Spika
Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa
Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Anne S. Makinda
akizungumza kwenye mkutano uliowakutanisha viongozi wa mashirika na
taasisi ili kujadili ukuaji wa uchumi 'Business Transforming Africa
Conference' ambao umeandaliwa na kampuni ya African Management Services
(AMSCO) ukiwa na lengo la kujadili umuhimu wa mafunzo kwa rasilimali watu katika kukuza uchumi.(Picha na Geofrey Adroph)
Naibu
Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Antony Mavunde akizungumza kuhusu
upatikanaji wa ajira katika nyanja mbalimbali hasa pale ukuaji wa
uchumi unapoimarika wakati wa kujadili ukuaji wa uchumi 'Business
Transforming Africa Conference' ambao uliwakutanisha dawau mbalimbali wa
ndani na nje ya nchi.
Mwenyekiti
wa Taasisi ya ATMS, Balozi Jan Berteling akizungumza jambo kwenye
mkutano huo uliowakutanisha viongozi wa mashirika na taasisi kuhusu
ukuaji wa uchumi 'Business Transforming Africa Conference' uliofanyika
katika ukumbi wa Hoteli ya Hyatt Recency jijini Dar.
Meneja
wa Heineken Afrika Mashariki na Kati, Kayode Adeuja akizungumzia jinsi
kufanya biashara na kukuza mtani kama kampuni hiyo ilivyoimarika wakati
wa kujadili ukuaji wa uchumi 'Business Transforming Africa Conference'
uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Hyatt Recency jijini Dar.
Mwezeshaji
wa Majadiliano Bi. Catherinerose Barreto(aliyesimama) akitolea
ufafanuzi moja ya jambo lililokuwa likijadiliwa katika mkutano huo
uliofanyika katika ukumbi wa Hotel ya Hyatt Recency jijini Dar
Baadhi ya wadau wakichangia mada kwenye majadiliano
Mwenyekiti
wa AMSC, Ali Mufuruki akizungumza na waandishi wa habari
walivyowakutanisha viongozi wa mashirika na taasisi ili kujadili uuhusu ukuaji wa uchumi 'Business Transforming Africa Conference'
Baadhi ya viongozi wa mashirika na taasisi mbalimbali wakifuatilia
majadiliano kuhusu ukuaji wa uchumi 'Business Transforming Africa
Conference' kwenye ukumbi wa Hyatt Recency jijini Dar
Spika
Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Anna Makinda
amesema ukuaji wa uchumi hauwezi kufikiwa endapo hakutakuwa na uwekezaji
wa kutosha katika mafunzo kwa rasilimali watu.
Mama
Makinda ameyasema hayo wakati wa Mkutano wa kujadili ukuaji wa uchumi
'Business Transforming Africa Conference' ambao umeandaliwa na kampuni
ya African Management Services (AMSCO) ukiwa na lengo la kujadili umuhimu wa mafunzo kwa rasilimali watu katika kukuza uchumi.
Amesema
hakuna usawa kati ya ujuzi unaotolewa mashuleni na mahitaji ya soko la
ajira jambo ambalo linachangia kwa kiasi kikubwa ukosefu wa ajira kwa
wahitimu wengi ambao hushindwa kukidhi mahitaji ya soko la ajira.
Kwa
upande wake Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Anthony Mavunde
alisema kuwa pamoja na jitihada zinazofanywa na wadau wote wanaoshiriki
katika kukuza uchumi ni muhimu kwa wadau hao kwenda sambamba na Mpango
wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano ili kuweza kufikia malengo ya
pamoja yaliyokusudiwa.
AMSCO imekuwa ikiandaa mikutano ya namna hii kwa lengo la kukuza uchumi wa taasisi, mashirika nchi kwa ujumla.
No comments:
Post a Comment