Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua gwaride katika hafla fupi ya kuwavalisha Vyeo Maafisa Magereza kwenye uwanja wa Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji, Ukonga jijini Dar es salaam Juni 12, 2017. Mheshimiwa mahaliwa alimwakisha Rais John Pombe Mgufuli katika hafla hiyo.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimvalisha Jeremiah Nkondo kuwa Naibu Kamishina wa Magereza katika hafla fupi iliyofanyika kwenye uwanja wa Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji, Ukonga jijini Dar es salaam Juni 12, 2017. Mheshimiwa majaliwa alimwakilisha Rais John Pombe Magufuli katika hafla hiyo.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimvalisha cheo Tusekile Mwaisabila kuwa Naibu Kamishina wa Magereza katika hafla fupi iliyofanyika kwenye uwanja wa Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji, Ukonga jijini Dar es salaam Juni 12, 2017. Mheshimiwa majaliwa alimwakilisha Rais John Pombe Magufuli katika hafla hiyo . (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimvalisha cheo, Afwililwe Mwakijungu kuwa Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Magereza katika hafla fupi iliyofanyika kwenye uwanja wa Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji, Ukonga jijini Dar es salaam Juni 12, 2017. Mheshimiwa majaliwa alimwakilisha Rais John Pombe Magufuli katika hafla hiyo . (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)
Manaibu Kamishina wa Magereza wakisoma Tamko la Ahadi ya Uadilifu kwa Viongozi wa Umma baada ya kuvalishwa vyeo na Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa aktika hafla fupi iliyofanyika kwenye uwanja wa Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji, Ukonga jijini Dar es salaam Juni 12, 2017. Mheshimiwa majaliwa alimwakilisha Rais John Pombe Magufuli katika hafla hiyo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika hafla fupi ya kuvalisha vyeo Maafisa magereza iliyofanyika kwenye uwanja wa Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji, Ukonga jijini Dar es salaam Juni 12, 2017. Mheshimiwa majaliwa alimwakilisha Rais John Pombe Magufuli katika hafla hiyo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na Maofisa magereza aliowavalisha Vyeo kwa Niaba ya Rais John Pombe Magufuli kwenye uwanja wa Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji, Ukonga jijini Dar es salaam Juni, 12, 2017. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amewataka maaafisa na makamanda wa Jeshi la
Magereza nchini waendelee kusimamia haki na usawa wanapotimiza wajibu
wao.
Ametoa
wito huo leo jioni (Jumatatu, Juni 12, 2017) wakati akizungumza na
maafisa na makamanda wa jeshi hilo katika hafla ya kuwavisha vyeo
maafisa 29 iliyofanyika kwenye viwanja vya Chuo cha Taaluma ya
Urekebishaji Tanzania (TCTA), Ukonga, jijini Dar es Salaam.
Waziri
Mkuu ambaye amefanya kazi hiyo kwa niaba ya Mheshimiwa Rais Dkt. John
Pombe Magufuli, amewavisha vyeo maafisa watano kuwa Naibu Kamishna wa
Magereza (DCP) na maafisa 24 kuwa Kamishna Waandamizi Wasaidizi wa
Magereza (SACP). Maaafisa hao walipandishwa vyeo Mei 25, mwaka huu.
“Ninyi
ni viongozi wakuu katika mikoa mnayotoka. Huko kuna makamanda walio
chini yenu na jamii inayowazunguka. Endeleeni kuwahudumiana na
kulitumikia Taifa hili kwa weledi mkubwa. Endeleeni kusimamia usawa na
haki katika kazi zenu za kila siku,” amesema.
Waziri
Mkuu amesema hana shaka na utendaji kazi wa jeshi la Magereza kwani
watumishi wake ni waadilifu. “Jeshi hili linayo nidhamu ya hali ya juu,
mbali ya jukumu lenu la ulinzi, mnafanya kazi nidhamu, weledi na
uadilifu mkubwa,” amesema.
Amesema
Serikali inatambua changamoto zinazowakabili katika utendaji wao wa
kila siku na kwamba inajitahidi kuzishughulikia hasa baada ya
kukamilisha zoezi la kuondoa watumishi hewa.
Mapema,
akimkaribisha Waziri Mkuu kuhutubia maafisa hao, Naibu Waziri wa Mambo
ya Ndani, Bw. Yusuph Masauni amewataka maafisa waliovishwa vyeo
wazingatie maadili ya kazi zao na uzalendo kama ambavyo wameapa kwenye
kiapo cha maadili.
Maafisa
watano waliovalishwa vyeo kuwa Naibu Kamishna wa Magereza ni SACP Uwesu
Ngarama; SACP Gideon Mkana (Mkuu wa Chuo cha TCTA); SACP Jeremiah
Nkondo (RPO-Kagera); SACP Tusekile Mwaisabila (RPO-Lindi) na SACP
Augustine Mboje (RPO-DSM).
Maafisa
24 waliovalishwa vyeo kuwa Makamishna Waandamizi Wasaidizi wa Magereza
(SACP) ni ACP Mbaraka Semwanza; ACP George Mwambashi; ACP Charles
Novati; ACP Faustine M. Kasike; ACP Joel Bukuku; ACP Deogratius Lwanga;
ACP Boyd P. Mwambingu (RPO Pwani); ACP Athumani Kitiku (RPO Mwanza) na
ACP Hassan Mkwiche (RPO Kilimanjaro).
Wengine
ni ACP Luhende D. Makwaia; ACP Hamza R. Hamza; ACP Jeremiah Y. Katengu;
ACP Mzee R. Nyamka (Kaimu RPO Morogoro); ACP Afwilile Mwakijungu (Mkuu
wa gereza la Isupilo, Iringa); ACP Ali Kaherewa (Kaimu RPO Singida); ACP
Ismail Mlawa (RPO Mtwara); ACP Chacha B. Jackson; ACP Rajab N. Bakari;
ACP Kijida P. Mwankingi; ACP Julius C. Ntambala; ACP Mussa M. Kiswaka;
ACP Justin Kaziulaya na ACP Bertha J. Minde.
(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMATATU, JUNI 12, 2017.
No comments:
Post a Comment