Inaelezwa
kuwa tangu kuibuka kwa mauaji ya watu wenye ualbino mwaka 2007
takribani makaburi 22 nchini Tanzania yamefukuliwa na watu
wasiojulikana.
Chama
hicho kimeiomba serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na rais John
Pombe Magufuli kuweka mkazo katika mapambano dhidi ya ukatili wa watu
wenye ulemavu wa ngozi kama ilivyoonesha nguvu za kutosha katika vita ya
dawa za kulevya na pombe aina ya viroba.
Akizungumza
juzi kwenye kikao cha viongozi wa chama watu wenye ualbino kutoka mikoa
ya kanda ya Ziwa ambayo ni Mara,Mwanza na Shinyanga na wanachama
wengine Afisa mahusiano na habari TAS taifa Josephat Torner vitendo vya
kufua makaburi ya watu wenye ualbino yanatishia amani yao
Torner
alisema wanaiomba serikali kuelekeza nguvu katika masuala ya mauaji na
ufukuaji wa makaburi ili kuwafanya watu wenye ualbino waishi kwa amani
ndani ya nchi yao. “Katika suala la mauaji ya watu wenye ualbino ambao
wamekuwa wakiishi kwa hofu tunaomba serikali hata kuwataja kwa majina
wanunuzi hao kama ilivyotokea kwenye masuala ya vita ya dawa zakulevya
na uuzaji bombe aina ya viroba”,alisema Torner.
Aidha
alisema wanalaani kitendo cha kufukuliwa kwa kaburi la Nelson Msogole
(50) aliyekuwa akiishi mji wa Songwe baada ya kufariki tarehe 28/3/2011
na kaburi lake kuonekana kufukuliwa tarehe 20/3/2017na watu
wasiojulikana. “Matukio haya yanaendeshwa kwa usiri hivyo tunahoji
kwanini imeshindikana ikiwa kwenye dawa za kulevya wameweza kutaja na
kumepiga hatua?”,alihoji Torner.
Alisema
Tangu kuanze kuibuka mauaji ya watu wenye ualbino mwaka 2007 makaburi
22 nchini yamekwisha fukuliwa katika mikoa ya Mbeya ,Tabora,Mwanza,Mara
,Kagera,Rukwa, na Shinyanga.
Aliiomba
serikali ya awamu ya tano iweke mikakati ya uelewa kwenye jamii kwani
huenda hawana uelewa na watuhumiwa wakibainika waadhibiwe kwa mujibu wa
sheria. “Hiki
ni kipimo cha serikali ya awamu ya tano kwa sauti ya wanyonge kwani
kuna baadhi ya watu wanaishi kwenye nchi yao kwa hofu na unyonge na
kuondolewa utu wao hivyo tuna imani serikali itaweka nguvu kubwa kuliko
kipindi cha nyuma”,aliongeza Torner.
Naye
Mwenyekiti wa chama hicho kutoka mkoani Mwanza Alfredy Kapole alisema
mkoa wa Mwanza unaongoza kwa mauaji ya vifo vya albino zaidi ya 17
vimetokea tangu mwaka 2007 hivyo aliiomba serikali kuweka ulinzi mkubwa
kwa watu hao kwani wanakiuka katiba ya nchi kwani kila mtu anastahili
kuishi.
Mwenyekiti
wa chama hicho kutoka mkoani Mara Joseph Sinda alisema kitendo cha
kufukua kinawafanya waishi kwa hofu kubwa na kuitaka serikali ijaribu
kuchunguza chanzo chake ni nini na kuthibiti kama kwenye madawa ya
kulevya na pombe aina ya viroba walivyofanya ili waweze kuishi kwa
amani.
Mwanaharakati
kutoka mkoani wa Shinyanga Eunice Zabroni aliiomba serikali
wawaimarishie ulinzi na elimu itolewe kwani wanaishi kwa hofu kwa
kukosekana ulinzi imara kuanzia ngazi ya vitongoji,vijiji kata na wilaya
hadi mkoa.
Chama
cha watu wenye ualbino Tanzania (TAS) kimelaani vikali vitendo vya
ufukuaji wa makaburi ya watu wenye ualbino vinavyoendelea kujitokeza
nchini hali inayowafanya waishi kwa hofu kubwa katika nchi yao.
Katikati
ni Afisa mahusiano na habari wa chama cha watu wenye ualbino nchini
Tanzania (TAS )Josephat Torner akizungumza wakati wa kikao cha viongozi
na wanachama wa chama hicho ambapo walilaani vitendo vya ufukuaji wa
makaburi ya watu wenye ualbino.Kulia ni Mwenyekiti TAS mkoa wa Mara
Joseph Sinda,kushoto ni mwenyekiti TAS mkoa wa MwanzaAlfred Kapole
-Picha zote na Suzy Butondo-Malunde1 blog
Afisa
mahusiano na habari wa chama cha watu wenye ualbino nchini Tanzania (TAS
)Josephat Torner ambapo alisema chama hicho kinaiomba serikali ya awamu
ya tano inayoongozwa na rais John Magufuli kuongeza kasi katika
mapambano dhidi ya ukatili wa watu wenye ualbino
Baadhi
ya wanachama wa chama cha watu wenye ualbino nchini Tanzania wakiwa
katika kikao hicho. Picha na Suzy Butondo-Malunde1 blog
No comments:
Post a Comment