Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na
Mwakilishi wa Benki ya Dunia Bwana Moderes Abdula aliyeuongoza Ujumbe wa
Washirika wa Maendeleo ulikuwepo Zanzibar kwa siku Nne kukagua miradi
ya Tasaf Awamu ya Tatu. Kati kati yao ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa
Maendeleo ya Jamii Tanzania Bwana Ladislas Mwamanga.
Balozi
Seif akizungumza na Ujumbe wa Benki ya Dunia ulioambatana na washirika
wa Maendeleo hapo Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar uliofika kukagua
miradi ya Tasaf.
Balozi
Seif kati kati waliokaa vitini akiwa katika picha ya pamoja na Ujumbe
wa Viongozi wa Benki ya Dunia na washirika wake wa maendeleo mara baada
ya kumaliza mazungumzo yao. Kushoto ya Balozi Seif ni Naibu Waziri
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Mihayo Juma Nhunga,
Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Nd. Joseph Abdulla Meza na Bibi Azzah Ammin
kutoka Shirika la Idadi ya Watu Duniani (UNFPA). Kushoto ya Balozi Seif
ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Jamii Tanzania (TASAF) Nd. Ladislas
Mwamanga, Mwakilishi wa Benki ya Dunia Bwana Moderes Abdula na Naibu
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Nd. Ahmad Kassim
Haji.
Balozi
Seif akiagana na Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Jamii Tanzania (TASAF)
Nd. Ladislas Mwamanga wakishuhudiwa na Mwakilishi wa Benki ya Dunia
Bwana Moderes Abdula.
Picha na – OMPR – ZNZ.
Benki
ya Dunia kupitia washirika wake wa Maendeleo imeamini ya kuridhika na
hatua kubwa iliyochukuliwa na Jamii ya Wananchi wa Visiwa vya Zanzibar
katika kusimamia miradi yao kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii
Tanzania{TASAF} Awamu ya Tatu katika kujiondolea Umaskini.
Viongozi
wa Ujumbe wa Washirika hao wa Maendeleo ulitoa kauli hiyo wakati ukitoa
tathmini ndogo kwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif
Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar baada ya kumaliza ziara yake ya
kukagua miradi ya Jamii inayotekelezwa kupitia Tasaf Tatu katika maeneo
mbali mbali ya Mjini na Vijijini Unguja na Pemba.
Kiongozi
wa Ujumbe huo kutoka Benki ya Dunia Bwana Moderes Abdulah alimueleza
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba ziara ya Ujumbe wake
imeshuhudia maendeleo makubwa yaliyopatikana katika Jamii kutokana na
kundi kubwa la Wananchi lilivyoamua kutekeleza kwa ufanisi mkubwa miradi
yao waliyoianzisha.
Bwana
Moderes alisema Zanzibar imeonyesha mfano bora katika uendelezaji wa
miradi ya Maendeleo kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii Tanzania {TASAF}
awamu ya Tatu kiasi kwamba Uongozi wa Benki ya Dunia kupitia Washirika
wake imefurahia hatua hiyo ya mafanikio.
Alifahamisha
kwamba Benki ya Dunia kupitia washirika wake imeamua kuunga mkono
miradi ya Maendeleo kwa Wananchi Maskini katyika Nchi zinazoendelea
ikilenga kuona ufanisi wa kudumu unapatikana katika kustawisha maisha
yao ya kila siku.
Wakitoa
ufafanuzi zaidi wa ziara hiyo ya kukagua Miradi ya Tasaf Visiwani
Zanzibar Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii Tanzania
Bwana Ladislas Mwamanga na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa ya
Kuhudumia Watoto { UNICEF} Bwana Paul Quarles walisema upo ushahidi wa
fedha zainazotolewa na Tasaf kutumika katika utaratibu Maalum uliowekwa.
Walisema
ujenzi wa nyumba za kudumu, upatikanaji wa sare za skuli, uanzishwaji
wa Vitalu vya miti ya kudumu, ujenzi wa majengo ya Skuli na Madrasa kwa
kaya Maskini ni mfanbo wa matumizi hayo sahihi ya fedha hizo.
Wameipongeza
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Watendaji wa Ofisi ya Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibarpamoja na Tawala za Mikoa na Serikali za
Mitaa kwa usimamizi wake mzuri kwenye miradi ya Mfuko huo wa Tasaf.
Akitoa
shukrani zake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi
alisema Benki ya Dunia kupitia Wadhirika wake wa Maendeleo haikupoteza
Fedha iliyotoa katika kuanzishwa kwa Mradi huo.
Balozi
Seif alisema Mfuko wa Tasaf tokea kuanzishwa kwake katika awamu zote
mbili zilizopita imeibua miradi mingi ya Jamii katika maeneo mbali mbali
Unguja na Pemba na kuweza kusaidia ajira na kupunguza Umaskini.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar kupitia Ujumbe huo ameiomba Benki ya Dunia
kuendelea kuiunga mkono Zanzibar na Tanzania kwa ujumla katika harakati
za kupambana na ukali wa maisha na kustawisha Jamii.
Ujumbe
huo wa Viongozi wa Benki ya Dunia ulioambatana na Washirika wake wa
Maendeleo yakiwemo Mashirika ya Umoja wa Mataifa Kuhudumia Watoto {
UNICEF} na lile la Idadi ya Watu {UNFPA}na Viongozi wa Tasaf Bara na
Zanzibar walikuwepo Zanzibar kwa ziara ya siku Nne kukagua Miradi ya
Tasaf.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
No comments:
Post a Comment