Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Dkt.
Juliana Pallangyo, (aliyesimama), akizungumza mbele ya wajumbe wa Kamati ya
Bunge ya Nishati na Madini, wakati wa ziara ya kamati hiyo kutembelea Mradi wa
Umeme wa Kinyerezi jijini Dar es Salaam, leo Machi 23, 2017
Meneja Msimamizi wa Mradi wa
Kinyerezi I, Yuka Mukaibo kutoka kampuni inayojenga mradi huo ya Sumitomo
kutoka Japan, akizungumza mbele ya wajumbe wa Kamati walipotembelea eneo la
Mradi jijini Dar es Salaam, Machi 23, 2017. Wakwanza kulia ni Naibu Katibu Mkuu
Wizara ya Nishati na Madini, anayeshughulikia Nishati, Dkt. Juliana Palangyo,
na wakwanza kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Dkt. Tito Mwinuka.
Naibu Mkurugenzi wa TANESCO, Mhandisi Khalid James, (aliyesimama), akitoa ufafanuzi wa utekelezaji wa Mradi huo mbele ya wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini waliotembelea kujionea maendeleo ya Mradi huo
NA K-VIS BLOG
SHIRIKA la Umeme Tanzania, (TANESCO), limeomba Kamati
ya Bunge ya Nishati na Madini ishauri Mamlaka iruhusu mizigo yake iliyokaa
bandarini kwa muda mrefu kutokana na swala la kodi iruhusiwe ili iweze
kukamilisha Mradi wa ujenzi wa Mradi wa Umeme wa Gesi wa Kinyerezi.
Hayo yamesemwa na uongozi wa TANESCO wakati wa
ziara ya Kamati hiyo iliyofanya kwenye Mradi huo jijini Dar es Salaam, Machi
23, 2017 ili kujionea maendeleo ya ujenzi wa Mradi huo muhimu.
“Mashine na vifaa vilivyozuiwa bandarini
viruhusiwe ili vikakamilishe mradi wa umeme wa Kinyerezi I&II na kodi
zinazopaswa kulipia mashine hizo zilipwe baadaye ili kuruhusu kazi ya kufunga
mitambo hiyo kwenye Mradi huo iweze kukamilika kwa wakati.” Alisema Meneja wa
Mradi kutoka TANESCO akiiambia kamati hiyo
Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Dkt. Tito Mwinuka, naye aliongeza kwa kusema, “inatupa shida
wakati mwingine, wakati hela inatakiwa tulipe kule bandarini, uwezo wa TANESCO
katoka makusanyo sio mzuri sana kutokana na madeni, hivyo kama tungeweza
kuruhusiwa kutoa vifaa hivyo bandarini, ingekuwa vema kwani kasi ya ukusanyaji
mapato ya TANESCO inapoongezeka ndivyo tunavyoweza kulipa lakini Mradi utakuwa
umeendelea.” Alisema Dkt. Mwinuka.
Mradi wa Kinyerezi I&II utakapokamilika,
utaweza kuzalisha umeme wa Megawati 425, Naibu Mkurugenzi wa TANESCO, Mhandisi
Khalid James aliwaambia wajumbe wa Kamati hiyo. “Megawati hizi zitaunganishwa
kwenye Gridi ya Taifa na hivyo kuongeza umeme.” Alisema Mhandisi James.
Mradi wa Kinyerezi I utagharimu kiasi cha Dola
za Kimarekani Milioni 188 huku Mradi wa Kinyerezi II ukigharimu kiasi cha Dola
za Kimarekani Milioni 344, aliongeza Mhandisi James.
Meneja Mkazi wa Mradi wa Umeme wa
Gesi wa Kinyerezi II, Markku Repo kutoka
kampuni ya Jacobsen Elektro(aliyenyoosha mkono), akifafanua mambo mbele ya wajumbe
wa Kamati wakati wa ziara yao. Wakwanza kulia ni Naibu Katibu Mkuu Nishati na
Madini, Dkt. Juliana Palangyo.
Wajumbe wakitembelea Mradi huo huku wakiongozwa na Meneja Msimamizi wa Mradi, kutoka kampuni ya Japani ya Sumitomo
Baadhi ya wajumbe wa Kamati hiyo, waksikiliza kwa makini maelezo yaliyokuwa yanatolewa na wataalamu wa TANESCO na wajenzi wa mradi huo
No comments:
Post a Comment