Mwenyekiti
wa Tamasha la Sauti za Busara Zanzibar Simai Mohammed Said akitowa
maelezo ya kukamilika kwa maandalizi ya Tamasha hilo kwa Mkuu wa Mkoa wa
Mjini Magharibi Unguja Mhe Ayoub Mohammed Mahmoud alipotembelea Ngome
Kongwe kujionea maendeleo ya matayarisho ya Tamasha hilo
litakalohudhuriwa na Wasanii wapatao 400 kutoka Zanzibar, Tanzania Bara
na Nje ya Tanzania kwa kutowa burudani ya Sanaa yenye ubunifu kwa
kutumia Tamaduni za Kiafrika. Hapo ni Jukwaa la amphitheatre.
Mkuu
wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Ayuob Mohammed Mahmoud akiwa na
Mwenyekiti wa Tamasha la Sauti za Busara Zanzibar Simai Mohammed Said
akimtembeza sehemu za kumbi zitakazofanyika kwa Tamasha hilo katika
Majengo ya Ngome Kongwe Zanzibar.
Fundi
Mkuu wa Tamasha la Sauti za Busara Zanzibar Hamza Omar Abbas akitowa
maelezo ya kukamilisha kwa ufungaji wa Vyombo vya Muziki na Umeme kwa
ajili ya matayarisho ya Tamasha hilo linalotarajiwa kufanyika tarehe
9-2-2017, wiki hii.
Mwenyekiti
wa Tamasha la Busara Zanzibar Simai Mohammed Said akitoa maelezo kwa
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud, wakati
alipofanya ziara kutembelea na kujionea maandalizi ya Tamaasha hiyo
wakiwa katika Jukwaa kubwa litakalotumika kwa Wasanii kutowa burudani
wakati wa maonesho mbalimbali ya Tamasha kwa Wasanii.
Fundi
Mkuu wa Tamasha la Busara Zanzibar Hamza Omar Abbas akimuonyesha vyombo
vya muziki vitakavyowawezesha Wasanii wakati wakiwa jukwaani wakiimba
kujisikia wenyewe sauti zao wakati wa show zikiendelea.
Mwenyekiti
wa Sauti za Busara Zanzibar Simai Mohammed Said akimuonesha ratiba ya
maonesho yote ya Tamasha hilo Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe Ayoub
Mohammed Mahmoud.
Mwenyekiti
wa Tamasha la Sauti za Busara Zanzibar Simai Mohammed Said akizungumza
wakati wa mkutano na wafanyakazi wa Tamasha hilo katika viwanja vya
mambo club ngome kongwe kwa ajili ya matayarisho ya Tamasha hilo.
Mkuu
wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe Ayoub Mohammed Mohamoud akizungumza na
wafanyakazi wa Tamasha la Sauti za Busara Zanzibar alipofika kutembelea
kujionea maandalizi ya Tamasha hilo na kuwataka kuitangaza Zanzibar kwa
wageni wanaotembelea kujionea maonesho ya Tamasha hilo la Tamaduni za
Kiafrika kuwakutanisha wasanii mbalimbali kutoka katika Nchi za Afrika.
Wafanyakazi
wa Tamasha la Sauti za Busara wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Mjini
Magharibi Mhe Ayoub Mohammrd Mahmoud akitowa nasaha zake kwa wafanyakazi
hao wakati alipofika kutembelea maandalizi ya Tamasha hilo
linalotarajiwa kufanyika keshokutwa Zanzibar tarehe 9-2-2017
Wafanyakazi
wa Tamasha la Sauti za Busara Zanzibar wakiwa makini kumsikiliza Mkuu
wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe Ayoub Mohammed Mahmoud alipofika
kutembelea na kujionea maandalizi ya Tamasha hilo kukamilika kwa
asilimia mia moja ya maandalizi yake.
Mkuu
wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud akiwa
katika picha ya pamoja na viongozi wa Tamasha la Sauti za Busara
Zanzibar.
No comments:
Post a Comment