya Puge,
lililotolewa na Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Mh. Dk. Hamisi
Kigwangalla.
No comments:
Post a Comment