Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt.
Aziz Mlima (wa kwanza kulia), akimkabidhi zawadi Afisa Mambo ya Nje,
Bi. Eva Ng'itu kutoka Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa. Bi. Ng'itu
amekuwa Mfakazi Hodari wa wa Wizara ya Mambo ya Nje kwa Mwaka wa Fedha
2016/2017. Dkt. Mlima aliwapongeza na kuwasihi wafanyakazi waliofanya
vizuri kuwa zawadi walizokabidhiwa iwe chachu ya kuongeza juhudi na
ufanisi katika utumishi wao.
Mkurugenzi
wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy
akimpongeza Bi. Ng'itu kwa kuwa mfanyakazi Hodari wa Wizara ya Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Bw. Mohammed Kheri kutoka Idara ya Mambo ya Nje Zanzibar akipokea zawadi yake kwa kuwa mfanyakazi bora wa Idara hiyo.
Bw.Joseph
Mlingi akipokea zawadi kwa kuwa mfanyakazi bora kwa upande wa madereva
wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Bw. Emannuel Luangisa akipokea zawadi yake ya kuwa mfanyakazi bora wa Idara ya Asia na Australasia.
Kaimu
Mkurugenzi wa Idara ya Diaspora na Mratibu wa Mafunzo wa Wizara ya Mambo
ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Tagie Daisy Mwakawago
naye akipokea zawadi ya ufanyakazi bora wa Idara ya Diaspora
Bi Eva Kaluwa kutoka Idara ya Sera na Mipango akipokea zawadi yake kutoka kwa Dkt. Mlima.
Bi. Kisa Mwaseba akipokea zawadi ya Mfanyakazi bora wa Idara ya Mashariki ya Kati.
Bi. Upendo Mwasha akipokea zawadi ya mfanyakazi bora wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda.
Bi. Nelusigwe kutoka Kitengo cha Ununuzi na Ugavi akipokea zawadi baada ya kuibuka mfanyajkazi bora wa Kitengo hicho.
Bw. Erick Ngilangwa kutoka Idara ya Afrika akipokea zawadi ya mfanyakazi bora wa Idara hiyo
Afisa
Habari wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi.
Rose Mbilinyi akipokea zawadi yake kutoka kwa Dkt. Mlima.
Katibu
Mkuu Dkt. Mlima akizungumza katika kikao cha baraza la wafanyakazi la
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Mkurugenzi Msaidizi kutoka Idara ya Mambo ya Nje, Zanzibar akichangia jambo katika kikao cha Baraza la Wafanyakazi.
Sehemu
ya wajumbe wa Baraza la wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakimsikiliza kwa makini Katibu mkuu
alipo kuwa akizungumza nao
Picha
ya pamoja ya Katibu Mkuu, Dkt. Mlima na wafanyakazi bora kutoka kwenye
Idara na Vitengo vya Wizara. Mwanamke pekee aliyeketi ni Bi. Eva Ng'itu
ambaye ameibuka mfanyakazi hodari wa Wizara nzima kwa Mwaka wa Fedha
2016/2017.
No comments:
Post a Comment