Her
Initiative iliyojulikana hapo awali kama Teen Girls Supportive
Initiative (TGSI) iliandaa mkutano ujulikanao kama Panda,
uliowakutanisha pamoja wanafunzi wakike kutoka vyuo mbalimbali nchini
pamoja na wadau mbalimbali wanaojishughulisha na biashara, ujasiriamali
na wanahabari, lengo likiwa ni kukuza upeo na uelewa wa wasichana katika
maswala mbalimbali ya maendeleo.
Her
Initiative ni asasi ya wasichana ambapo wao wenyewe ndio mhimili wa
maongezi, ambayo inawapa wasichana nafasi ya kuwakilisha na kusimamia
maswala yao wenyewe ya kiuchumi, kielimu, kiutamaduni na kiafya. Zaidi
inamjengea uwezo msichana kwa kutafuta suluhu ya changamoto zake
mwenyewe bila kutegemea watu wengine. Vyote hivi hufanyika kupitia
kampeni, matamasha, semina na kuwapa msaada wa mahitaji ya kielimu,
kiuchumi na kiafya kwa kushirikiana na wadhamini mbalimbali.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiBkqohH_Y2I1tG7zAsRfL_3c1JUtyPpEAhWip0L-8ZU0omH3Gv4srf9uUJG37GaVNP2mqmTLek1yZPwqnRYnxRz3QMVf39Fv1gmu2UxKgZjdLKalsUzEhF9CfxQM_KL0ugqvmlQLKbZ25M/s640/panda+3.jpg)
Faraja
Nyalandu mmiliki wa Shule Direct ambaye ndie alikuwa Mgeni Rasmi
katika Mkutano huo akiwsihi wanafunzi kuwa na nidhamu ya pesa kwa
kutumia kidogo na kuwekeza zaidi.
Akizungumza katika Mkutano huo, Mwenyekiti wa Her Initiative,
Maureen Richard aliwataka Wasichana kujishughulisha na vitu mbali mbali, kwani Uwezo wanao na
Panda ni mwanzo wa maendeleo mengi zaidi kwa wasichana. "Nina
wasihi wasichana wajitambue, wajithamini na wachakarike pia watumie
fursa walizonazo kujikwamua kiuchumi" alisema Maureen Richard.
Mkutano
huo ulifanyika mapema wiki iliyopita katika ukumbi wa Nkurumah, Chuo
Kikuu cha Dar-es-salaam. Watu mbalimbali mashuhuri walikuwepo kuwapatia
motisha na ushauri wasichana hao, wakiongozwa na Faraja Nyalandu mmiliki
wa Shule direct (mgeni rasmi), Elizabeth Muro "mshauri mkuu wa
Commercial Bank of Africa ", Jokate Mwegelo mmiliki wa "Kidoti", Martin
Kadinda "mshindi wa ubunifu wa mavazi" , Philip Makoye "mmiliki wa Mak
Juice".
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiXVvX6j0eTr_j-flER7HnwTw6y7aw-i6udmK_MP9-rHNTdX6HCpEi_zfDrs0h_ioM0Q31NNxG7aGV6-FwxgGXzCr5gdN4GePoSY9B5Ck5TpBh5MZ4ml36hHq8TmKZ1mn3Q4zSMGUfqvL_W/s640/panda+11.jpg)
Mwanzilishi
wa Her Initiative ambaye kwa sasa ni Kiongozi wa Nguvu ya Binti na
Mtangazaji wa vipindi vya Fema, Lydia Charles akitoa neno kwa wasichana
wenzake.
Mkutano huo wa PANDA 2017 ulidhaminiwa na TECNO MOBILE , EFM , RACHEL'S CHOICE Pamoja na MICHUZI MEDIA GROUP.
Philbert
makoye (Makjuice) akiwasihi wasichana kutumia nafasi wanazozipata
vizuri na kutokukata tamaa ya malengo walioyapanga .
Jokate
Mwegelo alimpongeza Lydia kwa ujasiri na Moyo wa kufanya kazi ingawa
alipitia changamoto nyingi. Pia alitoa wito kwa wasichana kuiga mfano
kutoka kwa muanzilishi wa taasisi hiyo, Lydia Charles ambaye kwa sasa ni
mtangazaji wa vipindi vya Fema.
Mwenyekiti
mpya wa Her Initiative Moureen Richard (Kati) akiwa pamoja na
mzungumzaji Elizabeth Muro (kulia) na Lydia Charles (kushoto).
Kwenye
tamasha hilo la Mwaka 2017 pia walitambua wasichana wanaojituma katika
Nyanja tofauti tofauti ambao ni Nandy, Diana Mbogo, Tuli Mwampanga,
Jihan Dimack, Genevieve Mpangala, Amina Sanga , Shamira Mshangama
mwanafunzi kutoka chuo cha Dar es salaam mwandishi wa vitabu.
Martin Kadinda akiongea na wasichana juu ya kuwa tofauti katika maisha na kutumia kipaji ili kujikwamua kiuchumi .
Baadhi ya wasichana walioshiriki katika tamasha hilo.
Timu ya maaadalizi ya tamasha hili kutoka shirika la Her Initiative.
wasichana wa walioshiriki katika tamasha hilo wakifurahia.
No comments:
Post a Comment