Na. Eliphace Marwa - Maelezo.
RAIS
Mstaafu Ali Hassan Mwinyi ameongoza mamia ya wakazi wa jiji la Dar es
Salaam katika maziko ya mwanasiasa mkongwe na aliyekuwa Mstahiki Meya wa
Jiji la Dar es Salaam, Kitwana Kondo.
Mbali
na Mwinyi wengine waliohudhuria maziko hayo yaliyofanyika katika
makaburi ya Tambaza ni Makamu wa Rais Mstaafu, Mohammed Gharib Bilal,
Mawaziri Wakuu Wastaafu, Salim Ahmed Salim na Edward Lowassa, Katibu
Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana, Mwenyekiti wa
Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba pamoja na wengine.
Akizungumza
nyumbani kwa marehemu, Mzee Mwinyi alisema, marehemu Kondo alikuwa ni
mtu ambaye alijitoa katika kulitumikia taifa kwa moyo wake, hivyo
mchango wake ni mkubwa katika kulitumikia taifa na hasa wakazi wa jiji
la Dar Es Salaam.
"Alikuwa
ni rafiki yangu ambaye tumefahamiana kwa muda mrefu sana, tumepoteza
mtu muhimu sana, lakini kazi ya Mungu haina makosa, tumuombee kwa
Mwenyezi Mungu amlaze mahali pema peponi," alisema Mzee Mwinyi
Kwa
upande wake, Kinana alisema, taifa na hasa wakazi wa Dar es Salaan
wamepata pigo kubwa kwa kumpoteza mzee huyo ambaye bado busara zake
zilikuwa zikihitajika.
"Alikuwa
ni kiongozi wa jamii,alikuwa ni mwalimu wa watu wengi katika manbi
mbalimbali, ni msiba mkubwa lakini nj kazi ya Mungu, tuendelee kumuombea
apumzike kwa amani," alisema Kinana.
Naye,
Waziri Mkuu wa Zamani, Edward Lowassa alisema, kutokana na kazi kubwa
iliyofanywa na Mzee Kondo ni vema uongoziu wa jiji kuangalia namna
ambavyo barabara moja ya jiji hilo likapewa jina la KK ikiwa ni
kuheshimu na kutambua mchango wake.
"Namuomba
Mstahiki Meya, barabara moja uiite KK, itakuwa ni heshima kumuenzi Mzee
Kitwana Kondo kwa kazi kubwa aliyofanya wakati wa uhai wake," alisema
Lowassa.
Naye
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) , Profesa Ibrahim Lipumba
alisema, mchango wa Mzee katika taifa ni mkubwa lakini kwa bahati mbaya
ni kama jmeshindwa kutambuliwa.
"Ni
mtu ambaye bahati mbaya sana historia ya nchi yetu haitambui mchango
wake katika kuleta uhuru wa nchii na kudumisha uhuru wa nchii," alisema
Profesa Lipumba.
Akieleza
chanzo cha kifo cha baba yake, mtoto wa kwanza wa marehemu Mzee Kondo,
Stara Kondo alisema, Baba yake alilazwa katika hospitali ya Hindu Mandal
Mei 18 kutokana na kuugua muda mrefu lakini alifariki juzi.
“Alikuwa
anaumwa muda mrefu lakini hadi anafariki madaktari walisema alipata
stroke (Kiharusi) na shinikizo la damu, tutamkumbuka kwa mambo mengi kwa
sababu ni baba lakini alikuwa ni kichwa cha familia,” alisema Stara
Baadhi
ya Ndugu Jamaa na Marafiki wakiwa wamebeba Jeneza lenye mwili wa
aliyewahi kuwa Mbunge wa jimbo la Kigamboni na Meya wa Jiji la Dar es
Salaam, Mzee Kitwana Kondo wakielekea kwenye maziko yake,leo Alhamisi
baada ya swala alasiri katika makaburi ya Tambaza jijini Dar es Salaam.
Mazishi ya aliyekuwa Meya wa Dar es salaam Mzee Kitwana Kondo jioni hii makaburi ya Tambaza jijini Dar
Mazishi ya aliyekuwa Meya wa Dar es salaam Mzee Kitwana Kondo jioni hii makaburi ya Tambaza jijini Dar
Mwili
wa Marehemu Mzee Kitwana Kondo ukiingizwa msikitini kwa ajili ya
kuswaliwa tayari kwa mazishi jioni ya leo ,katika Makaburi ya
tambaza,jijini Dar.
Ndugu
jamaa na marafiki wakiwa Makaburi wakisubiri kuupokea mwili wa Marehemu
kwa ajili ya Maziko katika Makaburi ya Tambaza,jijini Dar
No comments:
Post a Comment