Kamati
ya Viongozi wa dini ya Masuala ya haki za Binadamu, Kiuchumi na
uadilifu katika Uumbaji wakizindua Mapitio ya Ripoti ya Swali la Dola
Bilioni moja ,Tanzania inaendelea kupoteza fedha kiasi gani? wakizindua
Ripoti hiyo, wakiwa na Wabunge.
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii - Dodoma
Tafiti
mpya iliyozinduliwa hivi karibuni inasema serikali inapoteza fedha
zaidi ya Sh trillion 4 kwa mwaka kutokana na misamaha na ukwepaji wa
kodi. Pia repoti imesema serikali inapoteza Dola za kimarekani 1.3
biloni (2.9 trilion) kutokana na rushwa na ufisadi katika bajeti ya
Taifa.
Hayo
yamesemwa na Profesa Honest Ngowi alipokuwa akiwasilisha matokeo ya
utafiti na mapitio ya ripoti ya swali la dola bilioni moja na kuja na
swali Tanzania inapoteza kiasi gani cha fedha?.
Profesa
Ngowi katika mapitio hayo amepata kutaja kuwa, Mfumo wa ulipaji kodi ,
Mlipa kodi, Misamaha ya kodi, Utoroshwaji wa fedha nje ya nchi na
upotevu wa mapato, Ukwepaji kodi, Madhara na Gharama za upotevu na
kutokusanywa kodi ipasavyo ni moja ya mambo yanayochangia kupotea kwa
fedha hii.
“Tatizo
la utoroshwaji wa fedha nje ya nchi na upotevu wa mapato limeangaliwa
upya katika utafiti huu na kubaini kuwa Tanzania bado inapoteza mapato
kwa njia ya utoroshaji fedha zilizopatikana kwa njia zisizo halali,
Zinaondoshwa nchini visivyo na kutumiwa isivyo halali” amesema Prof
Ngowi.
Ametaja
kuwa fedha hizo zinaweza kuwa ni fedha zitokanazo na biashara haramu
kama biashara ya Dawa za kulevya, biashara haramu mipakani, uharamia,
usafirishaji binadamu, mapato kutokana na ukwepaji kodi na mapato
yatokanayo na rushwa.
Amesema kuwa sambamba na utoroshwaji wa fedha, tatizo la kutoa taharifa za uongo wa bei.
Kamati
ya Viongozi wa dini ya Masuala ya haki za Binadamu ,Kiuchumi na
uadilifu katika Uumbaji wakizindua Mapitio ya Ripoti ya Swali la Dola
Bilioni moja ,Tanzania inaendelea kupoteza fedha kiasi gani? wakiwa na
wabunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakionyesha Vitabu juu mara
baada ya uzinduzi.
Profesa
Honest Ngowi akifafanua juu ya Mapitio ya Ripoti ya Swali la Dola
Bilioni moja ,Tanzania inaendelea kupoteza fedha kiasi gani?
Askofu
Stephene Munga akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mapitio ya Ripoti ya
Swali la Dola Bilioni moja ,Tanzania inaendelea kupoteza fedha kiasi
gani?
Mbunge wa Msalala, Ezekiel Maige akizungumza wakati wa kuchangia mapitio ya ripoti hiyo
Sehemu ya washiriki wa mkutano huo.
No comments:
Post a Comment