Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
MAOMBI kwa ajili ya Taifa yamefanyika leo Jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na
Waziri
wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Afrika Mashariki
Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga pamoja na Mchungaji maarufu na mfanya
biashara na mwanzilishi wa Huduma ya Bill Winston, Bill Winston kutoka
nchini Marekani.
Mkutano
huo uliokuwa na lengo la kuliombea taifa uliweza kuhudhuriwa na
viongozi wa dini na serikali na Bishop kutoka nchini Zambia Bernard
Nwaka aliendesha maombi hayo.
Aliyewahi
kuwa Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia kanda ya Afrika Dr Oby Ezekwesili
aliweza pia kuchangia mada juu ya kuliombea taifa na namna wananchi
wanavyotakiwa kuishi ndani ya nchi yao.
Waziri
wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Afrika Mashariki
Mhe. Balozi Dkt. Augustino Mahiga akzungumza katika mkutano wa maombi
ujulikanao kama Tanzania National Prayer uliofanyika leo Jijini Dar es
salaam na kuendeshwa na Mchungaji maarufu na mfanya biashara na
mwanzilishi wa Huduma ya Bill Winston, Bill Winston.
Mchungaji
maarufu na mfanya biashara na mwanzilishi wa Huduma ya Bill Winston,
Bill Winston akizungumza na wananchi waliojitokeza kwenye mkutano wa
maombi kwa taifa ujulikanao kama Tanzania National Prayer uliofanyika
leo Jijini.
Aliyewahi
kuwa Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia kanda ya Afrika Dr Oby Ezekwesili
akizungumza na wananchi waliojitokeza kwenye mkutano wa maombi kwa
taifa ujulikanao kama Tanzania Natipnal Prayer uliofanyika leo Jijini.
Katibu
Mkuu wa Taasisi ya Kingdom Leadeship Network Tanzania (KLNT), Dk.
Charles Sokile akijadiliana jambo na Mratibu wa Kamati ya Maandalizi,
Carol Mbaga
Bishop
Bernard Nwaka kutoka Zambia akiongoza maombi kwa ajili ya taifa
yaliyofanyika leo Jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na Waziri wa Mambo
ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Afrika Mashariki Mhe.
Balozi Dkt. Augustino Mahiga,Mchungaji maarufu na mfanya biashara na
mwanzilishi wa Huduma ya Bill Winston, Bill Winston na Aliyewahi kuwa
makamu wa raisi wa benki ya Dunia kanda ya Afrika Dr Oby Ezekwesili.
Mkutano ukiwa unaendelea.Picha zote na Zainab Nyamka.











إرسال تعليق