Pages

February 12, 2017

RC KILIMANJARO NA KAMISHNA MTEULE WA MAMLAKA YA KUZUIA DAWA ZA KULEVYA WATEMA CHECHE

Kamishna Mteule wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za kulevya,Rogers William akizungumza wakati wa uzinduzi rasmi wa mazoezi kwa wananchi mkoa wa Kilimanjaro,uzinduzi uliofanyika katika uwanja wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi.
Viongozi wa Serikali walioshiriki katika uzinduzi huo,kutoka kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Moshi,Kippi Warioba,Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Saidi Meck Sadiki ,Mkuu wa wilaya ya Hai,Gelasius Byakanwa na Katibu Tawala mkoa wa Kilimanjaro, Mhandisi Aisha Amour.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Saidi Meck Sadiki akizungumza juu ya Dawa za kulevya mara baada ya kumalizika uzinduzi rasmi wa siku ya mazoezi ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Makamu wa Rais ,Samia Suluhu Hassan.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,Kamishna msaidizi Mwandamizi wa  Polisi,Wilbroad Mutafungwa akitoa salamu za jeshi hilo katika uzinduzi huo.
Baadhi ya viongozi wakifuatilia hotuba ya mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,(hayupo pichani) 
Mkuu wa Wilaya ya Hai,Gelasius Byakanwa akisalimia katika uzinduzi huo.
Katibu Tawala wilaya ya Hai,Upendo Wela akitoa salamu wakati wa uzinduzi huo.
Mwakilishi wa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi,Dkt Cyril Chami akitoa neno la ukaribisho katika uzinduzi huo.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

SIKU chache  baada ya kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,Dkt John Pombe Magufuli kuwa Kamishna wa mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya (Drug Control and enforcement Authority), Rogers William ameanza kutema cheche dhidi ya Wafanyabiara na watumiaji wa dawa za lulevya.

Kamishna huyo  ametangaza kushughulika kikamilifu na baadhi ya wafanyabiashara mkoani Kilimanjaro,wanaowatumia wanawake wajasiriamali wanaosafirisha mazao kwenda mikoani, kubeba Mirungi ama Bangi ndani ya mizigo ya mazao.

William alitoa kauli hiyo wakati wa mazoezi katika uwanja wa Chuo kikuu cha Ushirika Moshi (MoCU) baada ya mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro , Saidi Mecky Sadiki kutoa nafasi kwa Mkuu huyo wa usalama wa taifa mkoa wa Kilimanjaro , baada ya kumpongeza kwa kuteuliwa kwake.

“Tunayo orodha ya wafanyabiashara wasio waaminifu na wengine wananchi wa kawaida wanaowatumia wanawake wasio na hatia kusafirisha dawa za kulevya kama Mirungi na Bangi kwenda mikoani….hilo nitahangaika nalo mara nitakaporejea mkoani hapa katika mapambano dhidi ya vita hii”alisema Sadiki.

Kauli ya William ilifuatia baada ya Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Saidi Meck Sadiki kulitaka jeshi la Polisi kufaya uchungizi wa kina ili kuwaachia baadhi ya wanawake watakaobainika kutokuwa na hatia ama kufahamu kama walitumika kusafirisha dawa za kulevya bila ridhaa yao.

Akizungumzia kuhusu Dawa za kulevya,Sadiki alisema vita dhidi ya dawa  za kulevya za aina mbalimbali kwa mkoa wa Kilimanjaro imeanza muda mrefu na tayari zaidi ya watuhumiwa
689 wa dawa hizo wanashikiliwa katika kipindi cha mwaka mmoja kuanzia Januari mwaka 2016 hadi Januari 2017.

Sadiki alisema vita hiyo ni ya kudumu yenye changamoto kubwa baada ya mkoa wa Kilimanjaro kuwa na njia nyingi za Panya katika mipaka baina ya Tanzania na Kenya, huku ikizingatiwa kwamba Kenya inalitumia zao la Mirungi kama biashara halali.

“Watuhumiwa walikutwa na makosa 626 ambapo watuhumiwa 103 walifikishwa mahakamani nakupata adhabu za aina mbalimbali ikiwamo vifungo na faini ambapo wawili miongoni mwao walifungwa vifungo vya maisha gerezani na kesi 136 zinaendelea mahakamani”alisema Sadiki.

Sadiki alisema kadhalika watuhumiwa wengine 296 walikamatwa na Tani nne za Mirungi, watuhumiwa wengine 284 walikutwa na kilo 424 za bangi, huku magari matano na pikipiki 20 zikishikiliwa na polisi kwa tuhuma za kusafirisha dawa za kulenywa aina ya Mirungi na Bangi.

”Tumekuwa tukiendesha kampeni ya kukabiliana na dawa za kulevya kila wakati na kampeni hii ni ya kudumu, nawaasa vijana kuachana na biashara hiyo na badala yake watafute biashara halali”alisema Sadiki.

Aidha mkuu wa mkoa aliwataka wafanyabiashara na watumiaji wa dawa za kulevya wanaokimbia msako jijini Dar es salaam kutokimbilia mkoani mwake kwani kampeni ni ile ile na watakamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria.


Mwisho.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...