Ramani ya kiwanda
Wa
kwanza kushoto mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, alhaj Magid Mwanga ,wa pili
kushoto mkuu wa mkoa wa Pwani, mhandisi Evarist Ndikilo na Jack Feng
mkurugenzi wa kiwanda, wa tatu kushoto ni waziri wa viwanda, biashara na
uwekezaji Charles Mwijage na Ridhiwan Kikwete na Cliford Tandari
wakiweka udongo kwenye jiwe la msingi.(picha zote na Mwamvua Mwinyi)
Na Mwamvua Mwinyi, Chalinze
Waziri
wa biashara, Viwanda na Uwekezaji, Charles Mwijage, amezitaka taasisi
zinazohusika na uwekezaji kutokuwa na ukiritimba ili hali kufikia
malengo ya serikali ya kukuza sekta ya viwanda.
Aidha ameeleza kwamba, wizara hiyo, imeweka mazingira mazuri ya uwekezaji ambayo yatawezesha kuvutia wawekezaji wa ndani na nje.
Hayo
aliyasema huko kitongoji cha Pingo Chalinze,Bagamoyo,wakati akiweka
jiwe la msingi kwenye kiwanda cha Vigae cha Twyford Ceramics Ltd.
Mwijage alisema, uwekezaji huo unaendana na dhana ya Rais Dk John Magufuli wa kuifanya nchi kuwa ya Viwanda .
Alisema kwa kuanzishwa viwanda vingi vya aina hiyo kutasaidia kuongeza pato la nchi na kuzalisha ajira kwa wingi.
“Zipo
idara ambazo zinafanikisha uwekezaji ikiwemo brela, idara ya uhamiaji,
kazi, mamlaka ya mapato TRA, wizara ya ardhi, shirika la viwango TBS,
baraza la Mazingira NEMC ambazo zinapaswa kufanya kazi kwa wepesi ili
kufanikisha uwekezaji,” alisema Mwijage.
Alisema kati ya idara hizo baadhi zimekuwa zikifanya vizuri lakini nyingine zimekuwa zikiwapa usumbufu mkubwa wawekezaji.
“Wizara
yangu haina tatizo lakini kuna baadhi ya idara zimekuwa kero na
ukiritimba usio na sababu .,naomba kama kuna idara zinakuwa kikwazo
niambieni ili tuwachukulie hatua,” alisema Mwijage.
Mwijage
alisema nchi zilizofanikiwa kukuza uchumi wake kupitia viwanda zimeweza
kutoa ajira nyingi kwa vijana kupitia sekta rasmi na isiyo rasmi.
Mkurugenzi
mkuu wa kiwanda hicho Jack Feng alieleza, kiwanda hicho asilimia 95 ya
malighafi itakuwa inatoka nchini ambapo kigae kinatumia maliahafi zaidi
ya 10.
Alisema
mara kiwanda hicho kitakapokamilika agosti mwaka huu kitaweza kupunguza
asilimia 30 ya uagizaji wa vigae toka nje ya nchi.
Feng
alisema wanatarajia kuajiri wafanyakazi 2,000 moja kwa moja na 4,000
kazi za muda na gharama ya mradi huo ni dola mil. 56 sawa na bil. 120 .
Alisema watauuza hadi nje ya nchi ikiwa ni pamoja na Zambia, Uganda, Rwanda na Burundi .
Nae
mkurugenzi mtendaji wa kituo cha uwekezaji Cliford Tandari alisema kuwa
uwekezaji wa kiwanda hicho ni wa mfano kwani utavutia makampuni mengi.
Alisema
kwasasa kituo hicho kimeweza kutoa wigo mkubwa katika kuandikisha
miradi mbalimbali toka china na kufikia miradi 667 ambayo itazalisha
ajira 83,141 kwa watanzania ,miradi 452 ni miradi inayohusiana na sekta
ya uzalishaji viwandani.
Mkuu wa mkoa wa Pwani Injinia Evarist Ndikilo alisema ,mkoa huo una viwanda 264 huku vikubwa vikiwa ni viwili.
Ndikilo alisema uwekezaji huo ni mkubwa na unatarajia kukuza ajira kwa vijana wa mkoa wa Pwani na Tanzania kwa ujumla.
Alisema
mkoa wa Pwani bado una maeneo makubwa ya uwekezaji na tayari kuna eneo
lenye ukubwa wa hekari 5,000 linahitaji wawekezaji .
Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete aliwapongeza wawekezaji hao kutoka nchi ya China .
Alisema Chalinze imejipanga kuwa sehemu ya uwekezaji ambapo kuna ujenzi wa viwanda mbalimbali.
Ridhiwani alisema kuwa changamoto kubwa inayokabiliwa wananchi na wawekezaji ni ukosefu wa maji,.
Alibainisha
wamekuwa wakijitahidi kuikabili lakini bado hawajafanikiwa kuidhibiti
aliomba wawekezaji hao kutoa ajira bila ya kuwabagua wenyeji.
No comments:
Post a Comment