Na Abdullatif Yunus - Bukoba.
Wakati Shirika
la Afya Duniani WHO na Shirika la chakula na Kilimo FAO likipendekeza
kiwango cha unywaji maziwa kwa Binadamu ni lita 200 kwa mwaka,
imebainika kuwa nchi ya Tanzania unywaji wa maziwa kwa mwaka ni
asilimia 47, hii na sawa na chini ya robo ya kiwango kinachopendekezwa.
Kufuatia
Ripoti hiyo iliyotolewa na Mh Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo Na Uvuvi
Mhe. William ole Nashe (pichani) Serikali imejipanga kuboresha zao la
maziwa kuanzia kwa Mfugaji mpaka kwa mtumiaji, ili kuhakikisha zao hili
linakuwa na Tija,
Akihutubia
katika Uzinduzi wa wiki ya Unywaji Maziwa Kitaifa inayoadhimishwa
Mkoani Kagera katika Manispaa ya Bukoba, Mh. Naibu Waziri Ole Nasha
amesema,
“Takwimu
Ya zao la maziwa nchini zinaonyesha kuwa,Nchi ya Tanzania
huzalisha maziwa lita bilioni 2.1 kwa mwaka, ambapo 70% huzalishwa na
Ng,ombe wa asili ambao uzalishaji wake ni kati ya lita mpaka lita tano
kwa siku, hata hivyo tunao ng,ombe wachache wa maziwa wanakadiriwa
kufikia Ng,ombe laki saba na elfu themanini na mbili ambao wanakadiriwa
huzalisha maziwa lita nane hadi ishirini kwa siku.”
Aidha
Mh. Naibu waziri William Ole Nasha, ameongeza kuwa “ maziwa yanayoingia
viwandani kusindikwa kati ya maziwa yanayozalishwa ni 3% tu!, hapa
nchini kuna viwanda 75 vyenye uwezo wa kusindika lita laki sita na
Arobaini elfu kwa siku, lakini kwa sasa viwanda vinavyosindika Maziwa
ni 63 tu vyenye uwezo wa kusindika lita laki moja na elfu sitini na
saba na sabini za Maziwa kwa siku.
Hii ni sawa na wastani wa unywaji wa maziwa, ni takribani lita 47 kwa mwaka”
No comments:
Post a Comment