Pages

April 19, 2017

PPF yatoa elimu ya 'Wote scheme' viwanja vya Mashujaa, Dodoma

Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa akimpongeza mmoja wa wafanyabiashara wa kilimo cha pamba Riyaz Haider wakati wa akitembelea maonesho ya mifuko ya uwezeshaji wananchi Kiuchumi, baada ya mfanyabiashara huyo kupata mkopo kutoka katika benki kuu ya Tanzania kupitia benki ya NMB.

Mfuko wa Pensheni wa PPF unashiriki katika Maonesho ya Mifuko ya uwezeshaji Wananchi kiuchumi kwa ajili ya kutoa elimu juu ya Mafao yanayotewa na Mfuko huo.

PPF inatoa Mafao mbalimbali na katika Maonesho haya unatoa elimu juu ya mfumo wa ' Wote scheme' kwa sekta isiyo rasmi yaani wale wanaojiajiri kama vile mama lishe, dereva boda boda, wakulima, wafugaji, wajasiriamali, Wasanii, wote hawa wanathaminiwa na PPF ndio maana unato fursa za huduma za afya, mikopo ya maendeleo, mikopo ya Elimu na Mafao ya uzeeni.

Kupitia Maonesho haya PPF inasajili wanachama wapya hapo hapo viwanjani pamoja na kukabidhi vitambulisho vya uanachama wa Wote scheme.Hivyo ni fursa muhimu kwa wakazi wa Dodoma kufika katika viwanja vya Maahujaa kupata elimu hii muhimu na kujiunga na Mfuko huu ili kufaidika na Wote scheme.

Na kwa wale ambao hawapo Dodoma, wanaweza kutembelea Ofisi za PPF zilizopo karibu nao 
Mkurugenzi mtendaji wa asasi inayochochea uwekezaji sekta binafsi kwenye kilimo ( PASS ) Nicomedy Bohai akimuelezea mafanikio ya asasi hiyo Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa wakati wa maonesho ya mifuko ya uwezeshaji Wananchi Kiuchumi yanayofanyika katika viwanja vya mashujaa mkoani Dodoma. 
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa akitoa cheti kwa Mfuko wa Pensheni wa PPF kwa udhamini wa Maonesho ya Mifuko ya uwezeshaji Wananchi kiuchumi kwa Meneja wa PPF Kanda ya Mashariki na Kati Michael Christian ambaye alimwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa PPF William Erio, kushoto ni Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu, Sera ,Bunge, Vijana, Ajira na watu wenye ulemavu Mhe.Jenista Mhagama. 
Mzee Seleman Saleh akiwasikiliza Linda Mshana meneja wa mikopo kushoto na Mary Kapeja mkuu wa kitengo cha masoko na biashara wa UTT Microfince PLC kulia katika maonesho ya mifuko ya uwezeshaji Wananchi kiuchumi. 
Enock Humba, Afisa matekelezo wa bima ya afya na Grace Michael afisa masoko wa elimu kwa umma wakitoa maelekezo wa watu waliotembelea banda la mfuko wa bima ya afya katika viwanja ya mashujaa mkoani Dodoma. 
Meneja wa PPF wa Kanda ya Mashariki na Kati Michael Christian akimuelezea kazi za PPF ikiwemo mafao yanayotolewa na Mfuko huo kama vile ' Wote scheme' mmoja wa watu waliotembelea Maonesho ya Mifuko ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi. 
Afisa Mfawidhi wa PPF Astro Liganga akimfafanulia Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matilo fursa zilizomo ndani ya mfumo wa ' Wote scheme' wakati alipotembelea banda la PPF katika Maonesho ya Mifuko ya uwezeshaji Wananchi kiuchumi. 
Moja ya watu waliojitokeza katika maonesho ya mifuko ya uwezekezaji na uchumi toka jamii ya wafugaji akiwa katika banda la PPF ambalo wameanzisha mfumo unaotoa fursa kwa watu wote (hata wasioajiriwa) kuweza kuchangia kima cha chini Tsh 20,000 kwa mwezi ambao utamwezesha mchangiaji kupata mafao ya uzeeni na matibabu. 
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Mkoa na wawakilishi wa Mifuko ya uwezeshaji Wananchi kiuchumi mkoani Dodoma baada ya kufungua rasmi Maonesho ya Mifuko ya uwezeshaji Wananchi kiuchumi.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...