Mshambuliaji
wa timu ya Taifa ya Tanzania, Mbwana Sammata akiruka juu kushangilia
goli lake la kuongoza dhidi ya wapinzani wao Timu ya Taifa ya Botswana,
katika mchezo wa kirafiki wa rekodi ya Fifa, uliochezwa jioni hii katika
uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Sammata ameweza kuipachikia timu
ya Taifa bao hilo katika dakika ya tatu ya mchezo huo na kuwaacha wa
Botswana wakiduwaa na kuanza kumkaba wanne wanne
Mchezo
uliendelea kwa timu zote kufanya mashambulizi ya kuviziana kiufundi
zaidi huku Stars ikisumbua sana ngome ya Botswana ambayo ililemewa
kabisa kwa kosa kosa nyingi kutoka kwa washambuliaji wa Tanzania .
ilipotimu
dakika ya 87 mshambuliaji wa kimataifa Mbwana Sammata akapicha bao la
pili mara baada ya wa Botswana kucheza faulo na Mshambuliaji huyo kupewa
apige faulo.
Mbwana Sammata au kama watu wanavyopenda kumwita Samagoal amewza kuwa nyota wa mchezo wa leo kwa kuisumbua ngome ya Botswana.
Kikosi cha Taifa Stars kilichoanza .
Kikosi cha Timu ya Taifa ya Botswana.
Mbwana Sammata akiwa ametuliza mpira gambani mbele ya beki wa Botswana ,Ofentse Nato
Mbwana Sammata akimtoka beki wa Botswana, Ofentse Nato
Mbwana Sammata akipiga mpira langoni mbeleya mabeki wa Botswana
Mbwana Sammata akishangilia bao
Mbwana Sammata akishanngilia
Wachezaji wa Taifa Stars wakishangilia bao
Shiza kichuya akitawala mpira mbele ya beki wa Botswana Tapiwa Gadibolae
Ibrahim ajib akiwania mpira wa juu
Kiungo
wa Timu ya Taifa Stars, Himid Mao akiruka juu sambmba na Beki wa
Botswana kuwania mpira wa juu, katika Mchezo wa kirafiki wa rekodi za
FIFA, uliochezwa katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es
salaam. Taifa Stars imeshinda bao 2-0.
Simon Msuva akitawala mpira
Shiza kichuya na mpira
Beki wa kati wa Botswana , Mosha Galemonthale akimchezea vibaya Mbwana Sammata
Mbwana Samata akiondoka na mpira.
No comments:
Post a Comment